CHADEMA tuokoeni wana Kigamboni

Mkuu, unataka Chadema wawaokoe kivipi? Fafanua

Sawa kabisa Ritz ,kwa lipi elezea ili usaidiwe.Kulipia 100 au unataka watoe msaada kama magamba mil 500 jimboni ili mgawane nakulipia hiyo 100 nyingine?
 
CDM hawa watu hawana maana ni Mandumilakwili :eyebrows:! nadhani wajibange kwa 2015! Alafu wajue tunahitaji kuendelea hii nchi kodi zetu ndio maendeleo yetu.Gharama za maisha juu sana na mafuta ndio usisemeee!! hata wabunge wameongezewa Posho.Hivi ninyi wanakingamboni kile kivuko kinatumia maji ya bahari kujiendesha,Mbona nauli za daladala hamkupiga kelele.Dr.magufuli Big up mi nadhani katika mwaka wa bajeti ufuatao ikiwezekana kifanane na gharama za Chato au Pangani na wakibisha waje huku Pangani waone tunavyojitoea kuleta maendeleo.Sidhani kama CDM kwenye hoja ya maendeleo wakawa wapinga maendeleo.tumechoka ubabaishaji kama wa wanasiasa wa dar.Tubadilike

mchotile, Hakika uko sawa kabisa kwani wewe umeshindwa kuelewa kuwa population ya kigamboni na hali za watu hawa wanaoishi huku ni chini kabisa, sasa wewe mchotile unaposema kuwa kivuko kijiendeshe chenyewe, unajua pato la kila siku hapa fell? ama ndugu yangu mchotile umekurupuka!! tafakari hapa ....

Umeweza kujiuliza kwa yule kibarua aliyeajiria kwa muhindi, mshahara wake ni sh 120, 000 na anakwenda kwa siku 6 kwa wiki kazini (go and return ) kwa mwezi mzima atakuwa ametumia sh 15000 kwenye kivuko tu. na hapo asiwe anaishi kibada, Geza ulole ,Vijibweni au Kisiwani. sasa mchotile ongeza 28, 000 za daladala toka hapo fell mpaka mtu huyo anapoishi. Kama atakuwa anafanyia kazi mwenge ama ubungo atakuwa na ongezeko la sh 24, 000, Jumla itakuwa sh 67, 000. ukitoa sh 120000 ambao ndiyo mshahara unamkuta mtu yule anabaki na ......... jaza mwenyewe.

Na ndiyo maana mchotile ninasema Chadema waingilie kati ili watunusuru na gharama zisizokuwa za lazima.please try to analyse the figure na usikurupuke mchotile.

mchotile vipato vyetu viko chini sana ndugu yangu.
 
..........Umeweza kujiuliza kwa yule kibarua aliyeajiria kwa muhindi, mshahara wake ni sh 120, 000 na anakwenda kwa siku 6 kwa wiki kazini (go and return ) kwa mwezi mzima atakuwa ametumia sh 15000 kwenye kivuko tu. na hapo asiwe anaishi kibada, Geza ulole ,Vijibweni au Kisiwani. sasa mchotile ongeza 28, 000 za daladala toka hapo fell mpaka mtu huyo anapoishi. Kama atakuwa anafanyia kazi mwenge ama ubungo atakuwa na ongezeko la sh 24, 000, Jumla itakuwa sh 67, 000. ukitoa sh 120000 ambao ndiyo mshahara unamkuta mtu yule anabaki na ......... jaza mwenyewe.......

Sasa wale wanaoishi maeneo ya Goba, Kimara, Tegeta na wanafanya kazi huko kwa wahindi Kariakoo, jee wao huwa wanafanya nini kuweza kufika kazini? Au wa Kigamboni tu ndiyo wa kufikiriwa?

Jengine, jana Magufuli aliwakaribisha Wabunge wakakodi hicho kivuko na wakiendeshe, nadhani ni wakati wao wajipange halafu wamwonyeshe kwamba inawezekana kuwavusha watu wa Kigamboni kwa shilingi 50 na bado ukapata faida.
 
Ni siku tano sasa tangu lile ongezeko la nauli limeanza kutelezeka, hakika mambo yanakwenda ndivyo sivyo. kwa kawaida mtu anaweza kudhani sisi ni walalamishi tusiyopenda kuchangia pato la taifa ( cost shareling) shida inakuja pale hata pale bei ya mizigo ilipopanda,

Mfano mwenye guta ( baiskeli ya miguu mitatu sh ni 3500, sasa kiuchumi zile cost anazibeba mlaji wa bidhaa hizo, bei hizi zimepanda mara dufu.

Kwa wale wanafunzi wa vyuo(IFM, MAGOGONI , DIT, CBE Pamoja na Mwalimu nyerere memorial academy) wamepndishiwa nauli sasa ni sh 200



Niko kanda ya ziwa lakini hapo ulipo nakuona,
Usitudanganye sisi watu wazima, vyakula haviwezi kupanda kwa hiyo bei kuongezeka.
Kwanza Viazi vya Dar vinatoka na samaki zainatoka huko huko Kigamboni kwa hiyo bei itashuka kama hamtavusha.
Unalalamika Tsh.200 mwanafunzi wa Mabibo Hostel asemaje anaesoma UDSM?
Hamko Serious badala ya kulalamikia mafuta, yashuke ili gharama uendeshaji zisiwe juu nyie mnalalamikia mlipoangukia pua
 
cdm hawa watu hawana maana ni mandumilakwili :eyebrows:! Nadhani wajibange kwa 2015! Alafu wajue tunahitaji kuendelea hii nchi kodi zetu ndio maendeleo yetu.gharama za maisha juu sana na mafuta ndio usisemeee!! Hata wabunge wameongezewa posho.hivi ninyi wanakingamboni kile kivuko kinatumia maji ya bahari kujiendesha,mbona nauli za daladala hamkupiga kelele.dr.magufuli big up mi nadhani katika mwaka wa bajeti ufuatao ikiwezekana kifanane na gharama za chato au pangani na wakibisha waje huku pangani waone tunavyojitoea kuleta maendeleo.sidhani kama cdm kwenye hoja ya maendeleo wakawa wapinga maendeleo.tumechoka ubabaishaji kama wa wanasiasa wa dar.tubadilike
duh mchotile umeingia kwa kishindo yani leo leo umeingia na kumpa uyu kichomi magufuli big up?? Natmai we hauishi kigamboni, hakuna mandumilakuwili uku, we voted for cdm lakini changamoto ni kuwa hatukuzilinda kura zetu.bidhaa uku zimepanda bei kwa sababu ya ili tukio, wajua kati ya uku na upande wa pili bei ziko tofauti? Imagine ni bora kuvuka ukanunue just a 1kg ya mchele upande wa pili wa kivuko.pia zingatia km mbunge anayepokea mamilioni ya shilingi kaona maisha ni magumu sasa jiulize sie waendesha maguta, na hii ni moja kwa moja tunabaliki inflation wkt wenzetu nchi jirani wanaumia vichwa jinsi ya kupunguza inflation, tunaongozwa na mavuvuzela.... ,
 
ni siku tano sasa tangu lile ongezeko la nauli limeanza kutelezeka, hakika mambo yanakwenda ndivyo sivyo. Kwa kawaida mtu anaweza kudhani sisi ni walalamishi tusiyopenda kuchangia pato la taifa ( cost shareling) shida inakuja pale hata pale bei ya mizigo ilipopanda,mfano mwenye guta ( baiskeli ya miguu mitatu sh ni 3500, sasa kiuchumi zile cost anazibeba mlaji wa bidhaa hizo, bei hizi zimepanda mara dufu.kwa wale wanafunzi wa vyuo(ifm, magogoni , dit, cbe pamoja na mwalimu nyerere memorial academy) wamepndishiwa nauli sasa ni sh 200nadhani sasa chademahuu ndiyo wakati wenu wa kulisimamia taifa kutoka kwenye uonevu wa watanzania wanyonge, semeni kitu ndugu zangu najua serikali hii itawasikiatumebaki mayatima hatuna hata mtetezi.
mwita unayoyasema ni sahihi, lakini huu upuuzi ambao watanzania kwa nafasi pia mahala petu tofauti tumekuwa tukiumizwa wadhani tufanye nini?? Hao cdm tunaowahita wamepigwa marufuku ata kufanya mikutano kwa kisingizio cha alshaabab, maandamano hayaruhusiwi, i am so serious to join maandamano kupaza sauti zetu lkn are well organised, au ndo tutaandaa move ndani umo wakiwamo makenge ya ccm pia???kaka naona bado tunasafari ndefu ya kwenda kuweza kuwasilisha mashinizo yetu, problem hatuko organized, na najua tutasikilizwa sana na kutekelezewa wanatikisa kiberiti, kwani awa wakubwa waoga sana, wakumbuka maandamano ya cdm wakati ule ata president aliogopa na akasema wanataka kuiangusha serikali hawa cdm, together we can but we are not organised
 
poleni wana wa kigamboni kwa ongezeko jipya la nauli ya sh,200 lakini idadi kubwa ya wanakigamboni imewaponza wanachama na wapenzi wetu wa CHADEMA ambao walishindwa kucheza karata zao vizuri kuwachagua viongozi ambao wangewatetea katika shida mbalimbali leo wabunge wetu wa mkoa wa Dar,wanajifanya watetezi wao wazuri walivyolilia posho mpya upatikanaji wake unatokana na kodi za aina hiyo. Ukitaka kujua wabunge wa mkoa wa Dar hawana utetezi wowote Watoto wa Shule za Msingi za mkoa wa Dar waliandamana hadi ofisi ya Mkuu wa mkoa wakati huo Abass Kandoro kumuomba awasaidie kupunguza nauli ya Daladala ambayo ilitoka shilingi 50 hadi 100 kwa mwanafunzi wabunge wote wa mkoa huu walikaa kimya watoto wale walipigwa Virungu na Mapolisi wa nchi hii bila aibu wengine ni watoto wao wengine wadogo zao lakini hawakujali hilo. msukumo wa wabunge wa Dar ulikuwa upi????????? kwa waziri mwenye dhamana????????? nawaomba wananchi wa kigamboni tulipe nauli mpya tujipange vizuri tuje kuwaadhibu mwaka 2015 kuwanyima kura kwa sasa wanawadanganya kwa vile wakati wa bajeti mwaka jana 2011 walipitisha na kuunga mkono bajeti ya wizara ya John Mgufuli hakuna aliyepinga katika hao ukiondoa Kijanawetu John Myika naye amjitummbukiza bila kujua kwanza namshauri aache kujiunga na umoja wa Magamba aachane nao akitaka afanye ziara ya peke yake au ziara ya kichama hao Wabunge wanataka sifa tu mwisho watampoteza kijana wetu ona sasa wanachadema tunaanza kupungukiwa na imani juu ya kuungana nao mbona wao kwenye jumuhiya yetu wanatuzomeaaaaaaaaaaaa.Anatory Mujwahuzia.
 
Tatizo watu wameweka mbele mapenzi ya vyama kuliko hata watanzania wenzao,hao mnaowabeza mjue 2015 mtawahitaji wawape kura hata kama last time waliipa CCM,labda kama Chadema haitahitaji kura za mbunge na Raisi kutoka kigamboni mwanasiasa anaangaalia future haangalii matokeo yaliyopita,na kwa attitude hii Chadema inaweza isishinde 2015.
 
Hakika hali hii ya kupandishiana nauli bila hata kujadiliana, mbaya zaidi kilio chetu tunakielekeza ktk chama cha Chadema ili watusaidie kulisemea hili, wana Jf mnatubeza na kutukumbusha 2010, hebu mnajua jinsi tulivyojitahidi kuipigia chadema kura? Nadhani tusaidieni kupiga kelele na kutubeza
 
hilo la kujenga nakuunga mkono, kigamboni imechelewa na itachelewa,walipaswa kuweka miundombinu na utaratibu wa uendelezaji,ununuzi na upimaji,kigamboni ingekua mbali sana.

Ila si mlimchamgua mbunge wenu kwa kishindo? Amesaidia vipi?



BADILI TABIA, unajua sisi wana Kigamboni tunaishi kwa presha sanaaa..mara tunahamishwa......mara mji mpya, ..... oooohh msijenge...., Dah.. sijui hata tufanye nini, sasa leo nauli juuu...... alafu mbunge wa CCM... YAANI NDUGU ZANGU HATUJUI HATA Kesho watasema nini.

BADILI TABIA mimi nadhani nauli ingeendelea kuwa sh 100 na kama wangeweza wanafunzi wa vyuo vikuu wavuke bure kwani vipato vyao ni duni
 
hilo la kujenga nakuunga mkono, kigamboni imechelewa na itachelewa,walipaswa kuweka miundombinu na utaratibu wa uendelezaji,ununuzi na upimaji,kigamboni ingekua mbali sana.

Ila si mlimchamgua mbunge wenu kwa kishindo? Amesaidia vipi?
Na hapa ndipo napopata wasiwasi na hisia zako, hebu wewe ndg yangu una uwakika kuwa niliwapigia Magamba kura?
 
Jamani nataka kuuliza swali..

Hivi Tanzania hakuna utaratibu wa bunge au City vyombo vya wananchi kikatiba kupitisha ongezeko la bei za huduma za Kitaifa?..Kwnai inanipa chachu kubwa sana napojaribu kumeza swala hili maanake mashindwa kuelewa waziri anawezaje kupitisha kupanda kwa nauli jinsi atakavyo baada ya yeye na wizara yake kufikia maamuzi..

Je, makosa ni ya Magufuli kukiuka kanuni au katiba yetu wenyewe ndio inayompa mamlaka haya, maanake maamuzi kama haya hufanywa na shirika binafsi sio wizara ya serikali ama shirika la Umma..Jambo lolote linaloamriwa na waziri wa wizara huku majuu mara zote lazima liwe limepitishwa na bunge..
 
Jamani nataka kuuliza swali..

Hivi Tanzania hakuna utaratibu wa bunge au City vyombo vya wananchi kikatiba kupitisha ongezeko la bei za huduma za Kitaifa?..Kwnai inanipa chachu kubwa sana napojaribu kumeza swala hili maanake mashindwa kuelewa waziri anawezaje kupitisha kupanda kwa nauli jinsi atakavyo baada ya yeye na wizara yake kufikia maamuzi..

Je, makosa ni ya Magufuli kukiuka kanuni au katiba yetu wenyewe ndio inayompa mamlaka haya, maanake maamuzi kama haya hufanywa na shirika binafsi sio wizara ya serikali ama shirika la Umma..Jambo lolote linaloamriwa na waziri wa wizara huku majuu mara zote lazima liwe limepitishwa na bunge..

si unawajua watanzania ndugu yangu, magufuli yupo sahihi ajavunja sheria yoyote na ndio maana kawajibu wabunge wa dar kuwa ni wao wenyewe wabunge kwa ujumla walipitisha sheria ya kumpa waziri mamlaka ya kuongeza nauli, labda hapo mada zinachanganywa!
 
si unawajua watanzania ndugu yangu, magufuli yupo sahihi ajavunja sheria yoyote na ndio maana kawajibu wabunge wa dar kuwa ni wao wenyewe wabunge kwa ujumla walipitisha sheria ya kumpa waziri mamlaka ya kuongeza nauli, labda hapo mada zinachanganywa!
Alaaa kumbe wabunge ndio walipitisha sheria? sasa nadhani inabidi wakuu zangu tuzame ktk swala hili vizuri sana kuwabana hawa wabunge wenyewe maana naona kila mtu anamlalamikia Magufuli ningependa sana kuwajua wabunge waliounga mkono bungeni kuongezeka kwa nauli za Kigamboni...maana isiwe mchezo wa kinafiki mtupu.
 
Vuneni mlichopanda sasa. Wakati wa uchaguzi simnaweka akili uvunguni,na mnatumia masaburi kupiga kura?:lol::lol: now ndio mnawakumbuka CDM? kwani mbunge na madiwani mliowachagua wako likizo?Nyasi Mtakula na Kama vp pigeni mbizi, hii ndio CCM
 
Back
Top Bottom