- Thread starter
- #21
Bibie, matatizo ya watanzania siyo CHADEMA kukiri utoto au ujinga wa mtoto mwenzenu Nape. Matatizo ya watanzania yanatokana na sera mbovu za CCM, shule kukosa walimu, madawati na maabara, hospitali kukosa wataalam, dawa, maji, umeme na x-ray machines, wizi na ufisadi uliokithiri wa viongozi wa serikali ya CCM, kupanda bei kwa bidhaa zote, wakulima kukopwa mazao yao (korosho-Mtwara), viongozi wa serikali kukosa ubunifu na uongozi bora hivyo kuishia kuning'unika na kulalamika kila kukicha, na mbaya zaidi viongozi wa CCM kushindwa kabisa kutambua matakwa ya watanzania na badala yake kuanza kuwatumia wajinga kama wewe kushinda mitandaoni kutetea uvundo na umaskini wa fikra za CCM! Nakuhakikishia CCM haitapendwa na wananchi kwa propaganda za kichovu kama hizi, badala yake serikali yake itatue matatizo ya wananchi wake. Na wewe hutaisaidia CCM kwakushinda unaandika huu ujinga wako hapa jamvini! Poleni sana watoto.
Ni kweli lakini tambua kuwa hata leo hii CCM wakiitisha mkutano wananchi watakuja wengi kuliko unavyofikiri wewe mmoja au hujalijua hilo. Uchukiavyo wewe si kama nichukiavyo mimi na yule. Slaa kwenye uchaguzi uliopita alisema hamtambui Kikwete kwa sababu ameibiwa kura, lakini hadi sasa amekuwa kimya na wakati wakiri wa Serikali alisema wazi mahakamani kwenye kesi ya Lema kuwa anayetakiwa kufungua mashitaka juu ya uonewaji wa uchaguzi ni mhusika mwenyewe au Slaa si muhusika mwenyewe anasubiri wananchi tuandamane kwa shinikizo lake?