CHADEMA, serikali tatu na serikali ya majimbo

CHADEMA, serikali tatu na serikali ya majimbo

Chadema ni bendela fuata upepo wao siku zote hawana hoja wanafuata yale yanayotokea kwenye jamii ndiyo wanaruka nayo.
Kiongozi anapaswa kumsikiliza nani? Anayemuongoza, muwekezaji, bosi wake au
 
Jaji Warioba alitoa ufafanuzi mzuri kuwa, 'wananchi hawataki majimbo, mkataba wala serikali mbili! Wanataka tatu'. Vyama vyote hapa vikubwa vilipoteza. Ni mbumbumbu ndo hawakuelewa

Mimi sioni contradiction yeyote kati ya kuwa na serikali TATU na kuwa na majimbo!!! Kwani tutakapokuwa na serikali Tatu mikoa haitakuwepo? Kama mikoa itakuwepo ndio hayo kwa jina lingine yanaitwa majimbo ; tofauti yake tu itakuwa hao viongozi wa hayo majimbo hawatapatikana kwa mtindo wa kupeana zawadi na kiongozi wa nchi bali wananchi watamchagua ili awe accountable kwao!!!
 
chadema wanataka kuwe na serikali tatu. Wakati huo huo wanataka kuwe serikali ya majimbo. Kwa maana hiyo, kutakuwa na rais wa muungano na wakuu wawili wa serikali za bara na zanzibar. Pia kutakuwepo na gavana katika kila jimbo ambao watakuwa na mamlaka kamili kwenye majimbo yao.

Ukiondoa suala la gharama ambalo kwa demokrasia ni vyema kuzipitia kiutawala hii imekaa sawa? Utawala wa majimbo chini ya serikali tatu unawezekana? Dhana kuu ya sera ya serikali ya majimbo ni kuhamisha madaraka ya maamuzi kutoka kwa watu wachache na kuyarejesha mikononi mwa wananchi vijijini.

Kama ni hivyo, hizo serikali mbili za bara na zanzibar zitakazokuwa zinaongozwa na wakuu wawili zitakuwa zinafanya nini? Madaraka ya wakuu wa serikali hizo mbili hayatagongana na madaraka ya magavana wa majimbo? Kama serikali moja chini ya utawala wa majimbo haiwezekani, solution ni kuwa na utawala wa majimbo chini ya serikali tatu?
kwa hali ya kawaida tu ni kuwa umekurupuka kuandikahi posti yako kwani ungejipa muda kidogotu wa kufikiri usingeandika hivi.
kwenye rasimu ya katiba mpya hawakupendekeza serikali za majimbo na badalayake wamependekeza serikali tatu, binafsi sioni sababu ya chadema kutounga mkono muundo wa serikali tatu.
 
CHADEMA wanataka kuwe na serikali tatu. Wakati huo huo wanataka kuwe serikali ya majimbo. Kwa maana hiyo, kutakuwa na Rais wa Muungano na wakuu wawili wa serikali za Bara na Zanzibar. Pia kutakuwepo na gavana katika kila jimbo ambao watakuwa na mamlaka kamili kwenye majimbo yao.

Ukiondoa suala la gharama ambalo kwa demokrasia ni vyema kuzipitia kiutawala hii imekaa sawa? Utawala wa majimbo chini ya serikali tatu unawezekana? Dhana kuu ya sera ya serikali ya majimbo ni kuhamisha madaraka ya maamuzi kutoka kwa watu wachache na kuyarejesha mikononi mwa wananchi vijijini.

Kama ni hivyo, hizo serikali mbili za Bara na Zanzibar zitakazokuwa zinaongozwa na wakuu wawili zitakuwa zinafanya nini? Madaraka ya wakuu wa serikali hizo mbili hayatagongana na madaraka ya magavana wa majimbo? Kama serikali moja chini ya utawala wa majimbo haiwezekani, solution ni kuwa na utawala wa majimbo chini ya serikali tatu?

..hata mimi sipendi serikali za majimbo.

..naamini zitaongeza gharama, na zinaweza kuathiri umoja wetu.

..baada ya kusema hayo, nadhani cha msingi ni kubainisha kwa uwazi kabisa mipaka ya serikali za majimbo, za wabia[Tgk & Znz] wa shirikisho, na serikali kuu yaani serikali ya shirikisho la Tanzania.

..unaweza kuwa na idara/wizara za elimu za majimbo halafu ukawa na wizara ya elimu ya Tanganyika na nyingine Zanzibar. serikali ya shirikisho itakuwa haishughuliki na masuala ya elimu ya nchi wabia.

..pia unaweza kuwa na wizara ya afya ktk majimbo, serikali wabia wa shirikisho, na serikali kuu. kunaweza kuwa hospitali za majimbo, hospitali za wabia wa shirikisho, halafu serikali kuu ikawa inashughulika na taasisi za utafiti wa masuala ya afya,taasisi za udhibiti wa magonjwa ya milipuko, etc etc.

..mwisho, kunaweza kuwa na maeneo ambayo serikali za majimbo na wabia wa shirikisho haziyagusi kabisa. hapa nazungumzia masuala kama majeshi ya ulinzi, wizara .za mambo ya nje, na masuala mengine ambayo yatabainishwa kikatiba.

cc Ng'wamapalala
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hapa ndio ilikuwa kiini cha swali langu.

Hata kama katiba ya sasa ikiendelea na CDM ikashika madaraka, hawawezi kuweka serikali za majimbo kwa sababu itakuwa ni kinyume cha katiba. Kama tunaamini kuwa wazo lao ni kubadili katiba - wakiwa madarakani- ili kuwapo na serikali za majimbo then katiba yoyote itakayokuwepo si wanaweza kuibadili?

Kama wazo lao ni kubadili katiba kama watashika madaraka ili kuruhusu serikali za majimbo, then katika hali ya sasa sioni kama kuna ubaya wowote strategically kwa wao kukubali serikali tatu kama wanaamini hiyo itajenga mazingira mazuri zaidi wa kuweza kuitoa CCM madarakani (na bila shaka maslahi bora zaidi kwa wananchi?). Then wakishashika madaraka, wakaaminika, pengine inaweza kuwa rahisi zaidi kwao kuwashawishi wananchi juu ya suala la serikali za majimbo na accordingly kubadilisha katiba.

Katika mchakato wa kidemokrasia ni kawaida kufuata njia/chaguo la wengi hata kama ni tofauti na chaguo lako. Tumeona hata Zanzibar (Uamsho na makundi mengine) ambayo mwanzoni walikuwa na msimamo wa muuungano wa makataba (whatever that is!) lakini baada ya kuona hilo sio suala rahisi, nao pia wame soften na sasa naona wanakubali serikali tatu (kimsingi) lakini wanataka mambo ya muungano yapunguzwe zaidi.

Lakini suala la muhimu ni haya yote pamoja na misimamo/sera zao (iwe CCM, CDM, CUF, Uamsho etc) yanafanywa kwa maslahi ya nani? Wananchi, Chama, ama Kikundi cha watu fualani tu? Hili ni tatizo kubwa sana (nimeona mdau Ng'wamapalala ameligusia hapo juu).

Kwa hiyo, wakifanukiwa kuchukua madaraka chini ya serikali tatu watareconcile vipi na sera yao ya majimbo?

How will they convince the voters kuwa utawala wa majimbo unawezekana chini ya serikali tatu?
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Rudi tena darasani!!!!!! sasa hivi kuna Mikoa hiyo ni serikali,kuna wilaya hiyo ni serikali. Utawala wa majimbo maana yake ni scope ya maeneo mfano mikoa ya morogoro,dodoma,sindida ikaunda jimbo la kati na mkuu wa jimbo ni gavana na hapa maana yake tayari umeondoa wakuu wa mikoa 3 na pia umeondoa uteusi wa wakuu wa mikoa 3 na kurudisha mamlaka kwa raia. yaani unakubali akili ndogo ikatawala akili kubwa,pole sana

Na kama mwalimu utakuwa wewe basi nitafeli.

Ulichoadika hapo ni ufafanuzi wa utawala wa majimbo lakini hujajibu swali langu la how would you reconcile serikali tatu na utawala wa majimbo?

Inaonekana wanafunzi wengi huwa wanafeli simply kwa kutojua swali.
 
Mimi sioni contradiction yeyote kati ya kuwa na serikali TATU na kuwa na majimbo!!! Kwani tutakapokuwa na serikali Tatu mikoa haitakuwepo? Kama mikoa itakuwepo ndio hayo kwa jina lingine yanaitwa majimbo ; tofauti yake tu itakuwa hao viongozi wa hayo majimbo hawatapatikana kwa mtindo wa kupeana zawadi na kiongozi wa nchi bali wananchi watamchagua ili awe accountable kwao!!!

Ndivyo hivyo Chadema imependekeza majimbo yatakavyokuwa?
 
kwa hali ya kawaida tu ni kuwa umekurupuka kuandikahi posti yako kwani ungejipa muda kidogotu wa kufikiri usingeandika hivi.
kwenye rasimu ya katiba mpya hawakupendekeza serikali za majimbo na badalayake wamependekeza serikali tatu, binafsi sioni sababu ya chadema kutounga mkono muundo wa serikali tatu.

Yaani wewe ndiyo umekurukupa bila kusoma nilichoandika.

Thread yangu haihusiani na rasimu ya katiba, bali sera za Chadema za utawala wa majimbo na serikali tatu.
 
..hata mimi sipendi serikali za majimbo.

..naamini zitaongeza gharama, na zinaweza kuathiri umoja wetu.

..baada ya kusema hayo, nadhani cha msingi ni kubainisha kwa uwazi kabisa mipaka ya serikali za majimbo, za wabia[Tgk & Znz] wa shirikisho, na serikali kuu yaani serikali ya shirikisho la Tanzania.

..unaweza kuwa na idara/wizara za elimu za majimbo halafu ukawa na wizara ya elimu ya Tanganyika na nyingine Zanzibar. serikali ya shirikisho itakuwa haishughuliki na masuala ya elimu ya nchi wabia.

..pia unaweza kuwa na wizara ya afya ktk majimbo, serikali wabia wa shirikisho, na serikali kuu. kunaweza kuwa hospitali za majimbo, hospitali za wabia wa shirikisho, halafu serikali kuu ikawa inashughulika na taasisi za utafiti wa masuala ya afya,taasisi za udhibiti wa magonjwa ya milipuko, etc etc.

..mwisho, kunaweza kuwa na maeneo ambayo serikali za majimbo na wabia wa shirikisho haziyagusi kabisa. hapa nazungumzia masuala kama majeshi ya ulinzi, wizara .za mambo ya nje, na masuala mengine ambayo yatabainishwa kikatiba.

cc Ng'wamapalala

At least wewe umenielewa nilichokuwa nahoji.
 
Kwa hiyo, wakifanukiwa kuchukua madaraka chini ya serikali tatu watareconcile vipi na sera yao ya majimbo?

How will they convince the voters kuwa utawala wa majimbo unawezekana chini ya serikali tatu?

..kuna wanaodhani kwamba mfumo wa serikali 3 hauwezekani.

..wanadai nchi haiwezi kuwa ma "maraisi" watatu.

..kama tunaweza kuwa na serikali 2, basi tunaweza kuwa na serikali 3.

..USA wana serikali za majimbo 50, juu yake kuna serikali kuu Federal Govt'.

..we can take a lesson frm them, kuona tutafanya vipi na hayo majimbo 10 yanayopendekezwa na CDM.

..kuhusu ku-convince voters hiyo inaweza kuwa kazi ngumu kutokana na viwango vya uelewa, na vitisho/udanganyifu unaofanywa na watawala.
 
CHADEMA wanataka kuwe na serikali tatu. Wakati huo huo wanataka kuwe serikali ya majimbo. Kwa maana hiyo, kutakuwa na Rais wa Muungano na wakuu wawili wa serikali za Bara na Zanzibar. Pia kutakuwepo na gavana katika kila jimbo ambao watakuwa na mamlaka kamili kwenye majimbo yao.

Ukiondoa suala la gharama ambalo kwa demokrasia ni vyema kuzipitia kiutawala hii imekaa sawa? Utawala wa majimbo chini ya serikali tatu unawezekana? Dhana kuu ya sera ya serikali ya majimbo ni kuhamisha madaraka ya maamuzi kutoka kwa watu wachache na kuyarejesha mikononi mwa wananchi vijijini.

Kama ni hivyo, hizo serikali mbili za Bara na Zanzibar zitakazokuwa zinaongozwa na wakuu wawili zitakuwa zinafanya nini? Madaraka ya wakuu wa serikali hizo mbili hayatagongana na madaraka ya magavana wa majimbo? Kama serikali moja chini ya utawala wa majimbo haiwezekani, solution ni kuwa na utawala wa majimbo chini ya serikali tatu?
Serikali za majimbo ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa letu.viongozi waliopo sasa ni wengi kuliko wale wa majimbo.mfano jimbo la kanda ya ziwa ni mikoa ya mwanza,shinyanga,mara,kagera,geita,simiyu.kutakuwa na gavana mmoja tu.hesabu ya std1 umesave kodi za wananchi badala ya kwenda marafiki wa viongozi wanaoteuliwa kwa upendeleo.pia hawa magavana watachaguliwa na wananchi badala kupewa vyeo kama zawadi au kilipa fadhila.utitiri wa wabunge wanaosema ndiyo kwa kila jambo bungeni hawatakuwepo majimbo yatapunguzwa na kufanya wilaya kuongozwa na mameya na sio wakuu wa wilaya.na hawa wote watachaguliwa na wananchi na baada ya miaka mitano watatoa hesabu kwa wananchi.kwa hesabu std 1 wabunge na mameya watakuwa wachache na wakuu wa wilaya hawatakuwepo.Faida ni kubwa kwa mfumo wa majimbo kwanza tunasave kodi zetu,pili viongozi hawa watawajibika mojakwa moja kwa wananchi.
kuhusu zanzibar kwa watu wanaotumia akili kufikiri huwezi kupata taabu.zanzibar walishavunja katiba ya muungano maana yake ni kuwa hawataki muungano.waachwe waende kwa sababu hizi ni nchi mbili zilizoungana.kwa hiyo fikiria kwanza ulichonacho na ulichonacho ni Tanganyika.
 
..hata mimi sipendi serikali za majimbo.

..naamini zitaongeza gharama, na zinaweza kuathiri umoja wetu.

..baada ya kusema hayo, nadhani cha msingi ni kubainisha kwa uwazi kabisa mipaka ya serikali za majimbo, za wabia[Tgk & Znz] wa shirikisho, na serikali kuu yaani serikali ya shirikisho la Tanzania.

..unaweza kuwa na idara/wizara za elimu za majimbo halafu ukawa na wizara ya elimu ya Tanganyika na nyingine Zanzibar. serikali ya shirikisho itakuwa haishughuliki na masuala ya elimu ya nchi wabia.

..pia unaweza kuwa na wizara ya afya ktk majimbo, serikali wabia wa shirikisho, na serikali kuu. kunaweza kuwa hospitali za majimbo, hospitali za wabia wa shirikisho, halafu serikali kuu ikawa inashughulika na taasisi za utafiti wa masuala ya afya,taasisi za udhibiti wa magonjwa ya milipuko, etc etc.

..mwisho, kunaweza kuwa na maeneo ambayo serikali za majimbo na wabia wa shirikisho haziyagusi kabisa. hapa nazungumzia masuala kama majeshi ya ulinzi, wizara .za mambo ya nje, na masuala mengine ambayo yatabainishwa kikatiba.

cc Ng'wamapalala
Mkuu JokaKuu nimekupata. Mimi sina taabu na kuwepo kwa sera yoyote ile ambayo italeta maendeleo kwa haraka lakini ninapinga kuwepo kwa sera ambayo inagawa jamii na kuondoa utaifa kutokana na historia na tamaduni tulizonazo, lakini kikubwa zaidi, siogopi mabadiliko katika jamii kwa sababu mabadiliko ni sehemu ya maendeleo.

Kuna watu wanatoa mifano mbali mbali ya utawala wa majimbo katika mataifa mbali mbali namkatika mafanikio hayo wanasema hata Tanzania tunaweza kufanikiea lakini cha kushangaza wanashindwa kubainisha kiini au chanzo cha uwepo wa hayo majimbo katika mataifa mbali mbali.

Tanzania tulishawahi kuwa na utawala wa ma-chief ambao ukiungalia sana utagundua muundo wake ulikuwa unashabihiana na utawala wa majimbo lakini kutokana na mtazamo wa Watawala wa kipindi hicho, waliona utawala kama huo haufai na ndiyo maana ukafutiliwa mbali na badala yake kukaanzishwa utawala wa mikoa ambao unatambuliwa katika katiba ya 1977, sehemu ya tatu, kipengele cha 61.

Sintofahamu yangu inakuja kwenye implementation ya haya majimbo ikichukuliwa kuwa hii ni sera ya CHADEMA na siyo matakwa ya wananchi wote. Ninasema hivi nikiwa na maana ya kutaka kufahamu kama hii sera itakuwa sheria mama ndani ya katiba ya 'Tanganyika' au itakuwa ni sheria kama sheria za kila siku zinavyotungwa bungeni kwa maana kwamba serikali ya chama kingine ikiingia madarakani inaweza kufutilia mbali sheria ya serikali za majimbo kwa urahisi kwa vile haitakuwa na sera ya majimbo katika uendeshaji wa nchi.

Ninaona hili swala linaongelewa kinadharia na kisiasa sana badala ya uharisia katika implementation ikichukuliwa kuwa maswala ya kimaendeleo na uongozi wa majimbo unatofautiana kati ya jimbo na jimbo. Hata raslimali nazo zinatofautiana kati ya jimbo na jimbo.

Naomba uniweka sawa kwa hili swala kwa sababu naona kama CHADEMA wanapiga ngoma ya kisiasa ambayo haina wachezaji wengi nchini kutokana na upya wake.
 
..kuna wanaodhani kwamba mfumo wa serikali 3 hauwezekani.

Basically, ningependa serikali tatu only kama itasaidia kuvunjika kwa muungano kwa haraka zaidi. Otherwise, serikali moja tuu kama haiwezekana basi kila mtu achukue zake. Kwa nini tunalazimishana?

Kuendelea kuwepo kwa serikali mbili means huu muungano wa sasa bado utaendelea na jinsi Watanganyika walivyo legelege kudai haki zao ndiyo itakuwa imetoka hiyo.

..wanadai nchi haiwezi kuwa ma "maraisi" watatu.

This would be the most ridiculous thing to have happened in Tanzania. Kama alivyowahi kusema Sitta litakuwa jambo la kuchekesha duniani iwapo nchi maskini kama Tanzania itakuwa na marais watatu kama muundo wa serikali tatu. Huu ni uoga wa kufanya maamuzi magumu. Badala ya kutatua tatizo tunalizungukia tuu.

..kama tunaweza kuwa na serikali 2, basi tunaweza kuwa na serikali 3.

Why not serikali moja? Maana kama tunaweza kuwa na serikali tatu basi si tunaweza pia kuwa na serikali nne?

..USA wana serikali za majimbo 50, juu yake kuna serikali kuu Federal Govt'.

..we can take a lesson frm them, kuona tutafanya vipi na hayo majimbo 10 yanayopendekezwa na CDM.

Yes, Marekani wana utawala wa majimbo lakini hawa marais wawili au watatu. In fact, hapa ndipo ilipo hoja yangu. Yaani unakuwa na marais watatu wanaongoza serikali tatu ndani ya nchi moja. Halafu hapo hapo unakuwa na uatawala wa majimbo chini ya magavana. Are you kidding me? Does that make sense to you at all?

..kuhusu ku-convince voters hiyo inaweza kuwa kazi ngumu kutokana na viwango vya uelewa, na vitisho/udanganyifu unaofanywa na watawala.

Hata kama ukitumia common sense hakuna mamtiki ya kuwa na serikali tatu na utawala wa majimbo kwa wakati mmoja. It does not make sense at all. Either serikali tatu bila utawala wa majimbo au utawala wa majimbo pekee. Otherwise, ni yale yale.
 
Serikali za majimbo ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa letu.viongozi waliopo sasa ni wengi kuliko wale wa majimbo.mfano jimbo la kanda ya ziwa ni mikoa ya mwanza,shinyanga,mara,kagera,geita,simiyu.kutakuwa na gavana mmoja tu.hesabu ya std1 umesave kodi za wananchi badala ya kwenda marafiki wa viongozi wanaoteuliwa kwa upendeleo.pia hawa magavana watachaguliwa na wananchi badala kupewa vyeo kama zawadi au kilipa fadhila.utitiri wa wabunge wanaosema ndiyo kwa kila jambo bungeni hawatakuwepo majimbo yatapunguzwa na kufanya wilaya kuongozwa na mameya na sio wakuu wa wilaya.na hawa wote watachaguliwa na wananchi na baada ya miaka mitano watatoa hesabu kwa wananchi.kwa hesabu std 1 wabunge na mameya watakuwa wachache na wakuu wa wilaya hawatakuwepo.Faida ni kubwa kwa mfumo wa majimbo kwanza tunasave kodi zetu,pili viongozi hawa watawajibika mojakwa moja kwa wananchi.
kuhusu zanzibar kwa watu wanaotumia akili kufikiri huwezi kupata taabu.zanzibar walishavunja katiba ya muungano maana yake ni kuwa hawataki muungano.waachwe waende kwa sababu hizi ni nchi mbili zilizoungana.kwa hiyo fikiria kwanza ulichonacho na ulichonacho ni Tanganyika.

Kwa hiyo ungependekeza serikali ya majimbo huku ikiwa chini ya serikali tatu? Maana kama unapendekeza serikali ya majimbo halafu hapo hapo unaunga mkono uwepo wa serikali tatu it simply means unarudi kule kule.

Muundo wa serikali tatu bado utasababisha gharama kubwa za uendeshaji na kuwa mzigo mkubwa kwa taifa.

Kama alivyohoji Sitta somewhere "Unakuwa na Rais wa Zanzibar anasafiri kwenda nje, Rais wa Jamhuri ya Muungano naye anasafiri, Rais wa Tanganyika naye anakwenda nje ya nchi, hivi huko nje si watatushangaa na kutuona kioja nchi maskini inafanya hivi?"
 
CHADEMA wanataka kuwe na serikali tatu. Wakati huo huo wanataka kuwe serikali ya majimbo. Kwa maana hiyo, kutakuwa na Rais wa Muungano na wakuu wawili wa serikali za Bara na Zanzibar. Pia kutakuwepo na gavana katika kila jimbo ambao watakuwa na mamlaka kamili kwenye majimbo yao.

Ukiondoa suala la gharama ambalo kwa demokrasia ni vyema kuzipitia kiutawala hii imekaa sawa? Utawala wa majimbo chini ya serikali tatu unawezekana? Dhana kuu ya sera ya serikali ya majimbo ni kuhamisha madaraka ya maamuzi kutoka kwa watu wachache na kuyarejesha mikononi mwa wananchi vijijini.

Kama ni hivyo, hizo serikali mbili za Bara na Zanzibar zitakazokuwa zinaongozwa na wakuu wawili zitakuwa zinafanya nini? Madaraka ya wakuu wa serikali hizo mbili hayatagongana na madaraka ya magavana wa majimbo? Kama serikali moja chini ya utawala wa majimbo haiwezekani, solution ni kuwa na utawala wa majimbo chini ya serikali tatu?
Wakuu wa mikoa na wilaya leo wanafanya kazi gani wakati kuna serikali mbili? Hongera umeongeza idadi ya posti zako na likes.
 
Ni sawa na na mimi kukuuliza kama kutakuwa na utawala wa majimbo, then serikali za bara na Zanzibar zitakuwa zinafanya nini? Huoni kuwa kwa kuwepo kwa serikali ya majimbo na serikali tatu, bado utaendelea kuuliza swali ulilouliza?

Bado naendelea kusema kuwa nchi inahitaji kuwa na serikali na Tanganyika ni sawa na Zanzibar, Zanzibar imekuwa na serikali yake kwa kipindi cha miaka 50 na kuanza kuuliza sasa inafanya kazi gani sifikiri kuwa pana haja ya kufanya hivyo, pengine sisi Wazanzibari ndio tunajuwa nini inafanya. Utawala wa majimbo ni mfumo wa kiutawala ambao nchi unaigawa katika mipaka ya kijografia kiutawala. Kila nchi inakuwa na utaratibu wa kugawa mipaka ya utawala na kuna mifano mingi ambayo unaweza kukuta miji mikubwa zaidi ya mitatu au minne ikiwa kama jimbo moja chini ya kiongozi mmoja ambapo kunakuwa na kiongozi kila mji. Tatizo linakuwa pale unapochukulia majimbo kuwa sawa na majimbo ya nchi nyengine (mfano Marekani) ambapo haya majimbo ndio msingi wa muungano wa nchi.

That was not my point. Sisemi kuwa iwepo serikali ya Zanzibar, isiwepo serikali ya Tanganyika, lakini iwepo serikali ya majimbo.

Kwanini iwepo serikali ya majimbo wakati vilivyoungana sio majimbo bali ni nchi? Hata jina lenyewe la Tanzania lina lengo hilo la kuonyesha muungano wa nchi mbili, sasa nchi inakuwaje jimbo? Muungano ni mkataba ambao kuwepo kwake si lazima iwapo wahusika wataona hakuna haja lakini Tanganyika na Zanzibar zipo na hakuna njia ya kuzziondowa na ili ziongozwe basi zinahitaji serikali

Na serikali ya jimbo itakuwa inafanya nini? The way ulivyoeleza ni kama vile unataka kuendeleza tawawa za mikoa za sasa kupitia back door ya utawala wa majimbo.

Kwani kuna kosa gani kuwepo kwa Mikowa na kuunganisha mikowa fulani kuwa kwenye mfumo wa majimbo. Nilichoelewa mimi ni kuwa CDM wanahisi kuunganisha mikowa kuwa kwenye majimbo kutasaidia kuharakisha maendeleo ya Taifa. Hili la kusema kuwa ni gharama mimi sioni hivyo kwani sasa hivi si tuna wabunge wa wilaya, tuna wakuu wa mikoowa, tuna wakuu wa wilaya, tuna serikali za vijiji na kule Zanzibar wana serikali za majimbo na ngazi zote hizi zinatumia gharama.
 
umeuliza maswali ya msingi sana kwenye hoja yako hii EMT. lakini kwanza hebu tujaribu kutafakari kwa undani ni kitu gani ambacho wanachi wanataka wka sasa??

wananchi wanataka serikali 3 wao hawataki moja wala mbili wala serikali za majimbo, kama ndivyo wananchi wanavyotaka ni wazi kwamba matakwa yao ndio yatimie.

lakini kwa upande mwngine CDM walilenga gavana wa jimbo ndiye atakaye mreplace mbunge by so doing wabunge wapewe meno ya kuwawajaibisha watendaji wa serikali. to me hii ilikuwa inaniwia ngumu sana sana kuipatia picha itakavyokaa manake niliwaza kiutendaji wabunge wetu kwanza sio wachapa kazi ni watu wa maneno mengi pasipo utekelezaji na hapo hapo pia wabunge wetu zaid ya kujineemesha kwa kutaka maposho makubwa hawana jingine wanalo tusaidia sisi kama wananchi sasa leo hii wakipewa hayo mamlaka ya kiutedaji si ndio watatumaliza??

Hata wewe hujui unachokisema! Gavana ni kitu tofauti na mbunge au senetor wewe unachanganya mambo, gavana ni cheo cha utawala na mbunge au senetor ni vyeo vya uwakilishi.

Kimsingi kimuundo majimbo na mikoa au wilaya hamna tofauti. Kinacholeta tofauti ni kuwa chadema wanapendekeza muundo wa kuwajibika wa wananchi zaidi kuliko kuwajibika kwa Raisi kama ilivyo sasa kwa wakuu wa wilaya na mikoa na wakurungenzi. Kwenye muundo wa majimbo wasimamizi wa watendaji wote wananchaguliwa yaani gavana na mayor ambaye anakuwa badala ya mkuu wa wilaya na gavana badala ya mkuu wa mkoa wakurugenzi badala ya kuteuliwa na raisi hawa wanakuwa ni technical oficers watakaoajiriwa na ofice ya mayor chini ya halmashauri. Wabunge watendelea kuwepo kama ilivyo sasa na wataendelea na kazi zao kama ilivyo sasa ya kutunga sheria na kupitisha bajeti ya serikali kuu. Majimbo yatapata ruzuku toka serikari kuu kama ilivyo sasa kwa halmashauri.

Kimsingi siyo kwamba watanzania hawataki majimbo ila kwamba ni wachache wanaoelewa huu muundo maana wengi wanadanganywa na propaganda za ccm kuwa itakuwa gharama kubwa wakati kimuundo hakuna ongozeko lolote la watendaji ukilinganisha na muundo wa sasa ambao kuna watu kama wakuu wa mikoa na wilaya wamebaki na kazi moja tu ya umwenyekiti wa ulinzi na usalama basi zaidi ya hapo ni porojo tu. Mambo mengi yanafanyika kwenye halmashauri kiasi kwamba hawa wakuu hawana kazi huko zaidi ya kufukuzana na wakurugenzi kutaka wakatie kidogo maana pesa yote iko kwa wakurugenzi!

Kimsingi muundo wa majimbo haujarishi serikari tatu,mbili au moja maana kimuundo hamna tofauti na uliopo sasa ambao soidhani kama utabadilika hata kama tukiwa na serikali tatu au moja. Wazo la kubadilisha kutoka kuwajibika kwa Raisi na kuwajibika moja kwa moja kwa wananchi ndiyo inayoupa muundo wa majimbo kuwa mzuri ukilinaganisha na huu wa sasa ambao umekaa kikoloni zaidi. Ukiangalia hata sasa wakuu wa mkoa na wilaya hawana mahusiano mazuri na wananchi na wananchi huwa wanawaogopa maana wamekaa kidoladola tu muda wote vitishotisho tu kwa wananchi!

Nadhani hii itasaidi kuweka mambo sawa juu ya huu muundo!
 
Last edited by a moderator:
Wewe ni msemaji wa CHADEMA au unataka kuchafua hali ya hewa ndani ya CHAMA? mimi naamini wamejikanyaga,
endelea kuamini hivyo na usilazimishe na wenzio tuamini unayoamini! Bencho......
 
how would you reconcile serikali tatu na utawala wa majimbo?

Serikali kuu ya muungano itasimamia mambo yote ya muungano kama katiba ilivyoainisha. Wakati serikali za washirika wa muungano zitaongozwa kwa kufuata mfumo wa majimbo.

Utekelezaji wa sera ya serikali za majimbo utakua na urahisi kama kutakuwa na serikali moja lakini wananchi walikataa serikali moja.
 
Back
Top Bottom