GE2025 CHADEMA: Toka Oktoba 1 hadi 9, 2025 wametekwa watu 13! Ni karibu watu wawili kila siku!

GE2025 CHADEMA: Toka Oktoba 1 hadi 9, 2025 wametekwa watu 13! Ni karibu watu wawili kila siku!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
2,786
Reaction score
7,567
Salam Wakuu,

Hali imezidi kuwa mbaya nchini aisee! Yaani kila siku wanatekwa watu wawili, tumekuwa nchi ya ajabu sana! Na hawa ni wale wanaorekodiwa, halafu kuna wale ambao wanapotea kimyakimya taarifa hazifiki mtandaoni!

Tuendelee kuchukua tahadhari na kujilinda huku tukikosoa yanayofanyika, team Oktoba 29, cheza kwa step, watu wako kazini kusikiliza na kuzima sauti, hata muuza genge hapo mtaani kwako anaweza ndio akawa mchomaji! Cheza kwa step

=====

TAARIFA YA UTEKAJI

Chadema tumefuatilia kwa karibu matukio mbalimbali ya utekaji wa watu yaliyotokea nchini ndani ya siku tisa kuanzia tarehe 01 hadi 09 Oktoba 2025. Katika kipindi hiki, jumla ya watu 13 wametekwa, wengi wao ni viongozi na wanachama wa Chadema, pamoja na baadhi ya wanachama wa vyama vingine vya siasa na wananchi wa kawaida. Matukio haya yamezua wasiwasi mkubwa miongoni mwa jamii kuhusu usalama na uhuru wa raia. Matukio hayo ni kama yafuatayo:

LOBEZI KULILO MASANYIWA
Mnamo tarehe 01 Oktoba 2025, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Chadema Wilaya ya Busega alitekwa na watu wasiojulikana akiwa kazini kwake Nyamikoma. Mashuhuda wameripoti kuwa alitishiwa kwa bunduki na kulazimishwa kuingia kwenye gari na watu waliokuwa wamejifunika nyuso zao, kisha kuondoka naye kuelekea Barabara ya Mwanza. Hadi sasa hajulikani alipo.

ISSA HAMISI KAUDO
Mnamo tarehe 03 Oktoba 2025, Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Ikungi alitekwa na watu wasiojulikana baada ya kupokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kama mfanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, aliyemwomba afike kwa ajili ya kazi ya kuchomelea. Alipofika eneo la miadi, alilazimishwa kuingia kwenye gari aina ya Land Cruiser na kuondoka nao kusikojulikana. Tangu wakati huo, hajulikani alipo.

PAUL VESLASM
namo tarehe 03 Oktoba 2025, dereva bodaboda alitekwa baada ya kuchukuliwa na Issa Hamisi Kaudo kwenda Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, akielezwa kuwa kuna kazi ya kufanya. Alipofika kwenye eneo hilo, waliokuwepo walimuingiza kwa nguvu kwenye gari aina ya Land Cruiser na kuondoka naye kusikojulikana. Hadi sasa hajulikani alipo.

EVARIST JAMES RAMADHANI
Mnamo tarehe 03 Oktoba 2025, Mwenyekiti wa Bavicha Jimbo la Ikungi alitekwa akiwa nyumbani kwake baada ya kupigiwa simu na kuambiwa atoke nje. Tangu alipotoka, hajarejea nyumbani na hajulikani alipo hadi sasa.01

AMOS PAMBALA
Mnamo tarehe 04 Oktoba 2025, Katibu Mwenezi wa Chadema Kata ya Mafisa, Jimbo la Morogoro Mjini alitekwa baada ya kupokea simu na kuitikia wito. Tangu wakati huo, amepotea na hajulikani alipo hadi sasa.

IBRAHIM MUHIDIN MFANGAVO NA VIJANA WENGINE WATATU
Mnamo tarehe 04 Oktoba 2025, katika Kijiji cha Kakola, Kata ya Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama, vijana wanne walitekwa na watu wasiojulikana. Wa kwanza kutekwa alikuwa Ibrahim Muhidin Mfangavo, aliyetekwa nyumbani kwao mbele ya baba yake mzazi, Mzee Muhidin Mfarangavo. Vijana wengine watatu walitekwa walipokuwa wakifuatilia kwa bodaboda waliomteka Ibrahim, wakijaribu kuwafuatilia na kusaidia, lakini nao wakakamatwa na kuondoka nao kusikojulikana.

ABEDNEGO SANGA
Mnamo tarehe 04 Oktoba 2025, Katibu wa Bavicha Jimbo la Lupembe alitekwa akiwa kazini kwake katika duka la dawa. Watekaji waliwasili kwa gari aina ya Land Cruiser lisilo na namba za usajili, wakiwa na silaha za moto, wakaingia ndani ya duka na kumwondoa kwa nguvu, kisha kuondoka naye kusikojulikana.

HUMPHREY POLEPOLE
Mwanasiasa na mwanadiplomasia maarufu wa Tanzania ametekwa kuanzia usiku wa tarehe 6 Oktoba 2025, baada ya watu wasiojulikana kuvamia makazi yake mjini Dar es Salaam.

ROGERS YOHANA LUDOVICK
Mnamo tarehe 03 Oktoba 2025, Mwenyekiti wa Bavicha Jimbo la Ikungi alitekwa akiwa nyumbani kwake baada ya kupigiwa simu na kuambiwa atoke nje. Tangu alipotoka, hajarejea nyumbani na hajulikani alipo hadi sasa.

RAMSOM
namo tarehe 07 Oktoba 2025, mtengenezaji wa maudhui mtandaoni kupitia Tik Tok, ambaye amekuwa mkosoaji wa utawala wa Rais Samia tangu mwaka 2024, alitekwa akiwa nyumbani kwake. Mpaka sasa hajaripotiwa kama amepatikana.

Tunatoa wito kwa Serikali na vyombo husika kuchukua hatua za haraka kuhakikisha usalama wa raia wote bila kujali Vyama itikadi za Vyama vya Siasa. Tunawahimiza wananchi kujilinda na kuwa makini katika kipindi hiki kigumu ambapo matukio ya utekaji yamekithiri.

Imetolewa leo Alhamisi, 09 Oktoba 2025
Brenda Rupia
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi02


utekaji1.jpg
utekaji2.jpg
 
Tarehe 29 Oktoba kazi ni rahisi sana

We kuwa na kiberiti na mafuta tu na chupa yoyote.

Mali ya kiongozi wa CCM yeyote ishughulikie tu.
 
CCM wanahangaika na Chadema ambao wamejitoa ktk uchaguzi

Hii ni sawa na kifo Cha mfa maji hakosi kutapata
 
Back
Top Bottom