CHADEMA Tutumie Kanda na Matawi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,582
2,000
Natoa ushauri kwa CHADEMA kuongeza kasi katika ofisi za kanda na matawi.

Kila tawi linajua idadi ya wanachama na mahali walipo, watumike kueneza na kuhimiza kujiandikisha na kujiandaa kupiga kura 2014 Serikali za mitaa.

Wanachama na wananchi wapo tayari kuchangia katika harakati za kukomboa nchi.
 

bujash

JF-Expert Member
Aug 9, 2013
3,468
0
umesomeka mkuu,kila MwanaCDM alipo atambue wajibu huo na autekeleze kwa maslahi mapana ya nchi yetu!
 

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
47,817
2,000
Wewe kijana huko nchi gani? Hivi ujui kama chadema himekufa

Sasa hivi si chadema ni UKAWA.
 

TEKNOLOJIA

JF-Expert Member
Jan 6, 2014
4,306
2,000
Natoa ushauri kwa CDM kuongeza kasi katika ofisi za kanda na matawi.

Kila tawi linajua idadi ya wanachama na mahali walipo, watumike kueneza na kuhimiza kujiandikisha na kujiandaa kupiga kura 2014 Serikali za mitaa. Wanachama na wananchi wapo tayari kuchangia katika harakati za kukomboa nchi.

Unawashauri wrong politicians, Wenzako tumeshauri wee hadi vichwa vinatuuma lakini mambo yapo vile vile!Hawa viongozi wa CHADEMA wanakatisha tamaa kwakweli.Chama kinaendeshwa kisela sela tu.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
77,582
2,000
Bila shaka yoyote ushauri wako utafanyiwa kazi , MABORESHO YA DAFTARI NDIYO KIFO CHA CCM .
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
77,582
2,000
Unawashauri wrong politicians, Wenzako tumeshauri wee hadi vichwa vinatuuma lakini mambo yapo vile vile!Hawa viongozi wa CHADEMA wanakatisha tamaa kwakweli.Chama kinaendeshwa kisela sela tu.

majungu hayajawahi kumfanya mtu apate maendeleo .
 

Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Natoa ushauri kwa CHADEMA kuongeza kasi katika ofisi za kanda na matawi.

Kila tawi linajua idadi ya wanachama na mahali walipo, watumike kueneza na kuhimiza kujiandikisha na kujiandaa kupiga kura 2014 Serikali za mitaa.

Wanachama na wananchi wapo tayari kuchangia katika harakati za kukomboa nchi.

Kuanza kulenga matawi na mashina leo, kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka huu na mwakani, is a bit too late. Hilo linapaswa kuwekwa kwenye long term strategy plan.

Kwa sasa nadhani kinachotakiwa ni kuhakikisha zoezi la kuhakiki na kuboresha Daftari la Kudumu la Wapigakura linafanyika vizuri na kwa muda wa kutosha. Pia kuna haja ya kupeleka mashambulizi kwenye sheria za uchaguzi na zinazounda Tume ya CCM ya uchaguzi. Mambo haya yaende sambamba na kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa:

1. Wananchi wote kujitokeza kujisajili katika Daftari la kudumu la wapiga kura

2. Wananchi kushiriki kupiga kura muda ukifika

3. Wananchi kuacha tabia ya kuuza vitambulisho vyao vya upigakura, kwani kufanya hivyo ni kupoteza haki ya kupiga kura.

4. Kuthamini kura zao, kwani ni za msingi katika kuleta mabadiliko ya aina na muundo wa utawala.

Nadhani mpaka sasa binafsi siridhishwi kabisa na spidi ya ushughulikiaji wa mambo hayo!

Najua wengi kati yetu tulidhani mpaka kufikia uchaguzi mkuu, tume na sheria vitakuwa vimeshashughulikiwa automatically na Katiba Mpya, lakini ni wazi katiba ndiyo imefeli kwa sasa naitakuja kwa wakati wake. Kwa hiyo nilidhani watu wanatakiwa kubadili mbinu haraka na kupeleka mashambulizi kwenye malengo ya muda mfupi, lakini naona na hilo nalo halipo.

Ukweli ni kwamba, hii katiba imekwamishwa kwa makusudi. Na ni kweli kuwa kutegemea ipatikane ndani ya muda uliobaki, ni kitu kigumu. Sasa hayo mengine ya sheria, tume na Daftari nayo yasiposimamiwa vema na kwa wakati, itafikia muda wa uchaguzi umefika, Vyama vitasusia uchaguzi na uchaguzi hautafanyika. Hili nalo linafanyika kwa makusudi.

Nadhani tuhamishie mashambulizi upande mwingine, hayo matawi, na katiba vitakuja kwa wakati wake, maana ni kati ya vitu ambavyo huwezi kuvipata kwa spidi ya kulipua. Ukweli ni kuwa kukumbuka jana tulifanyaje tunahitaji kuangalia leo tukoje, lakini kujua kesho itakuwaje, tunapaswa kuangalia leo tunafanya nini!

cc: Dr.W.Slaa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom