CHADEMA, serikali tatu na serikali ya majimbo

CHADEMA, serikali tatu na serikali ya majimbo

Basically, ningependa serikali tatu only kama itasaidia kuvunjika kwa muungano kwa haraka zaidi. Otherwise, serikali moja tuu kama haiwezekana basi kila mtu achukue zake. Kwa nini tunalazimishana?

Kuendelea kuwepo kwa serikali mbili means huu muungano wa sasa bado utaendelea na jinsi Watanganyika walivyo legelege kudai haki zao ndiyo itakuwa imetoka hiyo.

This would be the most ridiculous thing to have happened in Tanzania. Kama alivyowahi kusema Sitta litakuwa jambo la kuchekesha duniani iwapo nchi maskini kama Tanzania itakuwa na marais watatu kama muundo wa serikali tatu. Huu ni uoga wa kufanya maamuzi magumu. Badala ya kutatua tatizo tunalizungukia tuu.

Why not serikali moja? Maana kama tunaweza kuwa na serikali tatu basi si tunaweza pia kuwa na serikali nne?

Yes, Marekani wana utawala wa majimbo lakini hawa marais wawili au watatu. In fact, hapa ndipo ilipo hoja yangu. Yaani unakuwa na marais watatu wanaongoza serikali tatu ndani ya nchi moja. Halafu hapo hapo unakuwa na uatawala wa majimbo chini ya magavana. Are you kidding me? Does that make sense to you at all?

Hata kama ukitumia common sense hakuna mamtiki ya kuwa na serikali tatu na utawala wa majimbo kwa wakati mmoja. It does not make sense at all. Either serikali tatu bila utawala wa majimbo au utawala wa majimbo pekee. Otherwise, ni yale yale.

..I had to go back and read what I wrote.

..hoja kwamba serikali 3 maana yake ni maraisi watatu ni upotoshaji.

..ninavyoelewa ni kwamba kutakuwa na mipaka ya madaraka baina ya serikali za nchi washiriki na serikali kuu.

..kwa msingi huo basi hata hao maraisi watakuwa hawalingani kimadaraka wala kimajukumu.
 
Kwa hiyo, wakifanukiwa kuchukua madaraka chini ya serikali tatu watareconcile vipi na sera yao ya majimbo?

How will they convince the voters kuwa utawala wa majimbo unawezekana chini ya serikali tatu?
Kulikuwa na hoja hapa pia hata hizo serikali tatu kwa namna zinavyopendekezwa conceptually inaweza kuwa ni kutekeleza sera ya majimbo (ingawa pengine CDM wanakusudia kuwa na majimbo zaidi ya mawili yanayopendekezwa!) na pengine hiyo ni sababu mojawapo CCM wamekuwa "nervous" juu ya pendekezo la serikali tatu.

Kama wakiona serikali tatu (kuu, na za majimbo mawili) hazitoshi, si "wanabadili" katiba (kwa maslahi ya wananchi wote?) kwa kugawanya "jimbo" la Tanganyika kupata majimbo say matano na hivyo kufanya shirikisho kuwa na majimbo sita. Hapa pengine ndio linakuja suala la kuwashawishi voters/wananchi ili wakubali kubadili katiba ili "kuongeza" idadi ya majimbo (kugawanya jimbo la Tanganyika).
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Wakuu wa mikoa na wilaya leo wanafanya kazi gani wakati kuna serikali mbili? Hongera umeongeza idadi ya posti zako na likes.

Kwa hiyo ukiondoa wakuu wa mikoa na wilaya halafu ukaweka magavana na hapo hapo ukaweka serikali tatu chini ya marais watatu wooote hao watakuwa wanafanya nini?
 
Kwani kuna kosa gani kuwepo kwa Mikowa na kuunganisha mikowa fulani kuwa kwenye mfumo wa majimbo. Nilichoelewa mimi ni kuwa CDM wanahisi kuunganisha mikowa kuwa kwenye majimbo kutasaidia kuharakisha maendeleo ya Taifa. Hili la kusema kuwa ni gharama mimi sioni hivyo kwani sasa hivi si tuna wabunge wa wilaya, tuna wakuu wa mikoowa, tuna wakuu wa wilaya, tuna serikali za vijiji na kule Zanzibar wana serikali za majimbo na ngazi zote hizi zinatumia gharama.

Umeelwa ninachohoji au unapindisha makusudi? Nasema hivi? Kuna mantiki gani kuwa na sera ya majimbo na pia kuunga mkono uwepo wa serikali tatu? How would you reconcile these?

Sikatai uwepo wa utawala wa majimbo, bali kuwepo kwa utawala huo chini ya serikali tatu.
 
Kimsingi muundo wa majimbo haujarishi serikari tatu,mbili au moja maana kimuundo hamna tofauti na uliopo sasa ambao soidhani kama utabadilika hata kama tukiwa na serikali tatu au moja.

So, what is the point ya kuwa na utawala wa majimbo kama kimmundo hautakuwa tofauti na huu uliopo sasa?
 
Serikali kuu ya muungano itasimamia mambo yote ya muungano kama katiba ilivyoainisha. Wakati serikali za washirika wa muungano zitaongozwa kwa kufuata mfumo wa majimbo.

Utekelezaji wa sera ya serikali za majimbo utakua na urahisi kama kutakuwa na serikali moja lakini wananchi walikataa serikali moja.

Fafanua hapo kwenye red. Una maana gani kusema kuwa serikali za washirika wa muungano zitaongozwa kwa kufuata mfumo wa majimbo? How?
 
..hoja kwamba serikali 3 maana yake ni maraisi watatu ni upotoshaji.

Kwani rasimi imependekeza kuwa na marais wangapi?

..ninavyoelewa ni kwamba kutakuwa na mipaka ya madaraka baina ya serikali za nchi washiriki na serikali kuu.

Na mipaka ya hao marais na magavana wa majimbo utakuwaje?

..kwa msingi huo basi hata hao maraisi watakuwa hawalingani kimadaraka wala kimajukumu.

Kimamtiki bado sioni maana ya uwepo wa marais watatu na utawala wa majimbo.

Sana sana hao marais washirika wataishia kuwa ceremonial kama alivyo makamu wa rais sasa.

Kwa sababu unapoongelea utawala wa majimbo it means that karibu shughuli zote zinazofanywa na serikali kuu sasa sitahamishwa majimboni na zilizosalia zingehamishwa kwa rais wa muungano na hivyo kuwafanya marais shirikishi redundant or merely ceremonial.
 
Kulikuwa na hoja hapa pia hata hizo serikali tatu kwa namna zinavyopendekezwa conceptually inaweza kuwa ni kutekeleza sera ya majimbo (ingawa pengine CDM wanakusudia kuwa na majimbo zaidi ya mawili yanayopendekezwa!) na pengine hiyo ni sababu mojawapo CCM wamekuwa "nervous" juu ya pendekezo la serikali tatu.

Kama wakiona serikali tatu (kuu, na za majimbo mawili) hazitoshi, si "wanabadili" katiba (kwa maslahi ya wananchi wote?) kwa kugawanya "jimbo" la Tanganyika kupata majimbo say matano na hivyo kufanya shirikisho kuwa na majimbo sita. Hapa pengine ndio linakuja suala la kuwashawishi voters/wananchi ili wakubali kubadili katiba ili "kuongeza" idadi ya majimbo (kugawanya jimbo la Tanganyika).

I see. Kwa hiyo, inawezekana tume ya Warioba imependekeza utawala wa majimbo mawili indirectly bila hata wao kufahamu.

Ningependa kusikia Chadema wakifafanua jinsi sera yao ya utawala wa majimbo ambayo wanaitumia kwenye chama inavyo-fit kwenye serikali tatu.

But on conceptual basis, kama wataona "majimbo mawili ya Tanhanyika na Zanzibar" hayatoshi watagawa "jimbo la Tanganyika" katika majimbo mengine au pia watafanya hivyo hivyo kwa "jimbo lka Zanzibar"?
 
  • Thanks
Reactions: SMU
.. pia watafanya hivyo hivyo kwa "jimbo lka Zanzibar"?
Naamini Zanzibar inatosha kufanya jimbo moja tu. Ikiwa lazima sana labda kuwe na "jimbo la unguja" na "jimbo la pemba"
 
umeuliza maswali ya msingi sana kwenye hoja yako hii EMT. lakini kwanza hebu tujaribu kutafakari kwa undani ni kitu gani ambacho wanachi wanataka wka sasa??

wananchi wanataka serikali 3 wao hawataki moja wala mbili wala serikali za majimbo, kama ndivyo wananchi wanavyotaka ni wazi kwamba matakwa yao ndio yatimie.

lakini kwa upande mwngine CDM walilenga gavana wa jimbo ndiye atakaye mreplace mbunge by so doing wabunge wapewe meno ya kuwawajaibisha watendaji wa serikali. to me hii ilikuwa inaniwia ngumu sana sana kuipatia picha itakavyokaa manake niliwaza kiutendaji wabunge wetu kwanza sio wachapa kazi ni watu wa maneno mengi pasipo utekelezaji na hapo hapo pia wabunge wetu zaid ya kujineemesha kwa kutaka maposho makubwa hawana jingine wanalo tusaidia sisi kama wananchi sasa leo hii wakipewa hayo mamlaka ya kiutedaji si ndio watatumaliza??

gfsonwin,
hapo kwenye red! sii wananchi bali wana siasa, wananchi wanataka elimu bora kwa watoto wao, hospital zenye dawa na vitanda vya kutosha kwa waja wazito, maji safi, barabara za kupitika muda woote hayo ya serikali moja, mbili tatu, ...., kumi hayahusu kabisa! kama unabisha muulize jirani yako! ila wanasiasa wanatafuta kila mbinu wajulikane wapo!
 
Muungano ukiwepo rais ni mmoja tu wengine ni watakuwa makamu wa rais .kila nchi itakuwa na utaratibu wake wa kuendesha nchi yake,kasoro yale tu muungano ni rais .tatizo liko wapi,nimekueleza kuwa madc hawatakuwepo tutakuwa mameya na wabunge wachache.gharamu zipi? Madc ma mrc hawatakuwepo.isipokuwa magavana wasiozidi kumi tu.balaza la mawaziri lisilozidi wwatu 20.gharama iko wapi ndugu ukilinganisha na sasa.
 
umeuliza maswali ya msingi sana kwenye hoja yako hii EMT. lakini kwanza hebu tujaribu kutafakari kwa undani ni kitu gani ambacho wanachi wanataka wka sasa??

wananchi wanataka serikali 3 wao hawataki moja wala mbili wala serikali za majimbo, kama ndivyo wananchi wanavyotaka ni wazi kwamba matakwa yao ndio yatimie.

lakini kwa upande mwngine CDM walilenga gavana wa jimbo ndiye atakaye mreplace mbunge by so doing wabunge wapewe meno ya kuwawajaibisha watendaji wa serikali. to me hii ilikuwa inaniwia ngumu sana sana kuipatia picha itakavyokaa manake niliwaza kiutendaji wabunge wetu kwanza sio wachapa kazi ni watu wa maneno mengi pasipo utekelezaji na hapo hapo pia wabunge wetu zaid ya kujineemesha kwa kutaka maposho makubwa hawana jingine wanalo tusaidia sisi kama wananchi sasa leo hii wakipewa hayo mamlaka ya kiutedaji si ndio watatumaliza??

Ila kama wewe ni mrembo kama iyo picha uliyobandika hapo, Naomba nikuulize, Je! umeshaolewa?
 
Kwani rasimi imependekeza kuwa na marais wangapi?

Na mipaka ya hao marais na magavana wa majimbo utakuwaje?

Kimamtiki bado sioni maana ya uwepo wa marais watatu na utawala wa majimbo.

Sana sana hao marais washirika wataishia kuwa ceremonial kama alivyo makamu wa rais sasa.

Kwa sababu unapoongelea utawala wa majimbo it means that karibu shughuli zote zinazofanywa na serikali kuu sasa sitahamishwa majimboni na zilizosalia zingehamishwa kwa rais wa muungano na hivyo kuwafanya marais shirikishi redundant or merely ceremonial.
EMT,

..Tanzania itakuwa na Raisi mmoja kama ilivyo sasa.

..kitakachobadilika ni upande wa Tanganyika[Tanzania Bara] kuwa na serikali na Raisi kama ilivyo kwa ndugu zetu wa Zanzibar.

..mipaka ya madaraka ya Raisi wa Tanganyika au Zanzibar na magavana wa majimbo itategemea na mambo gani itaamuliwa yashughulikiwe ktk level ya majimbo, na mambo gani yashughulikiwe ktk level ya nchi washirika.

..katika yale mambo ambayo hayatakuwa ya shirikisho, kuna mengine ambayo yatashughulikiwa na magavana, na mengine yatashughulikiwa na maraisi wa nchi washirika.

..u have to reserve u judgement at least for now on whether maraisi shirikishi watakuwa ceremonial or not kwasababu bado hatujajua nini kitakuwepo kwenye portfolio ya magavana wa majimbo. actually kuna wanaosema tofauti na wewe kwamba Raisi wa muungano/shirikisho ktk mfumo wa serikali 3 atakuwa ceremonial tu.
 
Last edited by a moderator:
Fafanua hapo kwenye red. Una maana gani kusema kuwa serikali za washirika wa muungano zitaongozwa kwa kufuata mfumo wa majimbo? How?

Kwa mfano Watanganyika wanaweza wakamua kuwa na majimbo sita. Kila jimbo litashughulikia mambo yasiyo ya Muungano katika maeneo yao shughuli za serikali za majimbo zitaratibiwa na serikali ya upande wa Tanganyika na hivyo hivyo kwa upande wa Zanzibar.
 
Kwa hiyo ukiondoa wakuu wa mikoa na wilaya halafu ukaweka magavana na hapo hapo ukaweka serikali tatu chini ya marais watatu wooote hao watakuwa wanafanya nini?
Jiulize swali moja tu.. Leo tuna serikali 2, wakuu wa mikoa na wilaya wanafanya kazi gani?... ukisha pata majibu ndipo tunaweza kwenda mbele..
 
Kwa hiyo ukiondoa wakuu wa mikoa na wilaya halafu ukaweka magavana na hapo hapo ukaweka serikali tatu chini ya marais watatu wooote hao watakuwa wanafanya nini?

mkuu we ni slow learner, kama utasema majimbo ina maana tutakuwa na magavana wa kuchaguliwa kama kumi, (toa maRC maDC yote). Ukisema serikali tatu majimbo hayapo wewe. Chini ya majimbo hata vurugu za Unguja na Pemba zingeisha, si Zanzibar tu!
 
Umeelwa ninachohoji au unapindisha makusudi? Nasema hivi? Kuna mantiki gani kuwa na sera ya majimbo na pia kuunga mkono uwepo wa serikali tatu? How would you reconcile these?

Sikatai uwepo wa utawala wa majimbo, bali kuwepo kwa utawala huo chini ya serikali tatu.

sera ya majimbo Warioba na watanzania waliikataa (nadhani kwa kutoelewa tu)! CHADEMA wakakubaliana na serikali tatu. Lakini, still it can excel well under serikali tatu! Tanganyika tutakomaa nayo. Tunasubiri katiba yetu
 
Umeelwa ninachohoji au unapindisha makusudi? Nasema hivi? Kuna mantiki gani kuwa na sera ya majimbo na pia kuunga mkono uwepo wa serikali tatu? How would you reconcile these?

Sikatai uwepo wa utawala wa majimbo, bali kuwepo kwa utawala huo chini ya serikali tatu.

Inawezekana wewe hutaki kunielewa lakini nitakujibu kwa ufupi
Wanataka serikali tatu kwa vile hatukuamuwa kuuwa nchi zetu, Zanzibar ipo na Tanganyika iwepo ili serikali ya tatu uwe ya muungano wa pande hizo mbili
2. Wanataka sera ya majimbo kama ni mbadala wa sera ya CCM ya mikowa (sijui kama unaelewa kuwa msingi wake ni sera ya madaraka mikoani)
Sasa huo umpindo unaoueleza unatoka wapi?
 
sababu za chadema kutaka serikali tatu ni kutokana na ukweli kwamba serikali moja kwa tz si rahisi maana haikubaliki visiwani. pia serkali mbili ni kitu kisichoeleweka hasa na watu wa Bara. kwa hiyo kinachobakia ni serikali tatu. pili serikali za majimbo ni hatua ya kuondoa ukiritmba na kuharakisha maendeleo hasa waliangalia nchi zenye mfumo huu ambazo zimeharakisha maendeleo yao kama USA, Nigeria na hapa karibu Kenya. hili ni suala la mjadala na mwisho litaamuliwa na watanzania. kinachotakiwa si kusema kijumlajumla kuwa serikali za majimbo ni mbaya au ni nzuri bali ni kuchabua kwa undani faida na hasara na hatimae watu watachuja wenyewe
 
Ndivyo hivyo Chadema imependekeza majimbo yatakavyokuwa?

If anything Chadema watapunguza huo utitili wa mikoa ili iwe michache kuwapunguzia mzigo wa gharama za uendeshaji wananchi!!!
 
Back
Top Bottom