CHADEMA, Tunaomba Bango hili Kila wilaya...

Mlachake

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
4,412
4,559
Naomba Bango hili liwe na Maandishi haya.

''MWISHO WA UZALILISHAJI HUU 2015''

attachment.php
 
hii ni fedheha kabisa, sasa hiyo mi baba khanga za nini? duh naomba mungu atusaidie watanzania
 
Kudadadeki wameua viwanda ili waje watupe kanga ili tuwape kula,hao wababa wanagombea wapeleke zawadi kwa wake zao.
 
Kwa hiyo wana jf huyu nepi hizo bidhaa huwa anatembea nazo kwenye gari lake?2015 labda wazipeleke somalia
 
inaniuma sana,nawachukia roho zao mbaya wantumia umaskini wa wazee wetu.
Kweli kabisa ccm inawanyanyasa wazee wetu. Naomba vijana tubadirike tusiwafuate akina Nape kwa udhalilishaji huu maana ni ahibu kwa kijana kufanya mambo ambayo ccm inafanya.
 
Naomba Bango hili liwe na Maandishi haya.

''MWISHO WA UZALILISHAJI HUU 2015''

attachment.php
Nape, muogope Mungu! Yaani hao wazee unawaimbisha sandakalaweee, aminaaa, mwenyekupataaa, apateeee! Wadau mnakikumbuka hicho kibwagizo? I wish mzee Nnauye(rip) angekuwepo akashuhudia huu upuuzi wako!
 
Nape anafurahia umaskini wa watanzania.Angalia tabasamu lake.Hata enzi za utumwa wanaume hawakugombania kanga.
 
Du Jamaa kawadhalilisha sana hawa wazee wetu. Watetea haki za binadamu mko wapi? Hii jamani haitakiwi iwe published, jirani zetu Kenya na Uganda wakiona watatudharua sana watanzania. si akavae yeye na mkewe haya makanga yake.
 
Nilikuwa naipenda sana CCM ila picha hii imenihuzunisha sana, imenisononesha sana. Hivi ingekuwa ni mama yangu au baba yangu ndo anaonekana hapo ningeuweka wapi uso wangu. Nataka kadi ya CDM sasa.
 
Back
Top Bottom