CHADEMA waifungulia CUF njia…

CHADEMA waifungulia CUF njia…

Eti gamba gumu ZeMarcopolo linaishauri Chadema! Kama maccm mngekuwa na akili nzuri za kushauri mngefanya hivyo kwa mwenyekiti wenu anayeboronga na kudanganywa kila siku.
 
Last edited by a moderator:
Unapofananisha objective A na B tena kwa awamu mbili tofauti, kutakuwa na factors ambazo zinaweza kuathiri matokeo. Factor mojawapo kwa suala hili ni uongozi wa spika, pili vugu vugu la siasa nk. Kwa mantiki hiyo bandiko lako limekuwa haliwezi kutoa majibu sahihi
 
Mnakuja kwa style nyingi sana, lakini ukweli uko palepele kwamba CDM ndio chama pekee kinachoweza kumkomboa Mtanzania.
Elewa mambo mawili;
1. CUF hawakuamua tu kushirikisha vyama vingine kuunda kambi ya upinzani bungeni, iliwalazimu kufanya hivyo kwa vile idadi ya wabunge wao haikutosha kuunda kambi rasmi bungeni. Wangetosha, thubutu!!?? kama kuna mpinzani angesogeza pua.
2. Usitegemee CDM ku copy jinsi CUF walivyokua wanaendesha kambi ya upinzani bungeni, kila chama kina mtazamo wake. CUF walikuwa wanaburuzwa na wabunge wa ccm na serikali yake, kitu ambacho CDM imekataa na haitadhubutu, na baadhi vielelezo vya hilo umeshavitaja.
 
Hamad Rashid mara nyingi tu ameshazungumzia masuala yanayohusu Tanzania Bara.

Umeshawahi kusikia Mbowe anazungumzia swala la Pemba?

Lissu mara ngapi anaizungumzia Zanzibar?
Nachokusihi usipende kusema wananchi wanachoshwa na CHADEMA...wakati hivi majuzi kimeshinda hadi nafasi za chini vijijini kwenye ngome ya CCM....wananchi wengi wengi wanajua na wanaona hawajachagua kuona...
CCM wanafanya nini bungeni chini ya Lukuvi...au kwa kuwa umeamua kuropoka....huyo Hamad unaemsema nae alitumia staili ya kutoka nje sakata la Meli kuzama zanzibar...
Mtajitahidi sana kwa propaganda hizi but mtawapata wazee wa dar tu na vijana wenye akili za kizee..otherwise you are wasting time and your calories to flogg a dead horse!
 
Mawazo yako yanavumiliwa kadri yanavyostahili.

Hata hiyo hoja ni jinsi vurugu za chadema bungeni zinavyoipa mwanya CUF kisiasa...

wenye maamuzi ya kutoa nguvu kwa cdm or cuf ni wananchi na cyo ccm wala wewe.huna mamlaka ya kuhukumu wala kuwasemea wananchi.jiulize pamoja na hizo vurugu unazozisema na propoganda mnazofanya juu ya cdm bado wananchi wanazidi kuwapa nafasi za uongozi katika chaguzi zinazoendelea.najua ungependa mawazo au ndoto zako zitimizwe lakini mwenye maamuzi ni mungu tu.
Wewe umekuja na uzi wa kuwasifia cuf na lukosi alikuja na uzi wa kuwasifia nccr mageuzi tunasubiri mwingie aje na uzi wa tlp.
 
kwa sasa Bunge zima Sugu ndio anazidi kupendwa na wananchi wa lika zote hadi vikongwe ni wanakuita Sugu nani.....Sugu sugu.........
 
wenye maamuzi ya kutoa nguvu kwa cdm or cuf ni wananchi na cyo ccm.huna mamlaka ya kuhukumu wala kuwasemea wananchi.jiulize pamoja na hizo vurugu unazozisema na propoganda mnazofanya juu ya cdm bado wananchi wanazidi kuwa nafasi za uongozi katika chaguzi zinazoendelea.najua ungependa mawazo au ndoto zako zitimizwe lakini mwenye maamuzi ni mungu tu.
Wewe umekuja na uzi wa kuwasifia cuf na lukosi alikuja na uzi wa kuwasifia nccr mageuzi tunasubiri mwingie aje na uzi wa tlp.

Ogopa sana vijana wenye akili za kizee...Mwenyekiti wa chama akitaka kuongea pumba zake anawaita wazee wa dar...huwa sio wazee pekee..huwa kuna vijana wenye akili za kizee pia among them.
Na ndio hawa wenye mawazo haya ya colonial era.
Ndio maana unaona kama hawafanani na vijana wengine kimawazo na kifikra.
 
Kwahiyo ni wajibu wa mbunge wa Pemba kuzungumzia maswala ya Tanzania bara lakini mbungewa Tanzania Bara hapaswi kuzungumzia maswala ya Pemba?
Najua hiyo ni sehemu ya sera ya chadema ya majimbo lakini haiko sahihi kwenye hilo.

Wabunge wa CHADEMA wanakuhusu nini? Waambie wabunge wa CCM wazungumzie Pemba na kokote unakotaka...CHADEMA wanazungumza yanayowahusu wananchi wao....shauri kwako,usishauri ambayo kwako hayapo na yamekushinda...huu huitwa UNAFIKI!
 
CHADEMA imeshindwa kuitumia vizuri nafasi yake kama chama kikuu cha upinzani kwa manufaa ya taifa.

Hali ilianza kuonekana tangu awali baada ya uchaguzi mkuu ambapo CHADEMA ilikataa kushikisha vyama vingine kwenye uongozi wa upinzani Bungeni. Uamuzi huu wa cHADEMA uliwasikitisha wapenda mabadiliko wengi.

Hii ni tofauti na chama cha wananchi CUF ambacho kiliishirikisha chadema kwenye uongozi wa upinzani Bungeni katika Bunge liliopita. Manufaa yake kwa taifa tumeyaona, Bunge la tisa liliweza kusimamia hoja nzito za kitaifa na kuitetemesha serikali mpaka Waziri Mkuu akajiuzuru. Bunge hili la 10 lina wabunge wengi zaidi wa upinzani lakini hakuna mafanikio yoyote katika kujenga hoja!

Zaidi ya hilo, mara kadhaa CHADEMA wamekuwa wakikimbia mijadala kwa mtindo wa kususa ambao haujawahi kuleta manufaa yoyote. Jambo kama la kususia hotuba ya Mkuu wa Nchi halikuwahi kutokea Bungeni wakati CUF ilipokuwa chama kikuu cha upinzani kwenye bunge la 9.

Kadri siku zinavyoenda wananchi wanazidi kushuhudia jinsi CHADEMA inavyoshindwa kuwakilisha maslahi ya taifa Bungeni. Jambo linalosikitisha zaidi ni kwamba siku hizi wabunge wa CHADEMA wakiongea taarifa pekee inayoweza kutolewa ni kwamba “wamemchana kiongozi fulani”.

Anayeongoza katika tabia hii ya “kuchana” ni Sugu ambaye jana ameelezewa kuwa alimchana mbunge wa Iramba Mashariki. Huo ndio ulikuwa mchango wake kwenye bajeti ya Waziri Mkuu!!!

Kwa kweli inasikitisha pale input ya speech ya mbunge katika kuchangia bajeti ya Waziri Mkuu inapokuwa ni kumchana kiongozi! Mambo haya hayakuwepo Bungeni wakati CUF ilipokuwa chama kikuu cha upinzani Bungeni. Hamad Rashid wa CUF alikuwa maridadi zaidi katika kusimamia shughuli na hoja za upinzani Bungeni kuliko anavyofanya kiongozi wa upinzani wa Bunge hili la 10.

Picha inayowekwa na CHADEMA ni kwamba upinzani ni vurugu. Wananchi wastaarabu wanaanza kuchukizwa na tabia za uvunjifu wa kanuni na kumkosea heshima Spika zinazofanywa na wabunge wa chadema. Hamad Rashid wa CUF hakuruhusu hili, lakini kiongozi wa sasa wa upinzani Bungeni anaona vurugu na kubishana na Spika kama burudani.

Nikumbushe tu kuwa taarifa zilizopo zinaonyesha hakuna mbunge hata mmoja wa CHADEMA aliyeweza kutekeleza ahadi zake alizotoa kwa wananchi jimboni. Kwahiyo wananchi wanaweza kuwa na imani na wabunge wa CHADEMA iwapo wataona angalau Bungeni wana michango yenye tija.

Kwavile jimboni wabunge wa chadema hawatekelezi ahadi na Bungeni wanaenda “kuchanana” wananchi watakuwa hawana sababu ya kuchagua CHADEMA. Hasahasa ikizingatiwa kuwa chadema kimekuwa ni chama kinachoainisha matatizo bila kutoa jinsi yoyote ya utatuzi.

Vilevile CUF watakuwa na sababu ya kuwaambia wananchi kuwa CHADEMA wameharibu image ya upinzani Bungeni - jambo ambalo ni kweli. Jambo hilo litaiwezesha CUF kuchukua kura nyingi za wapenda upinzani ambazo zingeweza kuwa za CHADEMA katika majimbo ya Tanznia Bara. Kwa vigezo hivyohivyo CHADEMA itaendelea kukosa kura za Zanzibar.

Bottomline: CHADEMA imeligeuza Bunge kuwa jukwaa la kampeni. CUF walipokuwa wanaongoza upinzani Bungeni walisimamia hoja kwa maslahi ya taifa. Tabia ya vurugu na kumkosea heshima Spika inayofanywa na CHADEMA ni mtaji wa kisiasa kwa CUF.

Ushauri: CHADEMA ijiepushe na tabia za mipasho mbele ya TBC mkiwa Bungeni. Sugu apewe mafunzo maaluma ya kuchagua maneno ya kuongea Bungeni – itafaa zaidi iwapo hotuba zake zitapitiwa na Mnyika kabla hajazisoma.
Matapishi yako ayazoe mkeo, cuf ndio ilifanya waziri mkuu ajiuzulu?
 
Hili suala la UGAIDI limekichafua sana chama cha Chadema.

Teh teh teh!kwa mtazamo wako!

Kawaambie wenzio huko Lumumba,huku mtaani hatuitaki CCM!

Endeleeni kufanya maigizo,lakini mfahamu kwamba siku zenu zinahesabika!
 
unabweka kama jibwa lilopewa bangi mbona umeshindwa mkanda uliouandaa na akina mwigulu umebuma huna msaada kwa nchi hii wengi tunakuombea usiku na mchana ufe tujue tumedondosha msaliti mmoja njia lete mada za maana sio chadema kila siku ukingojea mkono undondoke kama fisi Kikwete alihongwa suti pair sita amemega pande la nchi amempatia Brigedia Ali akiua wanayama wa kila aina akitumbua hata mimba za wanyama kupelekea watoto wa mfalme dubai wakati watoto wakimasai wakitanga tanga hujadili hayo wewe na chadema kwa sababu ikiwepo mwaka 2015 usalama wa taifa watakupoteza kuondoa ushaidi NNyamongo wananchi wanababuka midomo mifugo inakufamimea haioti kwa ajili ya sumu barrick wanamimina kwenye mito hata mirahaba na kodi haijakusantwa wewe husemi uko na chadema ambayo imekuinua wewe na familia yako mukahamia mjini na kuacha kupaa dagaa Bagamoyo imeuzwa kwa wachina kwa sababu ya kuwahonga kama jason alivyosema kwa kumuokoa mtto wa kikwete Ridhiwani mfanya biashara ya madawa ya kulevya hayo huyaleti tujadili kujua mkataba ukoje ili tuokoe kizazi hiki na kijacho wewe na chadema iliyokutoa mpaka usalama wa taifa wakakuona mtu wakutumika Tangu Kinana awe katibu mkuu tembe asilimia 42 amekuwa wakiuliwa kwa kasi hutaki achunguzwe ili kulinda wanyama wetu kwa kizazi hiki na kijacho wewe na chadema ili uimalize kwa sababu unajua safari yako ya kisiasa imeisha kutokana na kujikoroga Asilimia 62 ya watoto wamefeli na hii ni mlolong wa miaka mitano mfululizo huongei kitu uko na chadema inayokupa tija kwenye jamii kuonekana n muana siasa Wananchi wanakula mlo mmoja,mitaani watoto wamejaa wakati wakikwete wakivimbiwa ikulu kwa fedha za wala jasho hayo husemi huna hoja wewe , na nina imani wana JF wanajua mission yako ambayo imeabort umejifix mwenyewe na huta inuka
huyu KUPE hata ufanyeje hatakuelewa kabisa! Ni kumwacha tu maana ng'ombe anayemtegemea yupo mahututi! Matokeo yake sisi tunayajua! Mambo ya Kupe hayo!!??
 
Hili suala la UGAIDI limekichafua sana chama cha Chadema.

wakati mwingine masikio yanaweza kuchagua vya kusikiliza propaganda za ccm zimekosa nafasi kwa wapiga kura na mkitaka kujua hilo acheni sanduku la kura liamuwe pasipo ccm kuchakachua.
 
Hili suala la UGAIDI limekichafua sana chama cha Chadema.
CUF walisafishwa na nani kuhusu Tuhuma zao za Ugaidi, Udini na Vurugu (Ngangari).

Hivi hamuoni aibu kujitoa akili mchana kweupe?.
 
Back
Top Bottom