CHADEMA waamua kuchimba visima 11 Igunga na Kafumu haonekani tena Igunga!

Yaani wewe ndugu huelewi kazi ya chama cha siasa. Chama kiwe CDM, CCM Democratic (usa) au Labour (uk) HAKITOI PESA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO. Hapa CDM inapongezwa kwa kuwakumbuka wanaigunga even though hawakumchagua mgombea wake. Second CDM inapongezwa kwa kuonesha inavyoweza kutumia vema michango ya wanajamii na wapenda maendeleo. Ingekuwa Magamba kingechimbwa kisima kimoja tena msoga.

Wewe ndugu yangu unaonekana debe tupu ujui chochote.

CDM wamefanya nini? Eti wamewakumbuka watu wa Igunga.

Visima anajenga Sabodo hata uko Igunga alioamua kwenda kujenga visima ni Sabodo wala sio CDM kijana.

Kwa kukusaidia Sabodo anajenga visima 700 visima 200 atajenga kwenye majimbo ya ubunge walioshinda CDM.

Visima 500 atajenga sehemu tofauti tofauti hapa nchini.

Unaleta mifano ya UK. US. Kwenye mambo ya visima vya Sabodo
 
nampongeza "fisadi" sabodo kwa uamuzi wake huo.lakini naona pesa angewapelekea walengwa kabisa.....maaana hata ndani ya chadema hawawezi kukosa nondo wachache watakaotafuna pesa kidogo na kufanya msaada huo usiwafikie walengwa!
 
Wewe ndugu yangu unaonekana debe tupu ujui chochote.CDM wamefanya nini? Eti wamewakumbuka watu wa Igunga.Visima anajenga Sabodo hata uko Igunga alioamua kwenda kujenga visima ni Sabodo wala sio CDM kijana.Kwa kukusaidia Sabodo anajenga visima 700 visima 200 atajenga kwenye majimbo ya ubunge walioshinda CDM.Visima 500 atajenga sehemu tofauti tofauti hapa nchini.Unaleta mifano ya UK. US. Kwenye mambo ya visima vya Sabodo[WEWE KAMA BADO NI KIJANA MDOGO BASI UTAKUWA UNAENDELEA KUNUFAIKA NA MFUMO WA SIASA RAFI ZA WANAMAGAMBA]
 
Wewe unajua kama Sabodo, anauza ile kitu?

Ritz, halahala usitufanye watu wazima mazezeta.

Sabodo wala hafui dafu kwenye ligi ya 'wafadhili' wakubwa wa CCM kama akina Jeetu, Ladwa, Somaiya, Manji, Raza, Vithlani, Dewji, Abdurasil family, Mula (Mbeya), Assas (Iringa), Gulamali family, Patel mjenzi Msoga na wengineo. Na hapo haifikii hata robo ya yale majina 80 aliyopewa Mkulu na yeye kusema '....ama kweli kazi ipo...', na kuyakalia mpaka leo zaidi ya miaka 3.

Na ninakuambia, kama hao hata mmoja wao atajitokeza na kuchangia hata shilingi moja kwa CHADEMA, utasikia rungu la dola litakavyoshuka.


Tukirudi kwa Kafumu na Igunga, je kulikuwa na haja gani ya Chama kutumia takribani Shs 15 milioni (wengine wanasema zinafika hadi 30 milioni), kwa ajili ya kufanya sherehe ya 'kumpokea na kumpongeza kwa ushindi' Dar? Sherehe hizo pia zilifanyika Moshi na Arusha kabla ya kusitishwa.
 
nampongeza "fisadi" sabodo kwa uamuzi wake huo.lakini naona pesa angewapelekea walengwa kabisa.....maaana hata ndani ya chadema hawawezi kukosa nondo wachache watakaotafuna pesa kidogo na kufanya msaada huo usiwafikie walengwa!
mkuu uwe na staha na maneno yako, uyu sabodo ana huruma na watanzania wewe una muhita fisadi, kwani yawezekana unafurahia jamaa zetu vijijini wakiishi katika shida?? Maana mtu anaye toa kwa moyo den anabatizwa ufisadi, acha izo
 
Swala hapa ni CHAMA CHA SIASA KUTOA PESA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO. My point was and still is A political party no matter how strong or weak, it does not use its own financial capabilities to facilitate development programs or its own manifesto for that matter. You better THINK BIG. I doubt your being a thinker leave apart being a great thinker@ Rizt
 
Anayejenga visima ni Sabodo na sio Chadema. Tusipotoshe umma.
 
nampongeza "fisadi" sabodo kwa uamuzi wake huo.lakini naona pesa angewapelekea walengwa kabisa.....maaana hata ndani ya chadema hawawezi kukosa nondo wachache watakaotafuna pesa kidogo na kufanya msaada huo usiwafikie walengwa!

Mirija ya ufujaji cdm ni mingi sana hata helikopta wanayotumia kwenye kampeni huwa garama yake ya kukodi inakuwa inflated sasa siju hii hela ya visima kama itapona
 
Tuacha ushabiki, Kiongozi gani anaweza kuleta maendeleo ndani ya wiki mbili. Ni mapema sana kumsemea Kafumu.

Nakuhakikishia huyu jamaa Kafumu hawezi kuleta maendeleo Igunga katika kipindi chake chote cha ubunge.
Mfano mzuri kabisa wewe angalia mtangulizi wake R. Azizi. Kafanya nini cha maana zaidi tangu awe mbunge wa Igunga zaidi ya miaka 10?
Wewe mdanganyiki mkubwa sana. Haya kaa ukisubiri macho mpaka yakutoke pimaaaaa. Kalagabaho!
 
Tunamuomba NAPE ajibu hizi hoja maana naona kaona ukweli ila kaamua kukaa kimya kama haoni vile WAKATI YEYE NDIYE ALIYEKUWA KINALA WA MAANDAMANO YA KAFUMU DAR badala ya IGUNGA,,,
 
Tuacha ushabiki, Kiongozi gani anaweza kuleta maendeleo ndani ya wiki mbili. Ni mapema sana kumsemea Kafumu.

japo huwa unadai ni ww ni NEUTRAL...posts zko nyingi huwa hazidhibitishi hilo...kama uko SAU,CUF,UDP au chama kingine chochote ntakuelewa.
 
japo huwa unadai ni ww ni NEUTRAL...posts zko nyingi huwa hazidhibitishi hilo...kama uko SAU,CUF,UDP au chama kingine chochote ntakuelewa.
Huyu Mzee ni mmoja wa wale wanaoingia JF kwa gea ya neutral lakini baada ya muda hujisahau na kujikuta magamba yameota bila wao kujua.
 
Mimi binafsi huwa sina imani sana na wahindi!

Duniani kote tabia zao zinafahamika, CDM wapokee hiyo misaada lakini wajaribu kuwa makini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom