Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 46,933
- 32,342
Mkuu, hii ni "deal" imeishapangwa na Mbowe, Lowassa ndiyo mgombea urais wa Chadema hamna watu wa kumkata hayo ni makubaliaano kinachofanyika sasa hivi ni utelekezaji tu.Wanajukwaa uchaguzi wa mwaka huu una changamoto kubwa kwa chama tawala na wapinzani.
Tumeambiwa kuwa leo lowassa anachukuwa fomu ya kugombea urais kwenye ofisi ya makao makuu ya chadema ufipa DSM, swali, je anachukua fomu kupambanishwa na nani? kama kuna kushindanishwa kwa mchujo je atakuwa tayari kukubali matokeo endapo yatakuwa tofauti na ilivyotegemewa? na kama inajulikana wazi kuwa yupo upinzani ili kupeperusha bendera ya urais kupitia ukawa kwanini achukue fomu?
CHADEMA imetumia miaka tisa ikimwandaa-Dk. Slaa na familia yake-katika maisha ya taasisi ya Rais wa Tanzania kutokana na trends za kisiasa nchini. Ametembelea nchi nyingi duniani kujifunza kazi za Rais na mahitaji ya nchi. Amehudhuria mikutano na makongamano yenye shabaha ya kupanua mitazamo na fikra za kiutendani katika ofisi ya Rais.Mpaka wiki iliyopita, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Ezekiah Wenje alinukuwa na Stav TV akisema Kamati Kuu ya CHADEMA ilimpitisha Dk. Slaa kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA.
Kama hiyo haitoshi, alikuwa mbioni kutangazwa kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA au UKAWA.Matarajio na ndoto yake imefutika ghafla-baada ya ujio wa Edward Lowassa kwenye ulingo wa siasa za upinzani na kukabidhiwa kadi ya CHADEMA, na kama hiyo haitoshi, Edward Lowassa kimantiki anamtaka apeleke vielelezo vya ufisadi wake mahakamani au akae kimya!Kwa sasa hata wale waliokuwa wanadai ni Rais wa moyoni, hawaonekani tena!This is a sad ending for Dk. Slaa and his family!Kweli siasa hazina huruma na mbaya zaidi, hazina rafiki wa kudumu na adui wa kudumu!Politics is a brutal business!Ama kweli, tenda wema uende zako, usisubiri shukrani!.
Dr.Slaa hana sauti mbele ya Chadema yeye mwenyewe alikaribishwa tu inabidi afuate maagizo ya Mbowe, zaidi ya hapo atatangazwa msaliti, kaambiwa akagombee ubunge Karatu ndiyo maana yule mbunge wa Karatu safari hii kajitoa kugombea kumpisha Dr.Slaa.