CHADEMA vs CCM - Katiba mpya

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Wana bodi,

Katika kipindi hiki ambacho wana CHADEMA wanakamatwa kwasababu ya nia yao ya kutetea katiba mpya ni vyema kuji uliza kama katiba tuliyo nayo sasa hivi ina mapungufu na kama utumiaji wa nguvu na vyombo vya usalama ni sahihi. Vile vile katika kupinga au kutaka katiba mpya ni vyema kwa washika dau wote kuwa na sababu.

Haipendezi kutaka katiba mpya na kujihusisha na harakati zote bila kuwa na sababu au mapendekezo ya unacho taka kibadilishwe. Vile vile wanao pinga katiba mpya wanatakiwa kuwa na sababu ambazo zinawafanya wakatae mabadiliko yoyote kwenye katiba.

Ili kupata suluhisho wahusika wote wangetakiwa kufanya tathmini kwa undani kuhusu katiba tuliyo nayo sasa hivi waki orodhesha vipengele ambavyo lazima vibadilishwe na vipengele ambavyo lazima vibaki kama vilivyo.

Kama kuna sababu za ukweli na zenye manufaa za kufanya mabadiliko yoyote, ni vyema kama serikali na wana CCM wange jishusha kidogo na ku kubaliana na wana CHADEMA.

Njia inayo tumiwa na wana CHADEMA kudai katiba mpya ina ashiria kwamba hawata sikilizwa waki tumia njia za kistaarabu zaidi. Kama hamna mabadiliko yenye manufaa kwa watanzania, ni muhimu pia kwa wao ku kubaliana na wana CCM.

Tafakari,
Jumatatu njema
 
Back
Top Bottom