yakhe maalim yupo katika kazi kwani kazi tuliyomtuma hajaimaliza na wewe kama shahidi ,angalia tu na utakuja kuona kuwa jamaa ni MasterMind wa kuiondoa CCM kwenye madaraka ,haya ya huku yawache kama yalivyo ,CUF inasema wameshaingiza mguu mmoja ndani ya Ikulu sasa wanapigania kuingiza wa pili.Kazi huko mnakogombea umeya !Naama Mwiba, Maalim Seif anaendeleaje na mnofu wa ngurue alioamua kuisaidia CCM kutafuna huko yakhe?
Corrupted brain, corrupted mind, corrupted thinking
Conclusion: CRAP
Wekeni pembeni matusi,hapa nilipo nipo na mkuu tena wa ngazi za juu kabisa,amesema kipo kitu ilikuwa kitokee na kama sio polisi kuingilia kati basi ana uhakika Chadema wangetwishwa mzigo wa lawama.
Nyie wengine mpo kusubiri habari tu,hebu ingieni deep kwenye hili jambo ili mjue ni kipi hicho walichokuwa nacho polisi ???
Yakhe mimi ni mtu wa kwanza kulaani mambo haya ,tena ni nambari one,tokea 2001 ......sasa hii ya Arusha kwangu mimi ni muendelezo tu wa yale ambayo nikiyapinga kwa marefu na mapana ,siejui wakati huo mlikuwa wapi ,maana kama tungelikuwa pamoja wakati huo ,haya ya leo yasingetendeka,lakini mlitutenga na kutona wapemba si watu.
Now police forces kill your brothers and sisters ,poleni sana ,leo hii ndio mnatambua kuwa Serikali ya CCM ni mbaya,leo hii ndio mnatambua kuwa jeshi la polisi halitendi haki ,leo hii ndio mnatambua kuwa jeshi la polisi linauwa raia wasiokuwa na hatia.
Basi wandugu bado huo au hio ni dibaji tu,polisi hao watauwa,watatesa watanajisi na watafanya kila ovu mnalolijua na msilo lijua,kama nasema kama hamkuamua kupambana nao roho kwa roho basi hayo makelele yenu hayatakuwa dawa wala hawatayasikia,endeleeni kuleta matusi hapa labda mnaona hiyo ndio dawa.
Unafahamu jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza,mambo ambayo yangetokea kama maandamano yangefanyika yangelipelekea Chadema kufutwa na pia wengi wa viongozi kuishia gerezani.
Majanga ambayo yangetokea kusingelikuwa na wa kumshika isipokuwa wahusika wangelikuwa ni Chama cha Chadema.Ni vizuri Chadema kutafuta ni habari gani polisi walikuwa nazo na ni akina nani walitayarisha mipango hiyo ya hatari,Je ni UVCCM au Ni WaChadema.
Habari za kiintelijensia ambazo polisi wamesema wanazo au walizipata bila ya wasiwasi wowote ule zingehatarisha usalama wa raia wengi kuliko inavyofikiriwa ,nionavyo ndio maana polisi wakalazimika kuzima maandamano kwa njia yeyote ile alimuradi nia ya waliokusudia uovu kutumia maandamano hayo zisifanikiwe.
Inawezekana kabisa habari hizo zikawa na ukweli au zikawa ni rummors zisizo na uthibitisho wowote ule, sasa inakuja kuja hali ya kudhibiti ni pale tunaposema ni bora kukinga kuliko kutibu,polisi wamekinga.
Ingawa kuna watu humu watakuja na ujuwaji kulivyo wanavyojua,hao huwa nawaweka mkono wa kushoto na ni watu wa kupuuzwa,changamoto iliyopo ni uongozi wa juu kutafuta hizo habari za kiupelelezi kutoka kwa jeshi la polisi na kuwajua wabaya wao waliotaka kujichomeka ndani ya maandamano ili kujua ukweli wa mambo.Tugange yajayo yaliopita si ndwele ndivyo waswahili tusemavyo.
Wacheni Jazba ,muhimu ni kutafutwa walichokuwa nacho polisi ,jamani hasira hazijengi ,JF ni moja ya kiini zipatikanapo habari za kiintelejinsia ,sasa kale kaizi chetu ni lazima kapite huko kwenye vitalu vya habari za upelelezi ziwekwe hapa ,ikiwa Chadema na uongozi wao watashindwa kuzipata ,kama mnafahamu hili sio jambo jepesi ni lazima ukweli wa kilichokuwa kitendeke ambacho polisi walikihofia kielezwe ,nani atakieleza ,je Chadema wanazijua au wameshazijua ,au walipokamatwa walimegewa na sasa wamekaa kimya ,wengine wacheni kumwaga mavumba maana mna harufu mbaya ya midomo.
Mwiba umepoteza mwelekeo na credibility!
Habari za kiintelijensia zinaniambia kwamba unaishi kwa kutunga kubuni na kuzusha mambo na kuhisihisi bila kuwa objective!
Tungekuwa na watu kumi tu wenye uelewa kama wako hapa JF tungelikuwa tumefika mbali ,ila kama uonavyo tuna mambutwai wababe na wajuaji na wenye urithi wa matusi kutoka wanakokujua,ahsante kwa kunifahamu kwa kina.WanaJF,
Post ya mwiba inatafsiriwa kama "Crap" na wengi wa wachangiaji, mimi naoana ametumia kejeli kidogo kuwasilisha ujumbe mzito.
Amesema analaani mauaji ya raia wasio na hatia. Hili halina shaka limo kwenye post yake...pia amekwenda mbali kusema wakati 2001 wapemba waliuwawa na hawa hawa Polisi wa serikali inayoilinda CCM na si wananchi. walipofanya mauaji wengi wa watu walifurahia waliona ni sawa tu waliyofanya Polisi wakati huo.
Vyama vyengine vinapoandamana, maoni yanayotolewa humu Jf yanaweza kukufanya ujiulize masuali mengi na usipate jawabu..wengine husema "vunja miguu", "vunja mikono hao", washikishe adabu hao nk.
Waswahili husema "ukimuona mwenzako ananyolewa, wewe tia maji!"
Kwa hiyo, wakati tunauchungu, tunaomboleza vifo vya Watznia wenzetu, pia tutafakari zaidi kuwa ushabiki wa kichama pekee, unatupeleka pabaya, kuna mambo ambayo yanamgusa kila raia, aliye Arusha, aliye Lindi, aliye Tanga, aliye Mbeya, aliye Pemba na kwa hivyo, linapotokea kama hili la Arusha inapasa tushikamane na kudai haki zetu.
kama nimemfahamu vyema Mwiba ni kuwa kama jamii ya Tz ingesimama kidete kutetea, kuunga mkono na kutetea haki za Raia waliouwawa Pemba 2001 leo Polisi na serikali ya CCM isingekuwa na jeuri hii waliyoifanya Arusha.
Badala ya kutupiana matusi, tuutafakari ujumbe wa Mwiba na tuufanyie kazi.
Tushikamane! na Haki ya Raia inapokanyangwa sote, tuhisi kuwa tumeonewa na tudai haki hiyo.
Na CCM na serikali yake haitaishia hapo,itaendeleza kumpiga nyundo kila ambaye anatishia maslahi yao.
kauli za NCCR, CUF nk ni mwanzo mzuri, vyama vinaanza kuona ukweli na taasisi nyengine za kiraia pia. sasa isiwe kwa hili tu.