CHADEMA/UKAWA, mtawapokea Chenge na Rostam pia?

CHADEMA/UKAWA, mtawapokea Chenge na Rostam pia?

Uchafu wake ni nini kwa mfano? Naamini utakuja hapa na kutuambia uchafu wake ni Richmond, nasi tutasema uchafu wa Magufuli ni kuuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupwa huku akijua kuna upungufu mkubwa wa nyumba za watumishi. Baada ya hapo tunatafuta unafuu, kulikuwa na ulazima wowote wa kuuza nyumba? Na kwa upande mwingine wa Lowassa kulikuwa na ulazima sana wa kuingia mkataba na Richmond? Wote tutakubaliana kwamba kwa Lowassa nchi ilikuwa kwenye crisis kubwa ya umeme, lakini pia tutakubaliana kwamba Magufuli aliuza nyumba kwa interest yake tu, hakukuwa na any pressure ya kumpelekea kuuza nyumba. Kwa kuwa wote ni wachafu, basi mwenye unafuu ndiye tutakayempa kura.

daaaaah kweli..Leo Richmond imekuwa sio tatizo!! soon mtakuja badili na kusema escrow pia sio tatizo kama mama T nae atajiunga ukawa
 
Inajulikana kuwa hawa ni marafiki walioshibana ndani ya CCM na hata katika maisha ya kawaida. Ikiwa swahiba wao Lowassa atahamia CHADEMA/UKAWA, wanaweza nao kumfuata rafiki yao. Sasa ndugu zangu CHADEMA/UKAWA, mtakuwa radhi kuwapokea Andrew John Chenge na Rostam Aziz kuwa wanachama wenu?

Jibuni ili umma ufahamu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Nakushauri usipoteze muda kujaribu kuzuia mafuriko kwa mkono! Shughulikia mambo ya nyumbani kwenu! Ya kwetu tuachie sisi! Hivi unajua mteule tingotingo yuko wapi? Mbona mnamtelekeza mapema hivi?
 
Inajulikana kuwa hawa ni marafiki walioshibana ndani ya CCM na hata katika maisha ya kawaida. Ikiwa swahiba wao Lowassa atahamia CHADEMA/UKAWA, wanaweza nao kumfuata rafiki yao. Sasa ndugu zangu CHADEMA/UKAWA, mtakuwa radhi kuwapokea Andrew John Chenge na Rostam Aziz kuwa wanachama wenu?

Jibuni ili umma ufahamu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Mzee Tupatupa nadhani kwa hao sidhani kama hatawatathubutu maana kuna ile kesi ya ESCROW mh!!!!!!!!!!!!!!!Wakihamia tu Mkoa huu basi ujue wataozea JELA.

Na wakiwapeleka huko bora nihamie CCM maana atabaki mmoja na familia yake ambaye atakuwa rahisi kumtoa.

Ngoja tuwasubiri wenye CHAMA CHAO,siye wapangaji tumeambiwa kama hatutaki mafuriko tuhame MKOA.

Unajua nimewaza na kuwazua ila limeniumiza sana ,sasa kama mimi bintiyo ni mtu wa kawaida tu nimeumia hivyo Je,Mzee wangu Dr.Slaa,JJMnyika,Tundu Lissu hawa watakuwaje?Je Tundu Lissu atampigia kampeni Lowassa?Sielewi na sijui ila naogopa Uchafu umeingizwa rasmi mahali patakatifu.:crying::crying::crying:
 
Tupatupa ungenisaidia kitu kimoja kukielewa. Mbona ndani ya CCM iliyojaa uchafu na ghiliba nyingi mtu yeyote aliyekuwa akionekana kumuunga mkono Lowasa anafanyiwa mizengwe na kutishiwa hatima yake. Lakini wale waliokuwa wanajitokeza kumtukana na kumkashifu ndio wakawa wanazawadiwa vyeo na heshima wasizostahili kama Nape na Makonda?
Ukiona mchawi mmoja katika kundi la wachawi anachukiwa basi ujue pengine huyo sio mchawi bali yuko tuu ndani ya kundi la wachawi. Chuki za vigogo wa CCM kwa Lowasa zilikuwa za wazi kabisa, ila nguvu yake ilikuwa mtaji wa wanachama masikini na wengi wa CCM, na kama watahamisha support hiyo kutoka CCM na kumfuata Ukawa basi October ni kilio kikubwa ndani ya chama tawala.
 
Tutawapokea tu shida yetu sisi ni Madaraka basi.
Tupo tayari kufanya chochote ili tupate Madaraka , Kwani Kuna tatizo?
Halafu hiki Chama kina wenyewe ni Mali yetu binafsi tumetumia gharama kubwa kukifafanya kiwepo hapa kilipo.
Na hatukumuomba mtu awe mwanachama wetu ni kimbelembele chenu tu ndicho kilichowafanya mshabikie chadema hatukumuomba mtu.
 
daaaaah kweli..Leo Richmond imekuwa sio tatizo!! soon mtakuja badili na kusema escrow pia sio tatizo kama mama T nae atajiunga ukawa
Kila mtu anajua kwamba ESCROW siyo tatizo. Hawagawana pesa ya serikali. Waligawana pesa ya mtu binafsi ambaye alikwepa kodi. Kwa hiyo hawakuiba. Mwenye ushahidi kwamba waliiba aweke hadharani.
 
Mzee Tupatupa nadhani kwa hao sidhani kama hatawatathubutu maana kuna ile kesi ya ESCROW mh!!!!!!!!!!!!!!!Wakihamia tu Mkoa huu basi ujue wataozea JELA.

Na wakiwapeleka huko bora nihamie CCM maana atabaki mmoja na familia yake ambaye atakuwa rahisi kumtoa.

Ngoja tuwasubiri wenye CHAMA CHAO,siye wapangaji tumeambiwa kama hatutaki mafuriko tuhame MKOA.

Unajua nimewaza na kuwazua ila limeniumiza sana ,sasa kama mimi bintiyo ni mtu wa kawaida tu nimeumia hivyo Je,Mzee wangu Dr.Slaa,JJMnyika,Tundu Lissu hawa watakuwaje?Je Tundu Lissu atampigia kampeni Lowassa?Sielewi na sijui ila naogopa Uchafu umeingizwa rasmi mahali patakatifu.:crying::crying::crying:

Nimekuwekea bandiko langu kwenye Jukwaa la Uchaguzi Tanzania. Kajisomee binti yangu Tetty

Mzee Tupatupa
 
Last edited by a moderator:
Inajulikana kuwa hawa ni marafiki walioshibana ndani ya CCM na hata katika maisha ya kawaida. Ikiwa swahiba wao Lowassa atahamia CHADEMA/UKAWA, wanaweza nao kumfuata rafiki yao. Sasa ndugu zangu CHADEMA/UKAWA, mtakuwa radhi kuwapokea Andrew John Chenge na Rostam Aziz kuwa wanachama wenu?

Jibuni ili umma ufahamu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Mkuu tupatupa unashindwa kuelewa..... Watanzania na vijana wengi tumechoshwa na SHETANI/ZIMWI/FEDHULI/WEZI CCM, Hata kama UKAWA wangesimamisha jiwe ligombee urais ningelipigia kura yangu.
 
At least Leo umeuliza swali pasi na kuonesha unafiki
Unadhani kauliza kwa kupenda huyu ni team Slaa, kaumia sana Slaa kukatwa na nafasi yake kupewa Fisadi.

Si unajua Slaa ndiyo alimuita Lowassa Fisadi sasa kibao kimegeuka.
 
Safari hii hata kura inayotoa funza tutaitumia ili mradi CCM ing'oke madarakani.
 
El apewa Othman Masoud kuwa mgombea mwenza.
Masoud ni mwanasheria mkuu wa Zanzibar aliefukuzwa kwa kukataa katiba ya chenge.
Ni kijana msomi na makini
Timu imetimia na mechi imenogaa
 
Tupatupa ungenisaidia kitu kimoja kukielewa. Mbona ndani ya CCM iliyojaa uchafu na ghiliba nyingi mtu yeyote aliyekuwa akionekana kumuunga mkono Lowasa anafanyiwa mizengwe na kutishiwa hatima yake. Lakini wale waliokuwa wanajitokeza kumtukana na kumkashifu ndio wakawa wanazawadiwa vyeo na heshima wasizostahili kama Nape na Makonda?
Ukiona mchawi mmoja katika kundi la wachawi anachukiwa basi ujue pengine huyo sio mchawi bali yuko tuu ndani ya kundi la wachawi. Chuki za vigogo wa CCM kwa Lowasa zilikuwa za wazi kabisa, ila nguvu yake ilikuwa mtaji wa wanachama masikini na wengi wa CCM, na kama watahamisha support hiyo kutoka CCM na kumfuata Ukawa basi October ni kilio kikubwa ndani ya chama tawala.

Huo ndio utaratibu wa kichama

Mzee Tupatupa
 
Mkuu,mimi sikuwahi kuwa team ya Lowassa. Ni mchafu mtu huyu

Mzee Tupatupa

"Mwenye ushahidi kuwa mimi ni fisadi anipeleke mahakamani akanishtaji" mwisho wa kumnukuhu Lowassa

Hofu iko wapi kwenye kutekeleza kauli hii kutoka ndani ya kinywa chake?
uchafu huu ni uchafu gani usioshitakika?
 
Inajulikana kuwa hawa ni marafiki walioshibana ndani ya CCM na hata katika maisha ya kawaida. Ikiwa swahiba wao Lowassa atahamia CHADEMA/UKAWA, wanaweza nao kumfuata rafiki yao. Sasa ndugu zangu CHADEMA/UKAWA, mtakuwa radhi kuwapokea Andrew John Chenge na Rostam Aziz kuwa wanachama wenu?

Jibuni ili umma ufahamu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Mkuu labda kama utakua mbali sana na dhana ya objectives....

Mfano mwalimu anapofundisha darasani huwa kuna specific objectives ambazo mwisho wa somo mwalimu na mwanafunzi wanatakiwa wazifikie... mfano ukifundisha tenses objectives ni kwamba mwisho wa somo wanafunzi waelewe dhana ya tenses na waweze kuzitumia....

ukirudi kwa UKAWA/CHADEMA malengo yao ni kujenga jamii safi isiyo na mawaa....

Wanapohubiri ufisadi maana yake wanataka watu waache na kutubu!!! Sasa kama mtu amekolea na somo na yupo tayari kubadilika hayo sio mafanikio ya objectives??

Labda kama upo mbali na dhana ya Objectives!!!
 
Mkuu,mimi sikuwahi kuwa team ya Lowassa. Ni mchafu mtu huyu

Mzee Tupatupa

Kwa Nini UKAWA Wameamua LOWASSA Awe Mgombea wao wa Urais??..... Tundu Lissu Amelijibu Swahi hili kwa Ufasaha Kabisa hapo chni:

Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now.

Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007.

Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais.

Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais??? Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande.

Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010.

Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma. Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana.

Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach.

Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote. Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake:Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi.??

Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala.

Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.
 
Agenda ya kuu ya UKAWA kwa sasa ni kuuondoa mfumo kandamizi wa CCM na kuusambaratisha kabisa. Yeyote anayeweza kutoa mchango wa kufanikisha hili bila kujali anaitwa fisadi dagaa au fisadi papa anakaribishwa. Tunaisambaratisha CCM kwanza halafu mengine baadaye!!!
 
Lowassa akiihama CCM ni vyema aambatane na kupe wake.

Naishauri CCM kwamba wasipoondoka kwa hiari,iwakate maana ili kichaa asikusumbue,mswage na makopo yake.
 
Inajulikana kuwa hawa ni marafiki walioshibana ndani ya CCM na hata katika maisha ya kawaida. Ikiwa swahiba wao Lowassa atahamia CHADEMA/UKAWA, wanaweza nao kumfuata rafiki yao. Sasa ndugu zangu CHADEMA/UKAWA, mtakuwa radhi kuwapokea Andrew John Chenge na Rostam Aziz kuwa wanachama wenu?

Jibuni ili umma ufahamu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Hawana namna, tunaizika rasmi chadema sasa na ukawa yao!Viva CCM chama cha wakulima na wafanyakazi!Nimemkubali Komredi Kinana na Mangula
 
Back
Top Bottom