Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,760
Unafahamu jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza,mambo ambayo yangetokea kama maandamano yangefanyika yangelipelekea Chadema kufutwa na pia wengi wa viongozi kuishia gerezani.
Majanga ambayo yangetokea kusingelikuwa na wa kumshika isipokuwa wahusika wangelikuwa ni Chama cha Chadema.Ni vizuri Chadema kutafuta ni habari gani polisi walikuwa nazo na ni akina nani walitayarisha mipango hiyo ya hatari,Je ni UVCCM au Ni WaChadema.
Habari za kiintelijensia ambazo polisi wamesema wanazo au walizipata bila ya wasiwasi wowote ule zingehatarisha usalama wa raia wengi kuliko inavyofikiriwa ,nionavyo ndio maana polisi wakalazimika kuzima maandamano kwa njia yeyote ile alimuradi nia ya waliokusudia uovu kutumia maandamano hayo zisifanikiwe.
Inawezekana kabisa habari hizo zikawa na ukweli au zikawa ni rummors zisizo na uthibitisho wowote ule, sasa inakuja kuja hali ya kudhibiti ni pale tunaposema ni bora kukinga kuliko kutibu,polisi wamekinga.
Ingawa kuna watu humu watakuja na ujuwaji kulivyo wanavyojua,hao huwa nawaweka mkono wa kushoto na ni watu wa kupuuzwa,changamoto iliyopo ni uongozi wa juu kutafuta hizo habari za kiupelelezi kutoka kwa jeshi la polisi na kuwajua wabaya wao waliotaka kujichomeka ndani ya maandamano ili kujua ukweli wa mambo.Tugange yajayo yaliopita si ndwele ndivyo waswahili tusemavyo.