Kutokana na vyanzo vyangu vilivyopo Mahakama kuu ya Tanzania Leo Nape amefunguliwa kesi ya madai na imepewa namba 186 ya mwaka 2012.
Kesi hii ni kuhusiana na madai ya nnape kuwa CDM wana pokea pesa kutoka nje ya nchi.
Tuendelee kufuatilia
Updates.
Inaitwa civil case no.186 of 2012 ,board of registered trustees of chadema ... Plaintiff versus nnape nnauye defendant .
Hivi ile kesi ya Uchaguzi mdogo wa Igunga ilisimamiwa na Mahakama gani vile? Wewe inaonekana hujui hata ulisemalo! Maneno ya Tundu Lissu kuhusu Mahakama zetu na Majaji wake haiwezi kuzuia Haki za msingi za chama au Mwana-CDM yeyote.Hatuwezi kuwekewa Majaji kwenye Mahakama zetu ambao hawawezi kuamua kesi yoyote au kama wakitoa uamuzi ni kwa maelekezo ya Kiongozi fulani wa CCM au Serikali yake. Tunataka utawala wa sheria na siyo sharia!
Tundu Lissu alizungumza ukweli na ushahidi uko kwenye maandishi ukiwa umeandikwa na Majaji hao hao ambao hawakubalini na uteuzi wa kijinga unaoangalia udini,ukoo,ukabila na urafiki! Uteuzi wa aina hii unaofanywa na rais wako Kiwete unaenda kwa mfumo huo na kwa maana hiyo uteuzi huo hauna tija kwa Taifa sana sana unazidi migogoro na migongano ya kiutawala.
hapo kwenye red ndio tatizo sio nyinyiem ila ni wao em, Gosbertgoodluck ukisema nyinyiem unamaanisha sisi wasomaji wakati mimi sipo huko naomba utumie wao emProf. Safari, Lissu na Marando ni kikosi kamili cha ushindi dhidi ya Katibu Mwenezi wa NYINYIEM.
tusubiri tuone majingambo ya kilazi Nape maana nilimuona amevaa miwani utazani sio Mtanzania kumbe ni kichaa mmoja asiyejua nini anafanya
Ni wakati wa Chadema kuumbuka. Nape atakuja na ushahidi wa kutosha.
Tundu A. Lissu, Prof. Safari, Mabere Nyaucho Marandu etc. Je CCM watamlipia hizo Billion 3?
Anasimama na Lissu Mahakamani pembeni kuna Prof.Safari au kuna kitu gani kwa upande wa Chadema ? Na hii ndiyo watanzania watajua kwamba Chadema wako serious sasa .Komesha kuropoka bila ushahidi .Marando am sure hatakosa hapa kuongoza kuutafuta ukweli .
Matumizi mabaya ya rasilimali, hakukuwa na haja ya kumfungulia kesi labda kama watu wanatengeneza mazingira ya kupiga hela ya chama. Kama umahili wa wanasheria si bora wangewasaidia wananchi wanaosota na kesi na hawana hata msaada wa kisheria, hii itakuwa kesi kama ya mengi na manji wanaodaiana sh. 1 na wakifika mahakamani kesi zote zinasimama kuwapa nafasi wauza nyago watokee katika media na wasio na hatia wanarudi tena lupango.