Hassan J. Mosoka
JF-Expert Member
- Oct 26, 2010
- 682
- 323
Mabango haya ndo hasa maneno ya wananchi! CDM mwendo mdundo!! Kawashauri ccm wachonge mabango kisha wagawiwe watu! Let people's heart speaks
Ni vigumu kuangalia picha na kujua nini mkakati wa maandamano ya Chadema. Wanaoandama hawajui lengo kuu la kuandamana kwao, kwa sababu hakuna kauli mbiu. Wakifika uwanjani kuna msururu wa hotuba ambazo hazikuratibiwa.
Kwenye maandamano yao yote, kila raia anaandika chochote popote. Ni haki ya kujieleza kwa kila raia, lakini wanakosa strategic communication. Kuna wakati ujumbe kwenye mabango unakinzana na baadhi ya hotuba.
Sayansi ya public rallies inahitaji ujumbe uratibiwe na waandaaji. Wengine huchapa kabisa mabango na kugawia wananchi. Wananchi wanabakia nayo hata baada ya maandamano.
Mara kadhaa Chadema wameshashauriwa hapa kuboresha kitengo chake cha mawasiliano. Hadi maandamano ya leo inaonekana mbado. Sitaki kuamini kwamba eti Chadema nao hawashauriki kama ccm!
Ubora wa mabango nadhani ni wito wa kila mwenye mapenzi mema na CDM achangie. CDM bado ni chama kidogo kinachokuwa kila siku, usibaki kulalamika bila kuwawezesha.
Ujumbe wa mabango ni uwarisia wa maisha ya watu unaowatawala.Kama mtu una shida ukumbuki kama ujavaa vema.kama mtu umelala na njaa mswaki wapiga wanini asubuhi,Bongo ni nini waguswa.Hata kwa kutumia Tashishi,au Tasibia,LENGO UJUMBE UMEFIKA.
Nakubaliana na mtoa mada na pia wapinga mada hii. Public rally kama hizi za chadema siyo spontenous kama zile za Tunisia na Egypt, hivyo zinatakiwa zionekane kwamba ziko well and professionally communicated and coordinated. Hili halionekani, kinachoonekana ni Chadema kuambua tu tutaandamana halafu wanaandamana. Bihind it hakuonekani strong information communication and information management unit. Angalia walishindwa hata kulipia live coverage ili kupanua impact ya maandamano yao ya arusha na Mwanza. Wakiendelea na style hii, watakuwa wanatumia nguvu nyingi sana eneo fulani lakini impact yake haimwagiki maeneo mengine ambayo hawana ushawishi. Media is everything, ndiyo maana ccm wali invest sana kwenye media kwa gharama yoyote.
Nakubaliana na wale wanaosema kwamba wananchi wapewe nafasi ya kujieleza wanavyotaka. Lakini sikubaliani kwamba chadema wasiwe na namna wanavyowasilisha na kuhamasisha wananchi kupitia mabango katika haya maandamano. Kama chama wanatakiwa watuoneshe kwamba wanadai nini. Hizi hotuba hazipatikani full katika vyombo vya habari isipokuwa tu kwa wale waliohudhuria mikutano yao. Hivyo hatuwezi kusema eti walieleza malengo yao kwenye hotuba katika mkutano.
Kuna hotuba nzuri sana Dr. Slaa, Mbowe, na Zitto waliwahi kutoa maeneo tofauti wakati wa kampeni. Hatujaona jitihada za kuzirusha zile hotuba kwenye vyombo vya habari ili wananchi wote wapate ujumbe ni nini hasa chadema wanasimamia na waweze kufananisha na mambo yanavyokwenda.
Chadema wameambiwa mara nyingi tangu muda mrefu kwamba waanzishe tv na radio lakini bado wanacheza makida makida tu. Mimi naungana na mtoa mada kwamba in terms of accountability na kutekeleza maoni ya wananchi, Chadema hawana tofauti na CCM.
Uhalisia wa mabango (na uzuri/utamu wake) ni mabango yale yanayotoka kwa wananchi wenyewe...ni mioyo halisi inaongea..sio staili za ki-Chama 'kinachotawala' ambapo wahudhuria mikutano huandaliwa, na kufundishwa hadi kushaangilia..kushangilia wanaoneemeka kwa jasho la washangiliaji..na washangiliaji kutohisi hata matatizo waliyonayo wakati wa kushangilia (mfano mikono huchoka haraka kwa njaa)..ni fikra tu
Kumbe umelitambua hilo, na hata dola uwezo wa kushika hamna
I take it as a very minor discrepancy!
Mi napenda zaidi kama mabango yatakuwa community-baked/originated, kama ilivyo hapo, maana serikali inapata moja kwa moja kionjo cha mrejesho wa raia kuhusiana na taste ya huduma wanayoipata...hiyo ni live bila chenga!
MABANGO yanayokuwa generated na chama yawepo, well and good, lakini haya ya jamii yanaleta hisia za ukweli zaidi kwa asomaye....my take!
Km lengo kuu la maandamano limeshajulikana mabango ni mbwembwe tu....dhana kwamba nyimbo za maombolezo ni alama ya msiba/simanzi haibadilishi maana ya msiba hata km nyimbo hizo zingeacha kupigwa!
Nakuunga mkono. Kule ninakotoka kuna wenzetu wakifiwa huwa wanaweka burudani ya muziki na pombe kwa wale wanaokuja kukesha kwenye msiba kuwapa "company" wafiwa. Lakini hilo haliondoi ukweli kuwa ule unabaki kuwa msiba wenye majonzi kwa ndugu jamaa na marafiki wa marehemu.