CHADEMA waifungulia CUF njia…

CHADEMA waifungulia CUF njia…

CHADEMA imeshindwa kuitumia vizuri nafasi yake kama chama kikuu cha upinzani kwa manufaa ya taifa.

Hali ilianza kuonekana tangu awali baada ya uchaguzi mkuu ambapo CHADEMA ilikataa kushikisha vyama vingine kwenye uongozi wa upinzani Bungeni. Uamuzi huu wa cHADEMA uliwasikitisha wapenda mabadiliko wengi.

Hii ni tofauti na chama cha wananchi CUF ambacho kiliishirikisha chadema kwenye uongozi wa upinzani Bungeni katika Bunge liliopita. Manufaa yake kwa taifa tumeyaona, Bunge la tisa liliweza kusimamia hoja nzito za kitaifa na kuitetemesha serikali mpaka Waziri Mkuu akajiuzuru. Bunge hili la 10 lina wabunge wengi zaidi wa upinzani lakini hakuna mafanikio yoyote katika kujenga hoja!

Zaidi ya hilo, mara kadhaa CHADEMA wamekuwa wakikimbia mijadala kwa mtindo wa kususa ambao haujawahi kuleta manufaa yoyote. Jambo kama la kususia hotuba ya Mkuu wa Nchi halikuwahi kutokea Bungeni wakati CUF ilipokuwa chama kikuu cha upinzani kwenye bunge la 9.

Kadri siku zinavyoenda wananchi wanazidi kushuhudia jinsi CHADEMA inavyoshindwa kuwakilisha maslahi ya taifa Bungeni. Jambo linalosikitisha zaidi ni kwamba siku hizi wabunge wa CHADEMA wakiongea taarifa pekee inayoweza kutolewa ni kwamba “wamemchana kiongozi fulani”.

Anayeongoza katika tabia hii ya “kuchana” ni Sugu ambaye jana ameelezewa kuwa alimchana mbunge wa Iramba Mashariki. Huo ndio ulikuwa mchango wake kwenye bajeti ya Waziri Mkuu!!!

Kwa kweli inasikitisha pale input ya speech ya mbunge katika kuchangia bajeti ya Waziri Mkuu inapokuwa ni kumchana kiongozi! Mambo haya hayakuwepo Bungeni wakati CUF ilipokuwa chama kikuu cha upinzani Bungeni. Hamad Rashid wa CUF alikuwa maridadi zaidi katika kusimamia shughuli na hoja za upinzani Bungeni kuliko anavyofanya kiongozi wa upinzani wa Bunge hili la 10.

Picha inayowekwa na CHADEMA ni kwamba upinzani ni vurugu. Wananchi wastaarabu wanaanza kuchukizwa na tabia za uvunjifu wa kanuni na kumkosea heshima Spika zinazofanywa na wabunge wa chadema. Hamad Rashid wa CUF hakuruhusu hili, lakini kiongozi wa sasa wa upinzani Bungeni anaona vurugu na kubishana na Spika kama burudani.

Nikumbushe tu kuwa taarifa zilizopo zinaonyesha hakuna mbunge hata mmoja wa CHADEMA aliyeweza kutekeleza ahadi zake alizotoa kwa wananchi jimboni. Kwahiyo wananchi wanaweza kuwa na imani na wabunge wa CHADEMA iwapo wataona angalau Bungeni wana michango yenye tija.

Kwavile jimboni wabunge wa chadema hawatekelezi ahadi na Bungeni wanaenda “kuchanana” wananchi watakuwa hawana sababu ya kuchagua CHADEMA. Hasahasa ikizingatiwa kuwa chadema kimekuwa ni chama kinachoainisha matatizo bila kutoa jinsi yoyote ya utatuzi.

Vilevile CUF watakuwa na sababu ya kuwaambia wananchi kuwa CHADEMA wameharibu image ya upinzani Bungeni - jambo ambalo ni kweli. Jambo hilo litaiwezesha CUF kuchukua kura nyingi za wapenda upinzani ambazo zingeweza kuwa za CHADEMA katika majimbo ya Tanznia Bara. Kwa vigezo hivyohivyo CHADEMA itaendelea kukosa kura za Zanzibar.

Bottomline: CHADEMA imeligeuza Bunge kuwa jukwaa la kampeni. CUF walipokuwa wanaongoza upinzani Bungeni walisimamia hoja kwa maslahi ya taifa. Tabia ya vurugu na kumkosea heshima Spika inayofanywa na CHADEMA ni mtaji wa kisiasa kwa CUF.

Ushauri: CHADEMA ijiepushe na tabia za mipasho mbele ya TBC mkiwa Bungeni. Sugu apewe mafunzo maaluma ya kuchagua maneno ya kuongea Bungeni – itafaa zaidi iwapo hotuba zake zitapitiwa na Mnyika kabla hajazisoma.

Unaongea hewa kama vile hujasoma Ilboru
 
Mbona basi CHADEMA ilipata kura nyingi kuliko CUF hukohuko visiwani Zanzibar, umeshasahau UZINI?
 
Sijawahi katika siasa za vyama vingi kuiona CCM ikiweweseka kiasi cha kufikia hatua y HERI TUKOSE WOTE. Maana hapa wameishiwa kila Propaganda.

Sasa wanaona wamechakaa hawaaminiki, hawasikilizwi, haweheshimiki (wanatupiwa virago) wameamua kuwanadi wengine.

Sasa haya maneno ndiyo mtakwenda kuwaambia wamasai wa Loliondo kuwa CUF ni bora kuliko CDM, mkienda na Mtwara hivyo hivyo, Nyamongo hivyohivyo na kwingineko.

Sasa sijui ndiyo masharti ya ndoa yenu ya Zenji au mmeanza kuwachumbia na huku Bara?.

Sijawahi kuona mkiwapigia wengine DEBE!.
 
CHADEMA imechoka kiasi kwamba Mh. Sugu anachangia pumba bungeni na Mh. Nassari yeye hajui umuhimu wa Nyuki, kwa kweli 2015 CUF njia nyeupe kwao ya kuwa chama kikuu cha upinzani.
Huu ni uthibitsho kuwa wewe ni sumu. Is this the end of your thinking capacity?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Hakuna la maana ktk mada hii..KILA KUKICHA CHADEMA,vp hamuwataji NCCR.yaonekana chadema imewakalia vibaya
 
hivi mnataka nimtaje huyu mleta maada kwa jina lake na anapofanya kazi ili msiwe mbaangaika naye?
 
Me haijanitia moyo wa kuisoma yaani imenichosha.siwezi soma upumbavu
 
Tatizo hili lilisababishwa na ubinafsi wa kiongozi aliyeng´ang´ania kuhodhi nafasi ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni bila kuheshimu matakwa ya wabunge. Wabunge wengi walipendelea Kiongozi wa Upinzani Bungeni awe kijana aliyeonyesha uwezo wa juu katika Bunge la 9.

Madhara ya nafasi ya uongozi Bungeni kuchuliwa na mtu aliyetoka bench ndio haya.

Bunge letu lingekuwa na manufaa na upinzani ungeonekana kuwa na maana iwapo Kiongozi wa upinzania angekuwa kijana mwenye uwezo mkubwa ulioonekana bayana kwenye Bunge la 9, halafu naibu wake angekuwa hamad Rashid wa CUF ambaye ana uzoefu wa kuwa Bungeni tangu enzi za chama kimoja, halafu Mbowe angekuwa Chief Whip.

Mbowe pamoja na kuwa uwezo wake wa kufikiria ni mdogo kutokana na elimu yake, lakini ana busara za kuzaliwa. nafasi ya chief Whip angeimudu vizuri kama jinsi anavyomudu Uenyekiti wa chama.

Sasa hivi ni too late kufanya marekebisho hayo, lakini ni fundisho kwa upinzani kwa siku zijazo...
 
Sawa kabisa ulichomsema ila hebu tukae chini tujiulize kweli uwezo wa Hamad Rashid na Mheshimiwa Mbowe wapi na wapi?Mbowe sio mwanasiasa, nahisi ni hekima za baba mkwe tuu zinazotusumbua pale bungeni,i kulikuwa na sababu gani ya yeye kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni wakati majembe yapo??Kilichosemwa kwenye thread kina ukweli na unatuuma ila tuu itabidi tusiuonyeshe hadharani.
Hivi kuna asilimia ngapi ya wabunge wa CUF wanaotokea bara?
 
Ni vema kusoma thread na kuelewa kabla ya kujibu.
Usiwe kama Sugu.

umeelewa. Ila pia ukumbuke si tu chadema walikataa wapinzani wengine kuunda kambi rasmi bungeni bali PIA kanuni ziliwagomea wapinzani wengne kwa kuwa chadema walitosha na hata kuzidi ili kuunda kambi iyo peke yako. Ila zote za kutengua kanuni hazikuzaa matunda tarajiwa. Sugu tumemsikia,kasema serikali pumbavu ubomoe nchi yake kwa mikono yake,akitoa mfano usalama wasivomsaidia jk ktk teuz zake mpaka anateua waua elimu...mlango uliofunguliwa kwa cuf ni upi ?mana unajichanganya.
 
Hakika hichi Chama bora kife wanatamaa kuliko hata shetani.Wao wanawaza ikulu hata kwa njia ya ugaidi hakika Mungu yupo atakiangamiza si muda mrefu
 
Hakika hichi Chama bora kife wanatamaa kuliko hata shetani.Wao wanawaza ikulu hata kwa njia ya ugaidi hakika Mungu yupo atakiangamiza si muda mrefu
Hata Nelson Mandela aliitwa gaidi lakini mwishowe akachukua nchi. Sasa nyie endeleeni kupayuka siku tukichukua nchi jiandae kwenda segerea
 
CHADEMA imeshindwa kuitumia vizuri nafasi yake kama chama kikuu cha upinzani kwa manufaa ya taifa.

Hali ilianza kuonekana tangu awali baada ya uchaguzi mkuu ambapo CHADEMA ilikataa kushikisha vyama vingine kwenye uongozi wa upinzani Bungeni. Uamuzi huu wa cHADEMA uliwasikitisha wapenda mabadiliko wengi.

Hii ni tofauti na chama cha wananchi CUF ambacho kiliishirikisha chadema kwenye uongozi wa upinzani Bungeni katika Bunge liliopita. Manufaa yake kwa taifa tumeyaona, Bunge la tisa liliweza kusimamia hoja nzito za kitaifa na kuitetemesha serikali mpaka Waziri Mkuu akajiuzuru. Bunge hili la 10 lina wabunge wengi zaidi wa upinzani lakini hakuna mafanikio yoyote katika kujenga hoja!

Zaidi ya hilo, mara kadhaa CHADEMA wamekuwa wakikimbia mijadala kwa mtindo wa kususa ambao haujawahi kuleta manufaa yoyote. Jambo kama la kususia hotuba ya Mkuu wa Nchi halikuwahi kutokea Bungeni wakati CUF ilipokuwa chama kikuu cha upinzani kwenye bunge la 9.

Kadri siku zinavyoenda wananchi wanazidi kushuhudia jinsi CHADEMA inavyoshindwa kuwakilisha maslahi ya taifa Bungeni. Jambo linalosikitisha zaidi ni kwamba siku hizi wabunge wa CHADEMA wakiongea taarifa pekee inayoweza kutolewa ni kwamba “wamemchana kiongozi fulani”.

Anayeongoza katika tabia hii ya “kuchana” ni Sugu ambaye jana ameelezewa kuwa alimchana mbunge wa Iramba Mashariki. Huo ndio ulikuwa mchango wake kwenye bajeti ya Waziri Mkuu!!!

Kwa kweli inasikitisha pale input ya speech ya mbunge katika kuchangia bajeti ya Waziri Mkuu inapokuwa ni kumchana kiongozi! Mambo haya hayakuwepo Bungeni wakati CUF ilipokuwa chama kikuu cha upinzani Bungeni. Hamad Rashid wa CUF alikuwa maridadi zaidi katika kusimamia shughuli na hoja za upinzani Bungeni kuliko anavyofanya kiongozi wa upinzani wa Bunge hili la 10.

Picha inayowekwa na CHADEMA ni kwamba upinzani ni vurugu. Wananchi wastaarabu wanaanza kuchukizwa na tabia za uvunjifu wa kanuni na kumkosea heshima Spika zinazofanywa na wabunge wa chadema. Hamad Rashid wa CUF hakuruhusu hili, lakini kiongozi wa sasa wa upinzani Bungeni anaona vurugu na kubishana na Spika kama burudani.

Nikumbushe tu kuwa taarifa zilizopo zinaonyesha hakuna mbunge hata mmoja wa CHADEMA aliyeweza kutekeleza ahadi zake alizotoa kwa wananchi jimboni. Kwahiyo wananchi wanaweza kuwa na imani na wabunge wa CHADEMA iwapo wataona angalau Bungeni wana michango yenye tija.

Kwavile jimboni wabunge wa chadema hawatekelezi ahadi na Bungeni wanaenda “kuchanana” wananchi watakuwa hawana sababu ya kuchagua CHADEMA. Hasahasa ikizingatiwa kuwa chadema kimekuwa ni chama kinachoainisha matatizo bila kutoa jinsi yoyote ya utatuzi.

Vilevile CUF watakuwa na sababu ya kuwaambia wananchi kuwa CHADEMA wameharibu image ya upinzani Bungeni - jambo ambalo ni kweli. Jambo hilo litaiwezesha CUF kuchukua kura nyingi za wapenda upinzani ambazo zingeweza kuwa za CHADEMA katika majimbo ya Tanznia Bara. Kwa vigezo hivyohivyo CHADEMA itaendelea kukosa kura za Zanzibar.

Bottomline: CHADEMA imeligeuza Bunge kuwa jukwaa la kampeni. CUF walipokuwa wanaongoza upinzani Bungeni walisimamia hoja kwa maslahi ya taifa. Tabia ya vurugu na kumkosea heshima Spika inayofanywa na CHADEMA ni mtaji wa kisiasa kwa CUF.

Ushauri: CHADEMA ijiepushe na tabia za mipasho mbele ya TBC mkiwa Bungeni. Sugu apewe mafunzo maaluma ya kuchagua maneno ya kuongea Bungeni – itafaa zaidi iwapo hotuba zake zitapitiwa na Mnyika kabla hajazisoma.
Leo ndo nimekundia kuwa wewe ze makopolo kuwa unatumiwa na mmoja wa watoto wa kigogo wa nchi hii aliopo madarakani kufanya siasa za kukisafisha ssm na kukishambulia cdm.
Mimi sio mwanachama wa chama chochote apa TZ.ila uwa nashiriki kwenye chaguzi na uwa nachagua sera na sio chama wala mtu.
Kwa mtazamo wangu na research tulioifanya mwaka jana na mwaka 2010 kabla ya uchaguz mkuu. Cdm ni chama kinachoonesha kuwa ni imara kwa sasa kuluko chama chochotr kile Tz na kwamba ndo chama ambacho kinakubalika na wananchi wa ali ya chini, vijana, Watu wa lika la kati wanaopenda mabadiliko.
Cdm ndo chama ambacho kimefanikiwa kujiposition kenye mind ya WaTz walio wengi zaidi kuwa ni chama pekee kinachoweza kumfikisha mTz anapopataka.
Ni chama ambacho kimekifanya.hata ssm sasa kuamka na kuanza angalau kuganya kazi kufanyia kamati zake mbalimbali mabadiliko ili angalau wakimbizane na moto wa cdm.
Chadema ni chama kinachopendwa mpaka ndani ya ssm na baadhi ya watu wa taasisi nyeti za serikali hasa wanaopenda mavadiliko.Cdm ndo chama kinachosimamia lasilimali za umma mpaka wanaweza kugundua mambo libao ya kipuuzi yanayofanywa na serikali ya ssm kama kule maliasiri,Madini,EPA, wizara ya mambo ya njd na wizara ya fedha.unamkumbuko.mkulo je alikuwa nani?kwa nini aliondolewa?
Unamkumbuka dr slaa alivyobaini wizi mkubwa wa ufisadi kwenye account ya epa?trilioni zilizoko nje?
Kuusu bungune kwanza anza na uchambuzi yakinifu kuanzia bunge linavyoongozwa na kupangwa kw mijadala na utawala mzima ndani ya bunge zen ndo utagundua kuwa kwanini sugu jana alimchana mwigulu na serikali nzima.
Kwani wewe hauishi tz?kwani upo happy na mambo yanavyofanywa sasa apa TZ?Ivi wewe hii serikali ya ssm unaweza kweli ukakaa na ukajivinia nayo mbele ya watu kweli?Wewe umefungwa au wamekufanywa uwe msukule usiwez kuyambua hata nyumba yake aliyokuwa anaishi?Funguka acha kuendekeza njaa.
 
Sina shaka na upeo wa kamanda ZeMarcopolo bali najua ni uchovu na usingizi ndio uliopelekea mpaka kutema pumba hizi.
Yaani nyinyi mnapewa ushauri wa kuwasaidia mnatokwa povu.
Kwa hiyo mnaona sifa wabunge wenu kuingia bungeni na kuanza kupiga kelele kama walevi?
Sugu badala ya kuchangia hoja kwenye bajeti hata hajui bajeti ni nini yeye anaenda ku rap jina la mwigulu Nchemba.
Ni huyu Sugu ndio amechangia vijana wengi kufeli mitihani wakiamini kuwa ukiwa rapper wa bongo flava una nafasi kubwa ya kuwa kiongozi wa kisiasa.
Lakini siwashangai kwani hata yule Mchungaji wa kujiteua Msigwa naye juzi alillalamika eti kwa nini hakutajwa katika orodha ya wabunge waliopiga kelele bungeni.#
Wabunge wanatakiwa waende bungeni kutetea maslahi ya wananhi sio kupiga kelele kama walevi wa gongo.
Chadema kama wakipata wabunge kumi 2015 itakuwa ni bahati sana
BIG UP CUF na NCCR MAGEUZI
 
Back
Top Bottom