Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Ndugu zangu,
Katika hotuba yake ya kwanza bungeni ambayo wabunge wa Chadema walisaini posho na kisha kwenda kuingalia kwenye baa Raisi John Magufuli aliahidi kusimamia ukusanyaji wa mapato kupitia TRA ambapo kipindi hicho makusanyo yalikuwa ni wastani wa shilingi za kitanzania bilioni 800 na miezi iliyofuata kweli tukaona ukusanyaji ukiongezeka kufikia wastani wa zaidi ya shilingi Trilioni moja kwa mwezi.
Ajizi nyumba ya njaa,wakaanza kuibuka wapiga ramli wakiongozwa na KUB Mbowe wakisema "TRA inakusanya malimbikizo ya serikali ya awamu ya nne na wakiendelea hivyo itafika siku serikali haitakusanya hata senti kwani biashara zote zitakufa"
Leo zaidi ya miaka minne baadaye tunashuhudia mapato kuimarika kiasi cha kufikia shilingi trilioni 1.9 kwa mwezi Disemba 2019 hii ikiashiria sasa TRA wanakusanya zaidi ya mara mbili kwa mwezi ukilinganisha na miaka minne iliyopita.
Je kuna haja ya kuzingatia maoni ya kambi ya upinzani? Ni kweli kambi ya upinzani inaundwa na watu wenye "akili kubwa"?
Sent using Jamii Forums mobile app