CHADEMA wamfungulia kesi Nape

CHADEMA wamfungulia kesi Nape

Nyie si mliwachamba majaji pale bungeni sasa mnapeleka kesi zenu huko huko ,nakumbuka mliwasema sana pale bungeni na kuwapaka mivi ,iweje leo muwapelekee kesi yenu.Hiyo kesi ni jiwe lingine mtakalopigwa nalo.CDM hamna mnapokwenda ,hivi mnaielewa Tanzania na utawala wake au mnajiendea mkipapasa kama kipofu aliepoteza bakora.

Ukisikia Chama kinachowaburuza wanachama wake na kutojua kinachofanya basi ni CDM ,hawaelewi jana wamekula kitu gani ! Poleni sana.

Majaji ni walewale mliowavua nguo pale bungeni.

Hivi ile kesi ya Uchaguzi mdogo wa Igunga ilisimamiwa na Mahakama gani vile? Wewe inaonekana hujui hata ulisemalo! Maneno ya Tundu Lissu kuhusu Mahakama zetu na Majaji wake haiwezi kuzuia Haki za msingi za chama au Mwana-CDM yeyote.Hatuwezi kuwekewa Majaji kwenye Mahakama zetu ambao hawawezi kuamua kesi yoyote au kama wakitoa uamuzi ni kwa maelekezo ya Kiongozi fulani wa CCM au Serikali yake. Tunataka utawala wa sheria na siyo sharia!

Tundu Lissu alizungumza ukweli na ushahidi uko kwenye maandishi ukiwa umeandikwa na Majaji hao hao ambao hawakubalini na uteuzi wa kijinga unaoangalia udini,ukoo,ukabila na urafiki! Uteuzi wa aina hii unaofanywa na rais wako Kiwete unaenda kwa mfumo huo na kwa maana hiyo uteuzi huo hauna tija kwa Taifa sana sana unazidi migogoro na migongano ya kiutawala.
 
huyo mnyiramba nape a.k.a napegwa anatudhalilisha siye wanyiramba kwanini lakini?wote hata huyu nchemba madelu wanatia aibu.eti majesh yameapa kukilinda chama cha mapinduzi,mh haya,
 
Yes! very nice move, now we will be able to see who is telling the truth.
 
Hata kama jaji akipendelea ni ngumu kwani cdm kuna mawakili bingwa sana, Marando, Lisu, profesa safari watakoma!
 
ukisha ona unashindwa lazima utafute maneno mengi, CCM Hata siku moja haikurupuki, unawaona walioko CCM Lakini? CDM kuna nani? labda ZITTO TU ALIYEWAAMBIA CDM WENZAKE HAKUNA MSOMI KAMA YEYE, AND ITS TRUE, Ztto akitoka cdm kwisha,, Mwambie lema alienda UINGEREZA KUKAGUA MAHELKOPTA ALIKUWA ANAKUJUA, AU NDIO ANAJINADI AJIJENGE YEYE PAMOJA NA MBOWE NA FAMILIA ZAO? HUU NI MOTO WA KIFUU, WATANZANIA WANA AKILI SANA ,,,ENDELEENI KUANDAMANA WAKATI WENGINE WAKO KWENYE UTENDAJI!
Endelea kuhara hapa ccm ni full aibu kotekote,mmeanzisha operesheni yenu ya kuua raia na kuisingizia chadema mkitegemea wananchi watawa support,raia wakawashtukia,waandishi nao wamewageuzia kibao,waalimu hawawataki,ma doctors ndio kabisaa sasa mmemtelekeza nape awabebee madhambi yenu,mwaka huu kazi mnayo.
 
Afadhali huyu kibaraka ajibu hizo tuhuma zake mbele ya pilato. Maana anafanya siasa za propaganda bila kuelewa dunia ya sasa ni ya utandawazi (siyo ufunga siri). Inabidi athibitishe kauli yake. Na kama anamtegemea JK amekwisha, ajaribu kukumbuka na kujikumbusha juu ya Mgosi (baba Januari) alivyokuwa mropokaji na JK alimshangaa mpaka akamkatalia kwenda kuongea na maaskofu (alimwambia, yaani wewe ukienda mropokaji hivyo.....).
 
huyu nape anapenda sana umaarufu, ila njia anazotumia zinamgarim.
Hazimgharimu yeye mkuu!zinakigharimu chama chake,nape hana anachopoteza so far,mwenyekiti wake alimkoromea atoke akapambane na operesheni za cdm,huku yeye(mwenyekiti)akipaa kwenda ughaibuni kula bata,sasa dogo anaamua kuharibu jumla,anaropoka chochote kinachojaa mdomoni.
 
Wakuu, hivi inawezekana kesi hii ikaunganishwa na ile ya Mukama kudai kuwa Chadema wameleta magaidi toka Libya kuja kufanya fujo uchaguzi wa Igunga?
 
Ndugu Mahesabu with all due Respect sidhani kama hao Wanasheria wa Pro CCM uliowaorodhesha kama unawafahamu vyema.

1. Said Elmaamry - Huyu yuko bize sasa hivi kuhakikisha Mzee mwenzake Idd Simba haendi jela kwa kesi ya kutolewa sadaka na CCM wenzake. hapa usitegemee msaada wa Elmaamry.

2. Nimrod Mkono - huyu kila mtu anamfahamu vyema hana muda wa kujihusisha na kuharibu credibility yake kwenda kumtetea mtu ambaye inajulikana wazi huwa anaanza kuongea halafu ndio anafikiri. Mkono yeye anadeal na wezi wakubwa kabla hawajaiba yeye anawapa ushauri wa kisheria namna ya kujidefend kama kikinuka, mfano hai Rostam Aziz na Dowans yeye kila sehemu eti ana Power of Attorney lakini si mmiliki!!

3. Masumbuko Lamwai - Huyu ni sawa anaweza kwenda kusimama Mahakamani maana zama za kitabu chake zilishapita na mtu ukimuuliza kama kuna Wakili anaitwa Lamwai sidhani kama atakujibu, kwa kifupi Lamwai sasa hivi ni mahiri na gwiji la kunywa pombe na siyo sheria.

Mkuu Matola heshima mbele,
In addition to that, kuna watu wanamshauri Nape Nnauye amfuate Andrew Chenge amtetee. Wanasahau kwamba Chenge ni Pro-Lowassa na Nape Nnauye ni Anti-Lowassa. Kwa namna yoyote vile ni vigumu Chenge kumtetea Nape Nnauye. The same applied to Nimrod Mkono. Huyu ni Pro-Mafisadi, kwa hiyo vigumu amtetee Pro-Kujivua Gamba.

Yani cha kumshauri Nape, amtafute labda Joseph Thadayo au Marehemu Masumbuko Lwamwai.

TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
 
nape hana ushahidi kam cdm wanapewa pesa toka nje....mdomo umemponza
 
Tupo pamoja Radhia. Hakika tumekuwa watu wa kuchomekewa mauza uza kila siku, Katiba mpya watu wameipotezea, Ishu ya fao la kujitoa kwa mifuko ya jamii tumesahau, mauji yanayofanywa na polisi kimya kimya yanapotea, nategemea mpaka wiki ijayo tutakuwa tumesahau, migomo ya madaktari na walimu tumesahau zamani, mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha imekuwa wimbo uliosahaulika! Tunahamia kwa malumbano ya Nnape na CDM, yanatija gani kwa taifa? Let say Nnape amekutwa na hatia, na akalipa hiyo 3bn, mlalahoi wa kule kwetu Ngadinda au Ndapata atanufaikaje?

liache kuropoka
 
Back
Top Bottom