Naipongeza serikali na hususani jitihada kubwa zilizofanywa na waziri mkuu Mhe. Pinda kuzima uasi mkoani Mtwara. Kilichotokea Mtwara ni matokeo ya kampeni kubwa ya uchochezi inayoendeshwa nchi nzima na CHADEMA kwa jina la M4C. CHADEMA kama walivyo wataalamu wa hali ya juu katika masuala ya uzushi, kwa makusudi kabisa waliamua kumgombanisha mheshimiwa Rais na wanamtwara.
Walichofanya CHADEMA ni kuamsha hasira za wanamtwara kwa kuwajaza porojo kuwa mhe. Rais kaamua kuihamisha gesi kutoka Mtwara na kuipeleka kwa bomba kwao Bagamoyo ambako pia kunajengwa bandari mpya kwa kutumia pesa ambayo awali "ilitengwa" kwaajili ya ukarabati na upanuzi wa bandari ya Mtwara. Hali ni maneno ambayo yalichochea hasira za wanamtwara na kuamua kufanya fujo hadi kusababisha maafa na uharibifu mkubwa wa mali.
Baada ya waziri mkuu kufanikiwa kuzima uasi huo ulioandaliwa kiufundi, CHADEMA wameazimia kuhakikisha hali ya usalama hairejei Mtwara kwa kuhamasisha tena vurugu kupitia kampeni yao ya M4C na safari hii itaongozwa mkoani humo na Mhe Godbless Lema. CHADEMA wahurumieni watanzania ambao siku zote mmekuwa mkijipambanua kuwa mnawapenda sana iweje mnawaingiza kwenye chokochoko ambazo zinasababisha maafa yao?