CHADEMA wamfungulia kesi Nape


Naona kama vile mwisho wa Nape umefika coz hata mzee wa Kaya baba Mwanaasha kama vile keshachoka kimtindo
 
Nape inabidi umtafute Masumbuko Lamwai mjifungie nae chumbani mwezi mzima

hapa kila goti litapigwa .... ukome kuropoka
 
Kumbe wana Imani na mahakama hizi,siasa kweli noma,haki unaposhinda,ukishindwa hakuna

Ngoma kwa Nape is to be ready to prove beyond reasonable doubt.Hii phrase ya kisheria huwaga inanimaliza, kwani kama umetoa pumba shughuli unakuwa nayo
 
Nyie si mliwachamba majaji pale bungeni sasa mnapeleka kesi zenu huko huko ,nakumbuka mliwasema sana pale bungeni na kuwapaka mivi ,iweje leo muwapelekee kesi yenu.Hiyo kesi ni jiwe lingine mtakalopigwa nalo.CDM hamna mnapokwenda ,hivi mnaielewa Tanzania na utawala wake au mnajiendea mkipapasa kama kipofu aliepoteza bakora.

Ukisikia Chama kinachowaburuza wanachama wake na kutojua kinachofanya basi ni CDM ,hawaelewi jana wamekula kitu gani ! Poleni sana.

Majaji ni walewale mliowavua nguo pale bungeni.
 

Ni vizuri pia angefunguliwa kesi ya Mauaji Morogoro kwa kuwa alinena na yakatokea. Ushahidi wa kimazingira.
 
hapo ndio watadhihirisha kuwa wako.makini
 

SI majaji wote waliovuliwa nguo bungeni, isipokuwa tu wale waliopewa nafasi hizo kwa ajili ya ulaji na CCM bila kuwa na sifa stahiki
 
...sipendi nionekane kama mtabiri(shek Yahaya)...mimi ninavyoitazama hii kesi,uko mbele itabadilika kutoka CDM v/s Nape(CCM) na kuwa Tanzania v/s hizo nchi Nape atakazo zitaja...ni raisi sana kuanzisha vita lakini nivugumu sana kumaliza vita...Nape huo ujinga uliolopoka utaharakisha sana safari yenu ya kutoka madarakani...
 
Hapo ni pazuri sana, Nape anakwenda kuwaaibisha vibaya sana. Mtanambia.
You're msg is simple & clear, System at work. kwahiyo ni kichaa pekee ndio atakayepata tabu ya kujadili lolote la maana na wewe.
 
Ni wakati wa Chadema kuumbuka. Nape atakuja na ushahidi wa kutosha.

Ushahidi upi? Wa kupika? Maana Nyinyiemu kwa kupika hawajambo!!! Hata mkigushi CDM watapandia huko huko wakahakiki!! Chezea CDM wewe.
 
Pamoja na kuwa waliwasema majaji Vihiyo haimaanishi kuwa wasipeleke kesi zao Mahakamani. Kumbuka kuwa Wanahaki ya kuwakataa majaji ambao wanaona wanaweza kuhujumu kesi zao. Sheria inaruhusu hata Mahakama kuomba majaji wengine toka nchi wanachama wa jumuia ya Madola na sasa nafikiri hata kutoka nchi za EAC wakaja na kuiendesha kesi hiyo.
 
je akileta ushahidi unaoonyesha kuwa kweli pesa zilitolewa ila hakunamakubaaliano ya kuwapa rasilimali?
je waliotoa wakidhibitisha kuwa hawadai chochote?
je akishindwa hata kudhibitisha kuwa hakuna hata hela iliyopokelewa?

naomeni wanasheria mnifafanulie hukumu za hayo maswali hapo?
 
Ona sasa umeanza kujinyea kabla hata kesi haijaanza!! We umeambiwa CDM imemfungulia mashtaka nape nnauye! Wewe unaanza kututishia kujuta!!ooh mara mnyika kasoma bba sjui upuzi gani!!! We mbwira kwelikweli.
 
Matumizi mabaya ya rasilimali, hakukuwa na haja ya kumfungulia kesi labda kama watu wanatengeneza mazingira ya kupiga hela ya chama. Kama umahili wa wanasheria si bora wangewasaidia wananchi wanaosota na kesi na hawana hata msaada wa kisheria, hii itakuwa kesi kama ya mengi na manji wanaodaiana sh. 1 na wakifika mahakamani kesi zote zinasimama kuwapa nafasi wauza nyago watokee katika media na wasio na hatia wanarudi tena lupango.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…