CHADEMA tuokoeni wana Kigamboni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA tuokoeni wana Kigamboni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by IsayaMwita, Jan 5, 2012.

 1. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ni siku tano sasa tangu lile ongezeko la nauli limeanza kutelezeka, hakika mambo yanakwenda ndivyo sivyo. kwa kawaida mtu anaweza kudhani sisi ni walalamishi tusiyopenda kuchangia pato la taifa ( cost shareling) shida inakuja pale hata pale bei ya mizigo ilipopanda,

  Mfano mwenye guta ( baiskeli ya miguu mitatu sh ni 3500, sasa kiuchumi zile cost anazibeba mlaji wa bidhaa hizo, bei hizi zimepanda mara dufu.

  Kwa wale wanafunzi wa vyuo(IFM, MAGOGONI , DIT, CBE Pamoja na Mwalimu nyerere memorial academy) wamepndishiwa nauli sasa ni sh 200

  Nadhani sasa Chadema huu ndiyo wakati wenu wa kulisimamia Taifa kutoka kwenye uonevu wa watanzania wanyonge, semeni kitu ndugu zangu najua serikali hii itawasikia

  Tumebaki mayatima hatuna hata mtetezi.
   
 2. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Umesikika!
   
 3. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kwanini hamkuwachagua kwenye udiwani na ubunge?
  leo ndio mnaona umuhimu wao?
   
 4. d

  davidie JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mliwaona hawafai mkakubali kupokea kofia na kangaleo mnawaona wanamsaada kwenu?
   
 5. Igabiro

  Igabiro JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Acha unafiki wewe ubunge mmechagua CCM kwenye shida ndio unakumbuka CHADEMA, beba zigo hilo la hali zaidi, kasi zaidi na nguvu zaidi....
   
 6. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  Hapo ndo tulibugi, tulipewa kanga, chunvi za viroba na vijisenti kidogo tukawanyima kura, natumai lazima tufundishwe adabu kwani tumekuwa tukidanganywa tangu 1990 na serikali lafi hii ya ccm lakini bado hatujitambui, hili ni funzo ili siku nyingine tutie adabu.ni wazi hatukutaka watetezi wa kweli tukawachagua walafi ndo haya tunayaona na cha moto tunakipata ivyo tuwe wapole tukiingizwa katika lindi ili la umasikini na kuumizwa ayo ndo maisha bora tulokimilia na kuyachagua.nashauri tuangalie pia tujipanga kwa next time, kwani hii ndo ishakula kwetu, majuto ni mjukuu, tusoweza basi tupige mbizi kama walivyosema watawala wetu
   
 7. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Igabiro

  Ndudu yangu hapa utakuwa haututendei haki, sisi tulikichagua chama cha CHADEMA na ndiyo maana mama ANA KOMU alipata kura 38 elfu hizi ni pamoja na kura yangu mimi, sasa leo unaponihukumu tena kwa kejeli, nadhani hii siyo haki.

  Igabiro sasa hapa unataka kuwaaminisha wana JF kuwa sisi wana kigamboni hatukipendi chama cha CHADEMA? napenda wewe Igabiro ulione ongezeko hili kama tatizo kwa watanzania wanyonge kama mimi.
   
 8. M

  MAJANI YA KUNDE JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Zamani nilijua Kigamboni ni ya wazaramo maana walivyoipenda CCM kumbe wapo mchanganyiko.cham msingi Wanakigamboni vumilieni hayo ni malipo ya kofia ,Kanga,fulana na pilau.CHUKUA CHAKULA MAPEMA SHIDA ZAKO BAADAE.Chadema wala msiingilie ngoma hii wanajuana hao waziri wa CCM,wabunge CCM,wapandaji Kivuko CCM.Mnakula jeuri yenu.
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  unataka wafanyaje? Wanunue kivuko wachaji sh 100 mtu au 700 gari?
   
 10. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  KASHOROBANA

  Nadhani kanga, chunvi za viroba na vijisenti kidogo wengine havikutufikia, labda wewe ulivipewa lakini mimi sikuviona.
  Kashorobana, zingitia maada, ombi letu ni kuhamasisha Chadema iseme chochote kuhusu upandaji wa bei za nauli, najua serikali itasikia kulifanyia kazi, sasa wewe unafanya mzaha.................be careful my friend
   
 11. K

  KIROJO Senior Member

  #11
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mama wa watu(Kombo)kupitia CDM alipiga kampeni hamukumsikiliza mkahongwa masufulia ya wali,kofia na kaka,vitenge sasa ndo mnaona CDM ndo kimbilio,mimi naona mpate kwanza fundisho ndo akiri itakaa sawa,sisi na huku tegeta wala ,tuko shwari
   
 12. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  BADILI TABIA, unajua sisi wana Kigamboni tunaishi kwa presha sanaaa..mara tunahamishwa......mara mji mpya, ..... oooohh msijenge...., Dah.. sijui hata tufanye nini, sasa leo nauli juuu...... alafu mbunge wa CCM... YAANI NDUGU ZANGU HATUJUI HATA Kesho watasema nini.

  BADILI TABIA mimi nadhani nauli ingeendelea kuwa sh 100 na kama wangeweza wanafunzi wa vyuo vikuu wavuke bure kwani vipato vyao ni duni
   
 13. kadeti

  kadeti JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 491
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  macho na masikio kwa wabunge wa Dar tusikie na tuone watafanya nini?
   
 14. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  KIROJO, sasa unajua alipata kura ngapi mkuu? ni kweli kwamba mama alifanya vizuri katika uchaguzi ule ila tuu kura hazikutosha, najua wewe uko pembezoni sana, haujua geografia ya kigamboni, watu wake , bado kuna kila sababu ya kupeleka elimu ya urai hapa Kigamboni.
   
 15. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kadeti unawaongelea wabunge gani hao?
   
 16. m

  mchotile New Member

  #16
  Jan 5, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CDM hawa watu hawana maana ni Mandumilakwili :eyebrows:! nadhani wajibange kwa 2015! Alafu wajue tunahitaji kuendelea hii nchi kodi zetu ndio maendeleo yetu.Gharama za maisha juu sana na mafuta ndio usisemeee!! hata wabunge wameongezewa Posho.Hivi ninyi wanakingamboni kile kivuko kinatumia maji ya bahari kujiendesha,Mbona nauli za daladala hamkupiga kelele.Dr.magufuli Big up mi nadhani katika mwaka wa bajeti ufuatao ikiwezekana kifanane na gharama za Chato au Pangani na wakibisha waje huku Pangani waone tunavyojitoea kuleta maendeleo.Sidhani kama CDM kwenye hoja ya maendeleo wakawa wapinga maendeleo.tumechoka ubabaishaji kama wa wanasiasa wa dar.Tubadilike
   
 17. msweken

  msweken Senior Member

  #17
  Jan 5, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 191
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Onyesha kwanza juhudi zako za kujiokoa ili uokolewe!!
   
 18. K

  KIROJO Senior Member

  #18
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapi elimu ya uraia wapi Tungi,au tuangoma,au wapi hao watu wa kigamboni lazima mpate adhabu kwanza ili mjifunze kwa kufanya kosa, sisi tulilinda kura ,tulitoa macho hatukulala nyie mlifiki haki unapewa tu inatafutwa
   
 19. knownless

  knownless Senior Member

  #19
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  nafikiri swala la watu kulipa 200 ni sawa kwa vile si kubwa sana kulingana vivuko vingine,lakini kwenye baadhi ya vyombo vya usafiri bei yake haina uwiano.

  Muwatumie hao hao vichwa maji mliowachagua for the time being huku mkingoja kufanya mabadiliko 2015
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mkuu, unataka Chadema wawaokoe kivipi? Fafanua
   
Loading...