Chadema waboreshe Mabango yao

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Ni vigumu kuangalia picha na kujua nini mkakati wa maandamano ya Chadema. Wanaoandama hawajui lengo kuu la kuandamana kwao, kwa sababu hakuna kauli mbiu. Wakifika uwanjani kuna msururu wa hotuba ambazo hazikuratibiwa.

Kwenye maandamano yao yote, kila raia anaandika chochote popote. Ni haki ya kujieleza kwa kila raia, lakini wanakosa strategic communication. Kuna wakati ujumbe kwenye mabango unakinzana na baadhi ya hotuba.

Sayansi ya public rallies inahitaji ujumbe uratibiwe na waandaaji. Wengine huchapa kabisa mabango na kugawia wananchi. Wananchi wanabakia nayo hata baada ya maandamano.

Mara kadhaa Chadema wameshashauriwa hapa kuboresha kitengo chake cha mawasiliano. Hadi maandamano ya leo inaonekana mbado. Sitaki kuamini kwamba eti Chadema nao hawashauriki kama ccm!
 
hizi?
hebu ziangalie vizuri ili uzidi kuumia kabisa kumoyo
attachment.php
attachment.php

attachment.php
attachment.php

attachment.php
attachment.php

attachment.php
attachment.php

attachment.php
attachment.php

attachment.php
attachment.php

attachment.php
attachment.php

attachment.php
attachment.php
 
Mallaba, asante kwa kunisaidia kuweka ushahidi wa picha. Halafu ulivyozikusanya zote!
 
I take it as a very minor discrepancy!

Mi napenda zaidi kama mabango yatakuwa community-baked/originated, kama ilivyo hapo, maana serikali inapata moja kwa moja kionjo cha mrejesho wa raia kuhusiana na taste ya huduma wanayoipata...hiyo ni live bila chenga!
MABANGO yanayokuwa generated na chama yawepo, well and good, lakini haya ya jamii yanaleta hisia za ukweli zaidi kwa asomaye....my take!
 
Ubora wa mabango nadhani ni wito wa kila mwenye mapenzi mema na CDM achangie. CDM bado ni chama kidogo kinachokuwa kila siku, usibaki kulalamika bila kuwawezesha.
 
Km lengo kuu la maandamano limeshajulikana mabango ni mbwembwe tu....dhana kwamba nyimbo za maombolezo ni alama ya msiba/simanzi haibadilishi maana ya msiba hata km nyimbo hizo zingeacha kupigwa!
 
Uhalisia wa mabango (na uzuri/utamu wake) ni mabango yale yanayotoka kwa wananchi wenyewe...ni mioyo halisi inaongea..sio staili za ki-Chama 'kinachotawala' ambapo wahudhuria mikutano huandaliwa, na kufundishwa hadi kushaangilia..kushangilia wanaoneemeka kwa jasho la washangiliaji..na washangiliaji kutohisi hata matatizo waliyonayo wakati wa kushangilia (mfano mikono huchoka haraka kwa njaa)..ni fikra tu
 
Ni vigumu kuangalia picha na kujua nini mkakati wa maandamano ya Chadema. Wanaoandama hawajui lengo kuu la kuandamana kwao, kwa sababu hakuna kauli mbiu. Wakifika uwanjani kuna msururu wa hotuba ambazo hazikuratibiwa.

Kwenye maandamano yao yote, kila raia anaandika chochote popote. Ni haki ya kujieleza kwa kila raia, lakini wanakosa strategic communication. Kuna wakati ujumbe kwenye mabango unakinzana na baadhi ya hotuba.

Sayansi ya public rallies inahitaji ujumbe uratibiwe na waandaaji. Wengine huchapa kabisa mabango na kugawia wananchi. Wananchi wanabakia nayo hata baada ya maandamano.

Mara kadhaa Chadema wameshashauriwa hapa kuboresha kitengo chake cha mawasiliano. Hadi maandamano ya leo inaonekana mbado. Sitaki kuamini kwamba eti Chadema nao hawashauriki kama ccm!

Unachoongea wewe ni mawazo ya kupikwa na mabango ya kuandaliwa ndiyo wagawiwe wananchi, huo ni utumwa ambao si wa kizazi cha leo. Mabango hayo yameandaliwa na watu binafsi kutokana na hisia zao wanazopata kutokana na sera za Chadema. Kila mtu yuko huru kuonyesha hisia zake na kufikisha ujumbe wake kwa bango na staili anayoona yeye inafaa. Hivyo tofautisha na sera za CCM kutumia pesa za wananchi kutengeneza mabango na kuwagawia watu, na pia kuwasomba toka sehemu mbalimbali kwa malori kwenda kuhudhuria mikutano, huo ni utumwa wa kifikra.
Nguvu ya umma ina mvuto zaidi na hisia zaidi.
 
Ujumbe wa mabango ni uwarisia wa maisha ya watu unaowatawala.Kama mtu una shida ukumbuki kama ujavaa vema.kama mtu umelala na njaa mswaki wapiga wanini asubuhi,Bongo ni nini waguswa.Hata kwa kutumia Tashishi,au Tasibia,LENGO UJUMBE UMEFIKA.
 
Mr Mallaba jamaa umemuweza,ujumbe hautakiwi kufanana,utaonekana kama mwandishi nimoja ,la msingi kila mwenye kuweza aandike bango lake.ASANTE MALLABA.MWANZA WAMEONYESHA NJIA
 
Hayo ndio mabango ya uhalisia wenyewe... Hayaonyeshi tu hisia za watu na matamanio yao bali yanaeleza mengi. Kwa mfano ni watu wannamna gani ambao wanajitolea kwa hali na mali kuki-enzi chama bila ya ruzuku, kofia au fulana na posho. Maandishi yanadhihirisha elimu walioyopatiwa kwa miaka 50 ya uhuru na "chama cha mafisadi" ni ya namna gani? Yanaeleza ukereketwa na ubunifu ya waandamaji, pamoja na hayo Chadema wanaweza kuweka mabango yao ila yasiondoe uhalisia wa hali ya waandamaji
 
Ni vigumu kuangalia picha na kujua nini mkakati wa maandamano ya Chadema. Wanaoandama hawajui lengo kuu la kuandamana kwao, kwa sababu hakuna kauli mbiu. Wakifika uwanjani kuna msururu wa hotuba ambazo hazikuratibiwa.

Kwenye maandamano yao yote, kila raia anaandika chochote popote. Ni haki ya kujieleza kwa kila raia, lakini wanakosa strategic communication. Kuna wakati ujumbe kwenye mabango unakinzana na baadhi ya hotuba.

Sayansi ya public rallies inahitaji ujumbe uratibiwe na waandaaji. Wengine huchapa kabisa mabango na kugawia wananchi. Wananchi wanabakia nayo hata baada ya maandamano.

Mara kadhaa Chadema wameshashauriwa hapa kuboresha kitengo chake cha mawasiliano. Hadi maandamano ya leo inaonekana mbado. Sitaki kuamini kwamba eti Chadema nao hawashauriki kama ccm!

Unachoongea wewe ni mawazo ya kupikwa na mabango ya kuandaliwa ndiyo wagawiwe wananchi, huo ni utumwa ambao si wa kizazi cha leo. Mabango hayo yameandaliwa na watu binafsi kutokana na hisia zao wanazopata kutokana na sera za Chadema. Kila mtu yuko huru kuonyesha hisia zake na kufikisha ujumbe wake kwa bango na staili anayoona yeye inafaa. Hivyo tofautisha na sera za CCM kutumia pesa za wananchi kutengeneza mabango na kuwagawia watu, au kuwasomba kwa malori ili waje mikutanoni, huo ni utumwa wa kifikra.
Nguvu ya umma ina mvuto zaidi na hisia zaidi.
 
Pia kuna haja ya Chadema kuboresha Website yao iendane na taarifa wanazozitoa...! Website yao ipo so back dated...!

Pia nimenotice kuna kuingiliana katika kutoa taarifa ndani ya chadema, kila mtu anakua mzungumzaji na anatoa taarifa kwa jinis ya utashi wake...! Leo Myika akiamka anatatoa tamko, kesho Selasini nae anatoa tamko laek, keshokutwa Dr. Slaa nae anatoa lake, Mara nae Zitto anatoa tamko lake...!

NI vyema wakaweka njia moja na ya kueleweka ya kutoa taarifa na ya kutaarifu umma (kwa mfano msemaji wa chama) etc, na kuwe na njia muafaka na za kutegemewa kwa mafano radio, website yao, facebook etc...!

Lasivo itaishia kwamba wabunge wachache ndani ya Chadema watakua wanaonekana ndio wachapa kazi na wengine wanapoteza muda labda kwa vile wao huwa hawatoi matamko mara kwa mara...!

Chadema wajitahidi kuwa na mgawanyo na kushirikisha wabenge wengine katika Public Relations ili kuwajengea wabenge wengine nao mfahamiko na ueleweka wao kwa jamii. Wasipofanya hivo itaishia kuwa wabunge wale wale wachache ndio wataonekana kuwa na nguvu ndani ya chama.
 
Kinacho matter ni ujumbe uliopo kwenye bango. Ina maana hukuelewa ujumbe uliopo kwenye hapo mabango?
Check bango kama hili huko Libya. Simple.

tobruk.jpg

Ila inabidi waifanyie kazi website yao iwe more interactive and more connected to the people.
 
Duhh! Gurudumu naona unalamba matapishi yako mwenyewe? Alichoonesha mallaba ni tofauti na mawazo yako lakini unashabikia tena ujumbe wa Mallaba!!! Ebu ziangalie vizuri picha alizoweka Mallaba na uone kama ujumbe ulioko kwenye mabango ya wananchi yanakinzana na dhana ya maandamano yao? Tafadhali tumia akili kidogo tu kutafakari thread yako na majibu ya Mallaba. Umedanganya Umma.
Mallaba, asante kwa kunisaidia kuweka ushahidi wa picha. Halafu ulivyozikusanya zote!
 
Ni vigumu kuangalia picha na kujua nini mkakati wa maandamano ya Chadema. Wanaoandama hawajui lengo kuu la kuandamana kwao, kwa sababu hakuna kauli mbiu. Wakifika uwanjani kuna msururu wa hotuba ambazo hazikuratibiwa.

Kwenye maandamano yao yote, kila raia anaandika chochote popote. Ni haki ya kujieleza kwa kila raia, lakini wanakosa strategic communication. Kuna wakati ujumbe kwenye mabango unakinzana na baadhi ya hotuba.

Sayansi ya public rallies inahitaji ujumbe uratibiwe na waandaaji. Wengine huchapa kabisa mabango na kugawia wananchi. Wananchi wanabakia nayo hata baada ya maandamano.

Mara kadhaa Chadema wameshashauriwa hapa kuboresha kitengo chake cha mawasiliano. Hadi maandamano ya leo inaonekana mbado. Sitaki kuamini kwamba eti Chadema nao hawashauriki kama ccm!
Gurudumu

Mara nyingi ujumbe unaotoka direct kwa wananchi ndio huwa unawaingia vizuri watawala tofauti na ujumbe ulioratibiwa. Ni vigumu sana kwa serikali kujibu na kubeza ujumbe mbali mbali kutoka kwa wananchi wenyewe.

Nafikiri Mallaba amekupa jibu sahihi hatutegemei wananchi kugawiwa mabango na bendera za taifa kama tunakwenda kushangilia mpira.

'Freedom of Expression' kuandika bango lako na kuhakikisha limesomwa inakufanya ujione ni sehemu ya maandano na si msindikizaji.

Gurudumu usitake turudi tena kwenye enzi za kupangiwa nini tuchukue kwenye maandamano kama wakati wa siku ya muungano au siku ya wafanyakazi kuwa mabango na ujumbe wote lazima ukaguliwe na manager kabla ya kubeba.

Aangalia jumbe hizi ambazo ndizo zilimnyima usingizi Mubarak, it is simple and clear.

images
images
images
images
images
images
 
Gurudumu huelewi nini kwenye ujumbe huu huwezi kuandika hadi ukaandikiwe na balozi wa nyumba kumi kumi.

attachment.php
 
Back
Top Bottom