Hayo majibu ya Makene yako robo, sio lazima ukimbie kujibu bila ya kuwa na collective responsibility.
Makene hapo umepwaya sana kwa majibu ya kuedit.
Siyo lazima ujibu haraka ili uonekane unafanya kazi, bali umejidhalilisha sana kwa kutoa majibu yanayoonyesha ubishi dhidi ya hoja nzito na zilizopangiliwa za Chatanda.
Makene kwa hili umechemka, hakuna sehemu hata moja uliojaribu kujibu hoja au kutoa msimamo wa chama bali umetengeneza sintofahamu dhidi ya uwezo wenu wa kufikiri ulivyo kwasasa hapo ofisi zenu za makao makuu.
Mbona hukujibu hoja za Makamu Mwenyekiti Ndg Arfi?
Mbona hukujibu hoja nzito za Prof. Baregu?
Mbona hukujibu hoja za mara ya pili za Ndugu Mwigamba?
Mbona hujajibu hoja za mjumbe wa Baraza kuu kutoka Temeke?
Mbona hujajibu hoja za vijana wa Vyuo vikuu?
Mbona hujatoa ufafanuzi kwanini Mabere Marando kaondolewa kwenye nafasi yake bila Taarifa?
Kwa ufupi chama chenu mpaka sasa kimevurugwa, kuna haja mjipange au muwe kimya ili mjue nyufa zilizoko nyuma ya huu Mtikisiko na Mahitaji ya Majibu Mujarabu dhidi ya hoja muhimu zinazoibuka kila uchao.