Bramo
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 13,252
- 10,248
vijana wameichoka chadema
Vijana tunakutaka wewe maana huko Nyuma umejaaaliwa haswaaa
vijana wameichoka chadema
I agree with you to some extent!!... Lakini haka (kama kapo) ni kasababu kadogo sana miongoni mwa sababu kubwa nyingi za upinzani kushindwa na kugaragazwa ktk chaguzi nyingi zilizopita kwa maana ya ule mkubwa wa 2010 na zingine ndogondogo zilizofuata japo katika baadhi ya majimbo na kata upinzani uli - prevail.
Kwa hili hata tusidanganyane kabisa kwani si CHADEMA tu bali ni chama chochote kingine kinachoweza kuinuka leo au kesho, ni vigumu na hakitaweza kupambana kwa usawa na chama dola ambacho kwa sasa ni CCM chini ya mifumo ya uchaguzi hii tuliyonayo!!.
Wewe unafikiri kwa nini kwa sasa kuna misuguano mikali (between two oppossing sides...upande unaotetea mabadiliko na usawa katika jamii ya kitanzania chini ya UKAWA na upande unaotetea mfumo kandamizi wa kidemokrasia uliopo sasa ambao ni hawa watawala chini ya chama chao CCM) katika harakati za kuandika katiba mpya kuanzia katika mchakato wa awali kabisa wa sheria yenyewe,uundwaaji wa tume,ukusanyaji maoni ya wananchi uliokuwa unafanywa na Tume ya mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji Warioba,Mabaraza ya Katiba,Rasimu ya 1 na ya 2 ambayo sasa ndiyo iko huko Dodoma kwa hatua za mwisho kujadiliwa na kupitishwa na BMLK kabla ya kuletwa kwetu wananchi kuamua kama iwe au isiwe??
Jibu ni simple sana katika swali hili, kwamba, wanufaika wa mfumo huu wa demokrasia kandamizi isiyo na usawa wanafahamu fika kwamba si ELIMU YA URAIA wala sababu nyingine yoyote kwa sasa inayoweza kuwafanya washindwe katika uchaguzi wowote uliopo mbele yao, bali ni KUBOMOLEWA kwa mfumo unaowarahisishia kushinda kirahisi katika chaguzi ndogo zijazo na uchaguzi mkuu wa 2015!!......
Kwa hiyo watahakikisha kwamba na tena kwa gharama yoyote (hata kwa damu) kuwa mchakato huu wa uandishi wa KATIBA YA WANANCHI ambao kwa kweli ndilo kombora pekee litakalowaangamiza na kuubomoa mfumo wao walioujenga kwa takribani miaka 50 wanauhodhi na ndicho kilichofanyika!!..Na kiukweli KATIBA YA WANANCHI hii ambayo ina kila dalili ya kutopatikana ndiyo iliyokuwa njia pekee na sahihi ya kuleta mfumo mpya wa USAWA na HAKI katika nchi hii aidha tukiwa na muungano wetu huuhuu au nje ya Muungano.
Na hii maana yake ni kuuporomosha mfumo unaowanufaisha wao na familia zao,na rafiki zao,na jamaa zao na wale wanaowaunga mkono ambao ni wachache sana lakini kwa kuwa wana nguvu ya dola na fedha wanaweza kuishinda NGUVU YA UMMA tusipokuwa makini!!
Mengine yote ni kujidanganya na kucheza mchezo wa kombolela tu, otherwise tutaendelea kushindana na hawa jamaa ktk mazingira hayahaya magumu ambamo wanahodhi kila silaha ya ushindi na ikitokea mahali wapinzani wao bila kujali ni CHADEMA au chama kingine kimeshinda ujue kwamba basi mahali hapo wananuka kupita kiasi na hawakubaliki hata kwa fedha na polisi na usalama wao wa Taifa!!
Khaa!!! Ni ujinga wa hali ya juu kudhani watanzania wanahitaji mabadilikko ya siasa. Watanzania wanahitaji mabadiliko ya uchumi na mgawanyo ulio wa haki wa rasilimali za nchi. CCM ni afadhali kuliko Chadema. Hii inathibitishwa na mgao wa ruzuku zinazotolewa kutokana na kodi zetu ndani ya chama. Sasa hapa tukiwapa dola itakuwaje??? Angalia halmashauri zinazoongozwa na Chadema ni vurugu tupu hakuna mipango inayofanikiwa kwasababu hakuna muda wa kufanya kazi. Sasa hawa tukiwapa nchi itakuwaje?? Mabadiliko ya siasa yanahitajika na wale majobless wewe uchu wa madaraka na tamaa ya mali bila kufanya kazi ya uzalishaji. HATUDANGANYIKI
CDM imebaki mifupa tu hamna kitu tena.
Unaongelea IKULU GANI???????
lambda ya DULUTI........... kama unaongelea ya magogoni!! Pale MBWA HATII MGUU
![]()
Tanesco has been forced to shut the Mtera Dam due to the drought situation facing the country. I think we now need windmill farms in some parts of the country as we cannot continue to rely on rains.
ACT ndio chama kinachopendwa na vijana sasa hivi
Kuhusu Urais, kati ya uchaguzi ambao utakuwa ni rahisi kwa chama tawala, basi ni wa 2015.
Upinzani ninaouona upo ndani ya CCM yenyewe ni nani agombee urais.
Chadema haiwezi kusimama 2015 ikiwa na nguvu kama ile ya 2010. chadema imejiharibia yenyewe.
si kweli kuwa katiba mpya inaweza kusaidia chama cha upinzani kupata ushindi
hii ni kwa sababu wanainchi wa vijijini hawajui nini faida ya katiba kwa maisha yao ya siku za usoni
haya ninaypyasema ninauhaika kwa sababu mi nipo kijijini ila we nahisi uko mjini na unayoyasema ni ya watu wenye elimu
nasstza kuwa katiba itakuwa na mchango mdogo sana 2015 kama watu hawatapewa elimu ya uraia
act ni mnyama gani?
Duuh, kwani ni nini maana na tafsiri ya "kuishi mjini" na "kuishi kijijini" ndugu yangu?
Binafsi sioni tofauti yoyote kwa sbb kote huko wanaishi watu na kote huko wapo wajinga,wapumbavu na werevu pia!!
Muhimu ni uelewa na ufahamu wa mambo haijalishi unaishi katika eneo lenye hadhi ipi!.
Na ni hivi, labda ili tuelewane wote jipe muda kidogo wa kujielewesha maana ya "KATIBA YA WANANCHI". Baada ya hapo utakuwa katika nafasi nzuri sana kufahamu nafasi ya hiyo katika nyanja zote za maisha ya kila mtu kwa maana ya nafasi ya katiba katika mambo ya;
- Kijamii
- Kisiasa
- Kiuchumi
- Kiutamaduni
Nifahamuvyo mimi kukiwa na hakuna utaratibu mzuri wa namna ya kujitawala (siasa) hakika hutakuwa na uchumi imara,utakuwa na jamii iliyoparanganyika utakuwa na utamaduni ulio - shoboka. Hii yote inatokana na nini?
Ni katiba tu mkuu; na katiba kwa kukusaidia ni mfumo wa makubaliano uliatengenezwa na wananchi wenyewe ya namna watakavyoendesha shughuli zao za kiutawala (kisiasa),kiuchumi,kijamii na kiutamaduni katika nchi yao.
Na kama umenisoma vizuri katika post yangu,hakuna mahali popote nilipoandika kuwa katiba itawasaidia wapinzani kupata ushindi bali nimeandika kwamba si tu ELIMU YA URAIA pekee inayoweza kuwapa ushindi CHADEMA au chama chochote cha upinzani katika mazingira ya sasa ya siasa za ushindani zikiongozwa na chama dola CCM bali ni KUJENGA MFUMO MWINGINE UTAKAOLETA UWANJA ULIOSAWA WA USHINDANI!!..
Na fursa ilikuwa ni hii ya kujiandikia KATIBA MPYA (inayozingatia maoni ya wananchi wenyewe badala ya ile ya 1977 iliyoandikwa na watawala wenyewe kwa manufaa yao), ambayo,watawala chini ya CCM kwa makusudi na kwa kujua kuwa pengine yaweza ukawa ndio mwisho wao wa kushika hatamu za kutawala nchi hii wameuhodhi kuanzia katika hatua za awali kabisa. Na lengo lao ni mojatu waendelee na mfumo huu wa sasa unaowapendelea na kuwanufaisha wao chini ya katiba ya 1977!!
act ni chama makini cha siasa mkuu
ACT ndio habari ya mujini
mwaka 2015 ni mwaka ambao watu wengi wanaizungumzia kwa namna tofautitofauti
kuna wanaotamani mwaka wafike haraka ili washudie mabadiliko katika siasa za nchi,
kuna wengine hawaitamani mwaka huo ufike wakiwa hai kwa sababu wanafikiria yale ya kenya yasije kuwakuta kulingana na hali halisi ya sasa katika ulingo wa siasa
kuna wanaohamini kuwa hamna jipya litakalotokea bali ni ni ccm tena.
watz wote tunaamini kuwa kwa sasa ukitaka kujadili siasa ya tanz hauwezi kuacha kuzungumzia vyama viwili(ccm na CHADEMA)iwe kwa mazuri au kwa mabaya,iwe unazipenda ama la,uwe mwanasiasa ama la!
kwa muktadha huo ukweli ni kuwa 2015 hatuwezi kuzungumzia chama kingine chchote kushika dola tofauti na hivyo
kutokana na hali hiyo wafuasi wa vyama wamekuwa wakijinasibu kuwa wanauhakika wa ushindi 2015
mimi napenda jambo ambalo ni ya kawaida sana lakini ndio yenye ukweli wa ushindi uchaguzi ujao
kwanza ni lazima tukubaliane wote kuwa ccm ina nguvu vijijini hasa kwa akina mama na wazee na cdm wana nguvu kwa vijana wote si mjini wala vijijini,,
kwa hali hiyo cdm wanamini kuwa vijana watakapoandikishwa watskuwa na uhakika wa ushindi
ili jambo si kweli hata kidogo kwani hata ss cdm wanawafuasi vjn wenye miaka zaidi ya 25 lkn kwann bado wanashindwa vibaya hasa vijijini???
jibu ni moja kuwa VIJANA WENGI WA VIJIJINI HAWANA ELIMU YA URAIA
ninaposema elimu hiyo ni kuwa hawaoni sababu ya kupiga kura zaidi ya kushangaa elikopta na ksema people powerrrrrr
vijana wengi wa vijijini wamepoteza shahada na wengine wametupa kwa makusudi na wengine wanapewa pombe then wanambiwa walete shahada
ili jambo nina uhakika nao na nimelifanyia utafiti vya kutosha hasa mkoa wa ddma na musoma vijijini na singida
ss basi cdm wafanye jambo moja tu, nalo ni kufundisha elimu ya uraia kuhusu SHAHADA YA MPIGA KURA.
Wakifanikiwa hilo ikulu njia nyeupeee.
dhambi ya kumbagua zito inaitafuna chadema
Khaa!!! Ni ujinga wa hali ya juu kudhani watanzania wanahitaji mabadilikko ya siasa. Watanzania wanahitaji mabadiliko ya uchumi na mgawanyo ulio wa haki wa rasilimali za nchi. CCM ni afadhali kuliko Chadema. Hii inathibitishwa na mgao wa ruzuku zinazotolewa kutokana na kodi zetu ndani ya chama. Sasa hapa tukiwapa dola itakuwaje??? Angalia halmashauri zinazoongozwa na Chadema ni vurugu tupu hakuna mipango inayofanikiwa kwasababu hakuna muda wa kufanya kazi. Sasa hawa tukiwapa nchi itakuwaje?? Mabadiliko ya siasa yanahitajika na wale majobless wewe uchu wa madaraka na tamaa ya mali bila kufanya kazi ya uzalishaji. HATUDANGANYIKI