chadema ni janga la taifa. ni wanafki kupita kiasi hawa jamaa na maneno yao huwa ya blaa blaa sana.
Jenga hoja acha ushabiki wa kijinga.
chadema ni janga la taifa. ni wanafki kupita kiasi hawa jamaa na maneno yao huwa ya blaa blaa sana.
EMT kwa kuanzia napenda kukuuliza Serikali ya Zanzibar sasa inafanya nini?
Halafu nigekuuliza tena ulioona wapi nchi ikawa haina serikali? Yaani Tanganyika iwe ni nchi pekee katika uso wa dunia ambayo haina haja ya kuwa na serikali?
Muungano wa Tanzania ni muungano wa nchi mbili na hivyo inawajibika kila upande uwe na serikali yake iwapo makubaliano sio kufanya muungano wa nchi moja kama ulivyo wetu wa Tanzania.
Usawa uko wapi kama nchi moja inakuwa na serikali yake, usawa uko wapi ikiwa wananchi wa upande mmoja wanajihudumia kupitia serikali yao, huku upande mmoja unaongozwa na mchanganyiko wa pande mbili na wananchi wake wakitumia pato la jumla la pande mbili?
Inawezekana mtu alie nje ya taifa hili asifahamu huo mchakachuo uliopo na akashangaa huu ni mseto wa namna gani. Kuondowa mtafaruku huu ndio kunapohitajika kuwa na serikali ya Tanganyika.
Sasa nikujibu Serikali ya Tanganyika itakuwa inafanya nini. Serikali ya Tanganyika itakuwa inashughulikia mambo ya kiutawala wa Tanganyika na itakuwa haiingiliwi katika mamdo ya Watanganyika kama vile inavyofanyika kule zanzibar. Tanganyika itaamuwa iwe na wabunge wangapi na si lazima iwe wabunge wawe wengi kama sasa eti kila wilaya kuwa na mbunge. Pengine hayo majimbo yatatowa wabunge kwa bunge la Tanganyika. Kuulizia mfumo na gharama ni jambo la kipuuzi kwani tangu tulikpopata uhuru tumekuwa na mfumo mmoja? Mfumo wa utawala ni kitu cha kupangwa kulingana na mazingira na matakwa.
CHADEMA wanataka kuwe na serikali tatu. Wakati huo huo wanataka kuwe serikali ya majimbo. Kwa maana hiyo, kutakuwa na Rais wa Muungano na wakuu wawili wa serikali za Bara na Zanzibar. Pia kutakuwepo na gavana katika kila jimbo ambao watakuwa na mamlaka kamili kwenye majimbo yao.
Ukiondoa suala la gharama ambalo kwa demokrasia ni vyema kuzipitia kiutawala hii imekaa sawa? Utawala wa majimbo chini ya serikali tatu unawezekana? Dhana kuu ya sera ya serikali ya majimbo ni kuhamisha madaraka ya maamuzi kutoka kwa watu wachache na kuyarejesha mikononi mwa wananchi vijijini.
Kama ni hivyo, hizo serikali mbili za Bara na Zanzibar zitakazokuwa zinaongozwa na wakuu wawili zitakuwa zinafanya nini? Madaraka ya wakuu wa serikali hizo mbili hayatagongana na madaraka ya magavana wa majimbo? Kama serikali moja chini ya utawala wa majimbo haiwezekani, solution ni kuwa na utawala wa majimbo chini ya serikali tatu?
asanteChadema ni chama cha mashetani mkuu.
Kiwi, ameeleza vizuri sana.lakini kwa Tanzanian ni shida kuelewa. Chadema walipaswa kutekeleza mfumo huu kwenye sehemu ambazo wanaongoza council ili kutoa picha jinsi ambavyo wananchi wanavyoshiriki ktk kutoa maamuzi juu ya maendeleo yao ili uwe mfano,
Hivi kwa akili zako hujui kwamba kinachojadiliwa sasa ni rasimu ya katiba, na kwamba rasimu hii ilishakataa suala la majimbo (hivyo suala hili si sehemu ya mjadala wala hitaji la Chadema?)
Hoja ya CHADEMA kuhusu serikali za majimbo itakuwa na maana zaidi katika kupambana na hoja za muundo wa serikali uliopo kwa sasa, lakini inakuwa ni kaput katika kupambana na hoja za serikali tatu ambazo zimependekezwa CHADEMA, vile vile na tume ya Jaji Warioba.
EMT , labda tuanzie hapa: Hivi hata kwa katiba ya sasa CDM wangewezaje kutekeleza sera yao ya majimbo?
Shida ni kwamba pamoja na wananchi kukataa mfumo wa majimbo kama ulivyosema wewe mwenyewe, bado Chadema inatumia mfumo uliokataliwa na wananchi. Maana huwezi kuweka jambo pending wakati huo huo unalitekeleza.
Kama mfumo wa serikali tatu ndiyo ulikubaliwa basi Chadema waachane na utekelezaji wa sera yao ya majimbo.
Alichofanya Kiwi ni kujaribu kueleza dhana ya utawala wa majimbo na faida zake dhidi ya tawala za mikoa.
Ambacho hakugusia ni mahusiano kati utawala wa majimbo na serikali tatu zilizopendekezwa na kuungwa mkono na Chadema.
Nchi moja inakuwa na serikali kuu ikiongozwa na Rais na labda makamu wa rais.
Nchi hiyo inakuwa pia na serikali nyingine mbili zikiongozwa na Marais, au mawaziri wakuu or whaterver name you would like to call them.
Nchi hiyo pia inakuwa na utawala wa majimbo chini ya magavana.
How would you reconcile all these political administrations?
Na serikali ifunge office zote bara na visiwani kisa mswada unataka serikali 3?? Uvivu wa kufikiri ndio huu.. Basi.
Hata hivyo mimi binafsi nilimsikiliza zitto akifafanua kuhusu msimamo wa cdm ndani ya hoja hii ya idadi ya muundo wa serikali, nilihisi msimamo wa chama cha cdm ni serikali moja na sio tatu ama mbili.. labda msikilizeni wenyewe hapa. https://www.youtube.com/watch?v=JbV1eC_ztuw&feature=youtube_gdata_player
Still, how would you reconcile serikali kuu ya Mungano, serikali ya Tanganyika na serikali za majimbo?
upo sahihi mkuu, Top-Down leadership methodology ime-prove failure kwa changamoto za dunia ya leo, naikubali sera ya Majimbo na dhana nzima ya uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi iliyomo ndani ya sera hii.Laiti tungekuwa na serikali za majimbo serikali kuu isingewaburuza watendaji kutii amri kutoka juu. .
Kwa watu wanaoiangalia CHADEMA wakiwa nje ya jiko lake wanaona mapungufu mengi tu kuhusiana na utendaji wake. Mapungufu hayo inakuwa ni vigumu sana kuyaona walio ndani ya jiko na hata kama wakiyaona, inakuwa ni vigumu sana kuyatafutia majibu iwapo yanawagusa wafanya maamuzi katika hali hasi.Hapo ndipo ilipo hoja yangu. Kama moja ya misingi ya sera ya Chadema ya utawala wa majimbo ni kushusha na kugawanya madaraka, kuwa na muundo mpya unaosaidia utekelezaji wa majukumu na kupunguza ukubwa na gharama za uendeshaji wa serikali, basi hii inaweza isifanikiwa kama tutakuwa na siyo tuu na serikali mbili kama ilivyo sasa, bali serikali tatu.
Itategemea. Ikipita rasmi serikali tatu hata Zanzbar itabidi kurekebisha Katiba yao!!Kwa hiyo serikali ya majimbo itakuwa Bara tuu na siyo Zanzibar?
Mkuu hapa ndio ilikuwa kiini cha swali langu...Plan ni kwamba kama Chadema ikiingia madarakani basi itaanzisha utawala wa majimbo..
CHADEMA wanataka kuwe na serikali tatu. Wakati huo huo wanataka kuwe serikali ya majimbo. Kwa maana hiyo, kutakuwa na Rais wa Muungano na wakuu wawili wa serikali za Bara na Zanzibar. Pia kutakuwepo na gavana katika kila jimbo ambao watakuwa na mamlaka kamili kwenye majimbo yao.
Ukiondoa suala la gharama ambalo kwa demokrasia ni vyema kuzipitia kiutawala hii imekaa sawa? Utawala wa majimbo chini ya serikali tatu unawezekana? Dhana kuu ya sera ya serikali ya majimbo ni kuhamisha madaraka ya maamuzi kutoka kwa watu wachache na kuyarejesha mikononi mwa wananchi vijijini.
Kama ni hivyo, hizo serikali mbili za Bara na Zanzibar zitakazokuwa zinaongozwa na wakuu wawili zitakuwa zinafanya nini? Madaraka ya wakuu wa serikali hizo mbili hayatagongana na madaraka ya magavana wa majimbo? Kama serikali moja chini ya utawala wa majimbo haiwezekani, solution ni kuwa na utawala wa majimbo chini ya serikali tatu?