CHADEMA, wakati mwingine muwe mnakubali ushauri

Mwananchi wa chini

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
227
597
Na Thadei Ole Mushi.

WAKATI MASHA ANAONDOKA CHADEMA NILIANDIKA HAYA.

Binafsi naelewa dhana ya vyama vya upinzani nchini kuwa ni kuharakisha maendeleo. Pamoja na kwamba mimi si mwanachadema na huwa naisema Chadema ila kwa namna moja au nyingine kina mchango mkubwa sana katika kuharakisha maendeleo nchini.

Ni ukweli usiopingika kuwa Chadema na vyama vingine vya upinzani kwa umoja wao vimekuwa vikisukuma maendeleo ya nchi hii na ndio maana huwa natamani vikue na vije na agenda nzito ili serikali isilale usiku na mchana ihangaike kutuletea maendeleo. Leo hii tukirudi kwenye mfumo wa chama kimoja tutarudi kule kule tulipotoka...

Kwa sasa kuna hatari kubwa inakinyemelea chama cha chadema na inahitajika busara ya juu sana kukinusuru kutokana na balaa hilo.

Kwa sasa chadema kuna watu wanawinda nafasi ya uenyekiti wa chama. Wanaotajwa sana kwenye mbio hizo ukimtoa Mbowe ni:-

1. Lisu.

2. Sumaye.

3. Lowassa.

4.Laurence Masha.

5.Mbowe

Kwa mujibu wa katiba ya chadema ibara ya 6.3.2 kipengele cha "C" kinasema nanukuu "Kiongozi anayemaliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi" mwisho wa kunukuu.

Kwa mujibu wa ibara hiyo mheshimiwa sana MBOWE naye yumo kwenye mbio za kugombea tena kiti hicho.Nimepitia katiba yote ya Chadema hakuna mahali ambapo muda wa kukoma kuongoza umetajwa. Ila ibara ya 6.3.4 inaelezea mazingira ya kiongozi kukoma uongozi wake ambapo vipengele vyake vinasema:-

a) Kama kiongozi atajiuzulu mwenyewe

b) Kama kiongozi ataachishwa uanachama

c) Kama kiongozi atashindwa kutimiza majukumu yake

d) kwa kufariki.

Hakuna mahali ambapo katiba hii ianasema kuwa kama kiongozi ametumikia nafasi yake kwa kipindi cha miaka 10 kwa mfano hataruhusiwa kugombea tena .... hivyo niwatoe hofu wale wanaotaka Mbowe aendelee kuwa katiba haijamnyima labla aamue kujiuzulu jambo ambalo ni ndoto kwa Mbowe. Kwa maana hiyo jumla ya wanaoitaka nafasi hiyo kwa sasa ni watu 5 ambao tayari wanajukikana.

HISTORIA INASEMAJE?

Kwa historia ya nafasi hiyo ya uenyekiti kwa miaka ya hivi karibuni inaonyesha kuwa kila anayejaribu kusema anaitaka nafasi hiyo hukumbana na balaa la kisiasa.

Rejea Chacha wangwe, Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo, Mwigamba na wengineo. Inafahamika hili na uchaguzi wa mwisho Mbowe aligombea na kivuli baada ya kumfukuza Zitto na yeye kujidai wazee wamekuja kumshawishi agombee tena wazee toka Kigoma.

HALI IPOJE KWA SASA.

Mazingira ya uchaguzi unaokuja yapo tofauti kabisa na mazingira ya nyuma. Kwanza sura na haiba ya watu wanaotaka kumkabili Mbowe si watu wa kuwafukuza. Unapotaja mtu kama Lowassa, Sumaye na Lissu ukataka kuwafukuza itakulazimu ukae chini ufikirie zaidi ya miaka 2 athari za kuwafukuza.

Kama haya hizi habari zikithibitika ni kweli basi kwa ushauri tu ningemshauri mbowe asichukue form na astaafu kwa heshima. Nathamini na naamini na naujua mchango wa Mbowe kwa chadema. Najua kakitoa wapi chama hiki hadi kufikia mahali pa wanasiasa wakubwa kama kina Lowassa na Sumaye kuamua kuchukua kadi za chama hiki.

HATARI ILIYOPO

Kwa sasa kuna makundi yameshaanza kuundwa kila mtu niliyemtaja hapo juu anajijenga kivyake. Jambo hili litakipasua chama kabisa huko mbeleni. Na siamini kama chaedma kinaweza kuhimili mpasuko wa makindi haya ndio maana nashauri intellejensia ya chama kulichunguza hili na kulisimamia kusitishwa kwake kwa manufaa ya ustawi wa chadema. Wananchi wenye uelewa wanatambua mchango mkubwa wa vyama vya upinzani ndio maana naongea hili bila ITIKADI.

VIASHIRIA.

Kuna viashiria vingi vimeanza kujitokeza:-

1. Swala la uchaguzi wa kanda ya nyasa. Mpasuko unaojitokeza unasababishwa na team za wanaowania uenyekiti. Inasemakana Sesopi ni kipenzi cha Lowassa na angelitumiwa naye vizuri kujenga ushawishi wa mzee kukubalika kwenye kanda ya nyasa. Mbowe alishtukia dili na kumuondoa na kumuweka Msigwa kwa kuwa ni mtiifu kwake kwa maana hiyo atalinda maslahi yake.

2. Kupotea kwa Ben saanane hakumuumi sana mbowe kwa kuwa Saa nane ni mtu anayetamani mapinduzi ndani ya chama. Inasemekana Lisu ni kipenzi kikubwa cha Saanane na ndio maana alijitokeza hadharani kumtafuta na kumsemea Ben.

3.Vijana waelewa wa chadema kupata ujasiri wa kuhoji baadhi ya mambo ambayo yalizoeleka ila kwa sasa wanahoji sana swala la Demikrasia ndani ya chama. Inasemekana ni maandalizi ya kumwandaa mbowe kisaikolojia.

4. Mikutano ya ndani anayoiendesha Lowassa, kuna tetesi kuwa Lowassa anatumia fedha zake kufanya mikutano hiyo na mojawapo ya sera abagoieneza ni kukataa sera iliyomjenga mbowe ya uanaharakati badala yake chama kaiachane na harakati.

5. Sumaye aliuziwa jumba bovu kuambiwa akagombee kanda ya pwani ikiwa ni maandalizi ya kumuondoa kwenye kinyanganyiro hicho.

6. Masha na wenje kuwa ndio wagombea pekee ambao Mbowe alitaka wagombee ubunge wa Afrika mashariki ilikuwa ni mbinu ya kumtoa masha kwenye mawazo ya kugombea uenyekiti. Mbowe alijua ubunge wa Afrika mashariki ungemtuliza Masha na asingefikiria tena nafasi hiyo ya kudumu ya mheshimiwa mbowe.

7.Kuahirishwa kwa uchaguzi wa Chadema kwa sababu zisizoeleweka nayo ilikuwa ni kiashiria cha mvurugano uliokuwepo Chadema. Baada ya Lisu kupata misukosuko Mbowe ameanza kudeal na watu wengine wanaowazia nafasi hiyo. Jiulize tu nn kimemwondoa Masha katika wakati huu kukiwa na utulivu mkubwa ndani ya chama?

KUONDOKA KWA MASHA NI PIGO KWA LOWASSA.

Hakuna mwanachama yeyote zaidi ya Mbowe anayejua au aliyekuwa anawaza kama Masha anafikiria kuondoka. Lakini kwa waelewa wa mambo tulishaliona hili.

Katika mazingira ambayo wanachama wanaona kwamba chama kimetulia ndio masha anaondoka. Hili ni pigo la Lowassa aliyekuwa anatamani sana Masha kuwa mwenyekiti ajaye kama yeye angelifikiei tofauti juu ya kuongoza chama hicho.

Lowassa aliini kuwa kama.watampata mwenekiti toka Kanda ya ziwa ingekuwa rahisi sana kwake kushinda uchaguzi kwani angelifanikiwa kuivuruga CCM kanda ya ziwa ambako inakubalika sana kwa wakati huu. Masha ndiye mtu pekee aliyekuwa kichwani mwake lakini Mbowe alikuwa anawaza tofauti.

#Mbowe ni mwanasiasa ambaye ni Tallented na yupo Smart sana. Huwa nawaza huyu jamaa angelikuwa na degree moja tu ingelikiwaje? Kafanikiwa tena kumwondolea Masha dirishani kwa style ya ajabu na style isiyojulikana.

Sababu anazozitoa Masha za kujiuzulu siyo za Kweli amekutana na mkono wa kaka Mbowe kama wapiga kura wake wanavyomuita.

LEO 2018 MAMBO YANAENDELEA KUWA YALE YALE.

Hayo niliyoandika hapo juu niliyaandika tarehe 8/4/ 2017 hii hama hama ilikuwa haijaota mizizi. Leo Kuna kijana toka Chadema kayarudia Yale Yale kwa Style tofauti. Kijana huyu anaitwa Kibona Dickson noamba kuweka aliyoyaandika hapa. #NANUKUU...

MAGENGE YA FITINA NDANI YA CHADEMA KUELEKEA 2020.

Na Kibona Dickson.
(Mchambuzi huru).

Chama kikuu cha upinzani kina matatizo makubwa ya ndani kwa ndani kuelekea 2020.Ndani ya chama kumejaa chuki na fitina.

Niliwahi andika kuhusu hili,nikajenga hoja kwamba kuna mnara wa chuki na fitina ndani ya chadema.Niliandika kuwa mazingira ya chuki na fitina yanachochea madiwani na wabunge kuondoka.

Aidha,mazingira haya yanawasaidia ccm kuwapata wahanga wa fitina.Washindi katika mchezo wa kufitiniana ndio wanajifanya watabiri au wanakimbilia mitandaoni na kudai "waliohama wamenunuliwa."

kuna watu bila kufanya utafiti walinijibu "hakuna taasisi isiyo na migogoro." Wakadai migogoro ipo kila mahali,hata kwenye madhehebu ya dini kuna migogoro

Ni kweli.Lakini kuna tofauti kati ya migogoro(misunderstanding/conflicts/disputes) na Fitina.

Fitina ni zaidi ya migogoro. Ndio maana watu husema "ufalme uliofitinika,lazima utaanguka".Yanayoendelea Chadema yanaonesha chama hicho kimeshavuka kutoka kwenye stage ya migogoro na sasa kipo Kwenye stage ya kufanyiana fitina( kusambaratishana).

Chama kimegeuzwa kuwa magenge ya fitina na chuki;Magenge kuharibiana;magenge ya kumalizana kisiasa.

Hali hii isipokomeshwa,itasambaratisha chama kuelekea 2020 na ccm wataendelea kupata mavuna.

Huko nyuma upinzani ulizoea kuvuna wanachama wa ccm waliowahanga wa fitina,lakini sasa kibao kimegeuka,ccm ndio wanaovuna wahanga fitina kutoka upinzani.Ccm wanaijua fitina iliyoko...Wanajua nguvu ya Makundi yanayofitiana chamani.

Wahanga wakubwa wa fitina ni 1.watu wasiomuunga mkono Mbowe katika mipango yake ya kurejea kwenye uenyekiti.2.Kuna watu wanamtaka Tundu lissu.3.Kuna watu wanaotaka majimbo ambayo yako chini ya chadema,wanajianda kuwa eliminate wenzao; na 4 Kuna watu wanaohoji ruzuku.Watu hawa hawana amani Kwenye chama

Makundi haya ndani ya chama yanafanya kazi ya kujenga mnara wa chuki na fitina ili kuharibiana.Wanaofaidika na fitina za ndani ya chadema ni CCM.Wamevuna madiwani na wabunge na wataendelea kuvuna....

Tatizo la wanachama na viongozi wa chama kikuu cha upinzani ni kutokuwa na uwezo wa kuona udhaifu wao.Hawawezi kutafakari kitu kipya nje ya kilichoongelewa na kiongozi wao-mawazo mgando.

Nimefuatilia Kwa umakini clips za maneno ya Sauti yanayoendelea kusambaa mitandaoni;kundi moja ni mazungumzo kati ya wabunge wawili wa chadema;Kubenea na Komu.Kundi la pili ni Kati ya Meya Bony na mwanachama mmoja wa chadema.

Japo,ninaendelea kuthibitisha ukweli Sauti hizo,maudhui ya pande zote mbili ni 1.kuharibiana na 2.Mbowe na ruzuku.

Mazungumzo katika Sauti hizo yanadhihirisha fitina zilizovuka mipaka ya kuharibiana.Makundi yanafitiana;Yanazushiana na kutaka kutumia kila aina mbinu kuharibiana.

Kundi la Mbowe lina Nguvu ya kusambaratisha wengine.Kundi hili limefanikisha kuwaaminisha wanachama wengi kwamba kila anayehoji uenyekiti mbowe ametumwa na ccm.

Wanaotajwa kuwa vinara kwenye kundi hili ni wajumbe wawili kamati kuu;Bony,Meya wa ubungo na Lema,mbunge arusha mjini,aliyejizolea umaarufu wa kuandika fitina mtandaoni kutabiria wabunge wenzake kuhamia ccm.

Bony anaelezwa kumtumikia Mbowe kwa nguvu zake zote.Inaelezwa,anatumika kusambaratisha wengine wasiotaka Mbowe kuendelea kuongoza chama na pengine kugombea urais 2020.

Katika Maelezo ya sauti yanayosambazwa mtandaoni Komu anasikika akimweleza Saed Kubenea kuwa "Bony ndiye aliyemsambaratisha Mwita Waitara."

Saed na Komu wanaonekana kuzungumza kama wahanga wakuu wa kundi la Mbowe.

Chama ambacho wanachama wake wapambana kusambaratishana kinaelekea kudhoofika.Mwita Waitara alihamia ccm miezi miwili iliyopita akilalamikia "fitina ndani ya chama hicho"..

Inadaiwa,zawadi pekee anayoitarajia Bony kwa kutekeleza mapenzi ya Mbowe ni kupewa nafasi ya kugombea ubunge jimbo la ubungo 2020.

Mbowe anatajwa kuhusika kwenye ruzuku na aliyewahi kuwa mkurugenzi wa fedha pale makao makuu(Komu).Komu anatamani sana Takukuru waingilie kati ili kumshughulikia Mbowe.Takukuru ni taasisi ya kupambana na na kuzuia Rushwa Tanzania.Ni taasisi ya umma.
Ruzuku inayotajwa kutumiwa vibaya na Genge la Mbowe ni fedha za umma zinazotolewa kwenye chama cha siasa chenye wabunge.

Fitina na chuki ni mbaya.

Mwaka 2014 kabla ya uchaguzi mkuu ndani ya chama Zitto kabwe alionekana ni tishio kwa nafasi ya Mbowe.Fitina zilipikwa ili aondolewe kwenye chama.

Zitto na kundi lake walitengenezewa mashitaka ya uhaini ndani ya chama.Mwanasheria mkuu wa chama,Lissu alitumika sana kufafanua na kueleza kwamba Zitto na wenzake walitaka kufanya uhaini Kwenye chama.Lissu alisema hayo huku akijua kuwa hakuna uhaini Kwenye ngazi ya chama.

Fitina hizi,zilisababisha zitto kukimbilia kortini na baadaye kupoteza uanachama.Ofisi ya katibu mkuu wakati chini ya Dkt Slaa ilipiga kambi Kigoma ili kummaliza mhaini Zzk.

Aliporudi bungeni kupitia ACT,walewale waliodai ni msaliti na mhaini wakahitaji ushirika naye kupambana na ccm.

Yaleyale yanajirudia kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi.Kufitiana.

Niseme tu "Fitina ni mwiko"

Hiki chama bado ni tumaini la watanzania.Inahitajika,Busara ile ya wazee waliomshawishi zzk aondoe jina lake kugombea uenyekiti 2009 ili Mbowe apite bila kupingwa.Wazee ndani ya chadema wakae watoe ushauri ili chama kiondokane na fitina na kusambaratishana.

Hali kadharika nilisema "chama kufanye uchunguzi" Iundwe kamati huru ya kuchunguza yanayoendelea sasa kwenye chama.
Niseme tu "Fitina ni mwiko"

N.B:Wale mabingwa wa kutukana bila kuelewa.Hilo halinitishi,wala halitanizuia kuandika ninavyoona.Mimi si kama mnyama wa kufugwa akili.

kibonadickson@gmail.com.
Mwanaharakati huru.

I Concurred with him kuna SAA huwa nawaambia kuhusu Mbowe kukaa Pemben mnakuja juu. Tafakari kwanza.

Ole Mushi.
0712702602.
 
Ukiona maneno meeengi kama haya eti ni "USHAURI" ujue ni Uzandiki mkubwa...

Uzuri decision makers wa Chadema sio wajinga unawewa-swing kwa paragraph hovyo kama hivi.....

Ndio maana nawakubali sana CDM....Kuna vichwa wenye kufanya decision making
 
bavichaa yaani hamsikii akiguswa mboe...yaani mpo tayari cdm ife ila mboe abaki salama

Such a dishonest person.....eti Mboe,ni Mbowe..

As a man kua na decency ya ku-put some respect to your fellow man's name.....

Kila mwanadamu ana mapungufu,ila I hell know Mbowe is keeping CCM awake mwaka wa 20 huu...

Na kumuondoa tupieni kura sio some stupid articles like this zilizojaa majungu ya kike kike namna hii....
 
Ningeshauri kuwa Makundi yote yaangalie Maslahi ya Wanachama na Wapenzi wa CHADEMA badala ya kuweka Maslahi Yao binafsi mbele. Ningependekeza pia, Halima Mdee, Lema, Jackobs, wakae pembeni kidogo na waruhusu majadiliano ya pande hizi zinazokinzana yafanyike. Wazee wa CHAMA hebu watumie Busara zao kuwaondoa katika mtanziko hawa jamaa. Jumuiya zote ndani ya Chama zitafakari namna ya kukiweka Chama salama badala ya kujifanya vipofu na kushabikia Chama kumomonyoka kwa kauli za usaliti! Tusipokubali kukosolewa na kukosoana sisi kwa sisi, na kuyajenga sisi kwa sisi, hatutakuwa na legitimacy ya kukosoa wengine. Katika kipindi hiki ambacho CCM na Serikali Yake wameamua kutushughulikia kwa kila mbinu, Umoja na Ushirikiano ndio silaha yetu Namba Moja, na zipo startegies nyingi tu za kuwashughulikia wakaidi bila kuleta mizozo Wala mtafaruku! Pia wanaoanzisha mizozo hebu wakae chini watafakari the aftermath ya wanachokifanya, lengo Ni Nini?
 
Tatizo la CDM ni ujuaji wa kitoto. Utamshauri vipi akuelewe mtu ambaye tayari anaamini kuwa anachokijua ndio asilimia mia moja ya ukweli wa mambo.

Ni mwendo wa kumpigia mbuzi gitaa.
 
Uchambuzi mreeeeefu kwl ila ungeufupisha ukasema kua chadema wamteme mbowe tu na ww huwezi kua mshauri wa chadema ebu jaribu kushauri uko mlipo maana chadema sidhani kama inaweza kua inahitaji ushauri wa kiuongozi toka kwako au kwenu
 
Back
Top Bottom