Nategemea wanachama wapya wa CDM kuwa wafuatao.
Chenge, Karamagi, Tibaijuka, Rugemalila,Rostam, na bandidu wote wa mjini waliokuwa wanaitwa mafisadi, maana sasa wameshapata jeuri na pa kujidaia bila kuulizwa maswali.
Hivi Mbowe alikunywa mbege ya wapi?maana sasa CDM wanaingia kwenye defence mode ambayo CCM imekuwepo kwa miaka 8 iliyopita.
Kwa kweli siku nyengine mchague wenyeviti wenye angalau akili ya kufanya SWOT analysis.
Ninaamini kabisa Dr.Slaa, Tundu Lissu na wengine wamekubali kwa shingo upande, kwani hawana pa kwenda,washaongelea mbovu kila chama kwa midomo yao mirefu, sasa inabidi kujikaza kiume na kukenua meno kama mataahira pale watakapoambiwa waanze kumnadi ajenda kuu ya mikutano yao just a year ago...,FISADI MKUU.
Yani CDM kuna kitu hawajui.., wamejiweka kwenye catch 22 ya hatari.., ama wakubali kwa miaka 8 walikuwa wanawadanganya wananchi willingly just kupata umaarufu, au wakubali kuwa wameanza kuwadanganya wananchi kuanzia sasa hivi just kuingia Ikulu.
kwani kama wanatuambia Lowassa si fisadi kwa kuwa hakuwahi fikishwa mahakamani kwa ufisadi, asilimia 99 ya mikutano yao ilikuwa uongo walioujua dhahiri, na kama wanasema wamejua leo hii kuwa hakuwahi kuwa fisadi, basi hawafai zaidi, kwani walikurupuka kuaminisha watu vitu wasivyo na uhakika navyo.