LoyalTzCitizen
JF-Expert Member
- Sep 15, 2010
- 2,234
- 882
Ben Komba/Pwani-Tanzania/Monday, January 10, 2011/22:11:41
Chama cha demokrasia na maendeleo mkoani Pwani kimevunja mkutano wake wa hadhara uliokuwa ufanyike katika kiwanja cha Maili moja mjini Kibaha kutokana na ilichodai kujionyesha wazi kwa Polisi kutaka kuvuruga mkutano huo, baada ya kugundua mpango wa kuingiza Polisi zaidi kutoka maeneo ya jirani.
Akiongea na mwandishi wa habari hizi Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Pwani, BW. BUMIJA SENKONDO amesema taarifa za uchunguzi uliofanywa na vijana wao uligundua mpango mzima wa Polisi kuanzisha vurugu kwa makusudi ili waweze kuwadhalilisha na kuwashambulia wanachama na viongozi wa chama hicho kama walivyofanya Arusha , hali ambayo anasema inachochochewa na Katibu wa CCM, BW. YUSSUPH MAKAMBA kwa sababu ambazo mpaka sasa hazipo bayana kwa kukataa kuzungumza na CHADEMA kama alivyonukuliwa na vyombo vya habari.
BW. BUMIJA amebainisha uzoefu kwa chama chao ni kulindwa na maaskari watano, sasa iweje leo wapatiwe askari zaidi ya mia mbili kwa ajili ya ulinzi, na wengine wao wakionekana katika makao makuu ya Jeshi la Polisi mkoani Pwani wakiwa wanajiandaa kukabiliana mkutano wao usiku wa kuamkia siku ya mkutano wao , kitu ambacho kiliwastua na kuamua kusimamisha kufanyika kwa mkutano huo wa hadhara ambao ungehudhuriwa na wagombea nafasi mbalimbali za uwakilishi kupitia tiketi ya chama hicho kutoka Tanzania nzima ambao walishindwa.
Mbali na tukio la kuhairishwa mkutano wa hadhara ambao ulikuwa ufanyike katika kiwanja cha Maili Moja kutokana na hofu ya viongozi wa chama hicho na kutokana na walivyojifunza kutokana na tukio la Arusha, ambapo watu watatu walikufa na wengine kadhaa kujeruhiwa, viongozi kadhaa wa kitengo cha vijana wa CHADEMA wamekamatwa usiku wa kuamkia Jumatatu saa nane usiku kwa kilichodaiwa kuvunja vijiwe vya CCM.
Waliokamatwa ni mwenyekiti wa vijana Jimbo la uchaguzi Kibaha mjini. BW. ISAAC na BW. MATIMBWA
Akiongea katika wakati tofauti mkuu wa wilaya ya Kibaha, HAJAT HALIMA KIHEMBA amewaasa wapinzani kuacha kufanya maandamano kama inavyoamriwa na jeshi la Polisi ili kuepusha vurugu zisizo na lazima, amesema wao kama serikali wasilaumiwe kuwa ni wabaya.
Amesema wana usalama wana utaalamu wa kutosha katika tasnia hiyo, hivyo wanapogundua hali inayoweza kuhatarisha usalama wa raia na mali zao, hivyo amewasisitiza wananchi kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Jeshi la Polisi na hasa wakizingatia malengo na utaalamu wao katika masuala ya ulinzi na usalama, ameviambia vyama vya siasa kuwa wanarusiwa kufanya vikao lakini sio maandamano.
END.