CHADEMA wafikiria kuingia Msituni endapo Msajili wa vyama atakifuta

CHADEMA wafikiria kuingia Msituni endapo Msajili wa vyama atakifuta

Siasa za misituni zishapitwa na wakati.
Mara ya mwisho Rais wa nchi kutokea msituni ni lini? Wapi?
Ila siasa za kuteka kulawiti kuua ndizo zinazoenda na wakati?
 
Sasa hivi kila neno la CHADEMA ni Sheria kwa Wananchi.

Na huu ujumbe umfikie msajili wa Vyama vya siasa Nchi, Nyahoza na Mtungi.

Maamuzi ya Msajili wa vyama ni kumfurahisha Samia na Genge lake.

Kutokana na kilichotokea 29.10.2025, nipo tayari kulipiza kisasi..

Nasubiri Mtungi ajichanganye ndo atajua maharage sio mboga.

Naunga mkono hoja.
View attachment 3594950
CHADEMA WAFIKIRIA KWENDA PORINI KUPIGANIA MADARAKA, YATOLEA MFANO ANC

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Sumbawanga Mjini, Adolph Mkono, amesema mazingira ya kisiasa yanayoikabili CHADEMA yanaweza kuwasukuma kufikiria njia mbadala za mapambano ya kisiasa endapo chama hicho kitaendelea kubanwa.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kabwe wilayani Nkasi, Mkono alisema historia inaonyesha kuwa vyama vinapobanwa vinaweza kubadili mbinu za kupigania haki zao.

“Ni kama wanataka kutushawishi sisi badala ya kufanya mikutano ya hadhara kama hii tuanze kufikiria pori lipo wapi tuanze mapambano ya kuiondoa serikali madarakani,” alisema Mkono.

Alieleza kuwa ANC, chama kilichoanzishwa mwaka 1912 nchini Afrika Kusini, kilifutwa mwaka 1960 na serikali ya kibaguzi ya makaburu, hali iliyowalazimu viongozi na wanachama wake kwenda porini kuendesha harakati za ukombozi dhidi ya utawala huo.

Mkono alisema baada ya miaka ya mapambano, serikali ya Afrika Kusini iliruhusu kurejea kwa ANC mwaka 1990, kabla ya chama hicho kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 1994 na kuingia madarakani.
nchi hii hakuna wapinzani kuna waganga njaa tu. Ni mpumbavu pekee anaweza kuifananisha ANC na CDM. WaTZ wana akili, siyo malofa ambao wanaweza kununuliwa kwa pesa. vijana wa TZ ni werevu, siyo malofa wa kutumika kwa maslahi ya wachache. Unataka uingie porini? 29th oct uliingia road???

CDM mkiingia msituni jueni wazi tutakaowashughulikia ni sisi raia wa kawaida hata siyo serikali. CCM ni busara ikabidhi madaraka mpaka hapo utakapoundwa upinzani mwingine ambao una watu serious na wanaojielewa,siyo "njaa-dema'. yaani anc ulinganishe na cdm??? anc unaweza kulinganisha na tanu siyo cdm. cdm unaweza kulinganisha na kile chama cha malema ambaye kafungwa.
 
Kashoga kama hako kanaweza hata kushika manati ya kuwindia ndege kweli?!!!! Tusitafutiane dhambi jamani. Wanakariboshwa huko maporini.
 
Ila siasa za kuteka kulawiti kuua ndizo zinazoenda na wakati?
Ndiyo,dunia nzima kwa sasa iko huku Maduro,Kashoggi,Besidye etc ni mfano tu.

Nitajie Rais wa nchi aliyetokea msituni hivi karibuni.
 
msijaribu kuichezea amani
Amani ipi hiyo watu 700 +wanapotea mnasema wamejiteka?

Amani ya kumvamia mtu na kumfunga pingu halafu baadae mnasema alikua anaigiza ?

Nenda kwenye familia za akina Mdude , Ali Kibao, Soka, Chaula, Kaswahili , Dioniz Kipanya , Ben Saanane, Azori Gwanda, Polepole kawaambie masuala ya amani utapata majibu yako.
20260521_045828.jpg
20260521_045748.jpg
 
Back
Top Bottom