CHADEMA, serikali tatu na serikali ya majimbo

CHADEMA, serikali tatu na serikali ya majimbo

Jiulize swali moja tu.. Leo tuna serikali 2, wakuu wa mikoa na wilaya wanafanya kazi gani?... ukisha pata majibu ndipo tunaweza kwenda mbele..

Kwa hiyo, the best option ambayo Chadema imekuja nayo ni ku-replace hao wakuu na mikoa na wilaya with serikali tatu zilizo chini ya marais watatu na utawala wa majimbo?
 
mkuu we ni slow learner, kama utasema majimbo ina maana tutakuwa na magavana wa kuchaguliwa kama kumi, (toa maRC maDC yote). Ukisema serikali tatu majimbo hayapo wewe. Chini ya majimbo hata vurugu za Unguja na Pemba zingeisha, si Zanzibar tu!

I better be a slow learner that a fast learner bi ku-grasp chochote.

Kama "ukisema serikali tatu majimbo hayapo" kwa hiyo basi sera ya Chadema ya utawala wa majimbo haipo tena baada ya chama hicho kuunga mkono pendekezo la serikali tatu?
 
EMT,

..Tanzania itakuwa na Raisi mmoja kama ilivyo sasa.

..kitakachobadilika ni upande wa Tanganyika[Tanzania Bara] kuwa na serikali na Raisi kama ilivyo kwa ndugu zetu wa Zanzibar.

..mipaka ya madaraka ya Raisi wa Tanganyika au Zanzibar na magavana wa majimbo itategemea na mambo gani itaamuliwa yashughulikiwe ktk level ya majimbo, na mambo gani yashughulikiwe ktk level ya nchi washirika.

..katika yale mambo ambayo hayatakuwa ya shirikisho, kuna mengine ambayo yatashughulikiwa na magavana, na mengine yatashughulikiwa na maraisi wa nchi washirika.

..u have to reserve u judgement at least for now on whether maraisi shirikishi watakuwa ceremonial or not kwasababu bado hatujajua nini kitakuwepo kwenye portfolio ya magavana wa majimbo. actually kuna wanaosema tofauti na wewe kwamba Raisi wa muungano/shirikisho ktk mfumo wa serikali 3 atakuwa ceremonial tu.

What if niki-reserve my judgment na baadae kukuta kuwa actually hao marais shirikishi ni ceremonial kutokana na uwepo wa utawala wa majimbo?

Why wait now badala ya ku-make sure sasa kuwa kutakuwa hakuna tatizo la kuwepo kwa marais watatu na utawala wa majimbo?
 
..wakati mwingine unajenga hoja kama vile uko sure kwamba maraisi shirikishi watakuwa ceremonial.

..wakati mwingine unajenga hoja kama huna uhakika huo, na hoja zako zinaashiria kwamba unaamini Raisi wa shirikisho atakuwa hana tofauti na maraisi shirikisho--hoja ya "maraisi watatu."

..now, let go with ur line of thinking kwamba maraisi shirikisho watakuwa ceremonial. unashauri nini kifanyike kurekebisha tatizo hilo, wakati huo huo tuki-retain mfumo wa majimbo??

NB:

..Kenya, Mozambique, Ghana, DRC, wana mfumo wa majimbo. Tunaweza kuchukua mazuri toka huko na kuachana na mabaya ya mifumo hiyo.

cc Nguruvi3, Mwita Maranya, Zitto, Kitila Mkumbo, Edwin Mtei, Mchambuzi
 
Last edited by a moderator:
Ukisoma rasimu iliyopo uwepo wa Tanganyika kama ilivyo znz hauwezi kutoa kiongozi ceremonial.
Shirikisho lina mambo 7 kati ya 20+ yatakayohitaji mtendaji.

Tatizo la kuwa na marais 3 si la Tanganyika. Chanzo chake ni znz kutokubali kuwa na kiongozi kama waziri mkuu. Wao wanaamini uwepo wa jina rais hata kama halina maana yoyote, ni sehemu ya Utamaduni.
Hivyo huwezi kuwa na rais wa pande moja.

Serekali za majimbo hazina maana nyingine zaidi ya hizi za mikoa zilizopo. Tofauti ni kuwa viongozi wake watatokana na wananchi na kutakuwa na majimbo yenye mabunge yao ndiyo maana yanapendekezwa kwa kanda.
Hili si jambo geni, mbona kuna bunge la Texas, Crolina n.k. na yanafanya kazi bila tatizo na serikali kuu.

Mambo ya serikali kuu yameainisha kuwa saba, mengine yatashughulikiwa na serikali za washirika ambazo kama Tanganyika itaamua kuwa na majimbo nayo itakuwa na mipaka yake katika ngazi mbali mbali.

Hadi sasa hivi tuna serikali kuu, serikali za mikoa, wilaya, halmashauri, vijiji na vitongoji na hatuoni kama kuna tatizo, kwanini!

Kwa hiyo, the best option ambayo Chadema imekuja nayo ni ku-replace hao wakuu na mikoa na wilaya with serikali tatu zilizo chini ya marais watatu na utawala wa majimbo?
Mada hii imejadiliwa sana humu jamvini. Kama huna access na ufafanuzi tafuta.
 
..now, let go with ur line of thinking kwamba maraisi shirikisho watakuwa ceremonial. unashauri nini kifanyike kurekebisha tatizo hilo, wakati huo huo tuki-retain mfumo wa majimbo??

Nini madhumuni ya sera ya Chadema ya utawala wa majimbo?

..Kenya, Mozambique, Ghana, DRC, wana mfumo wa majimbo. Tunaweza kuchukua mazuri toka huko na kuachana na mabaya ya mifumo hiyo.

Lakini hawana marais watatu.
 
Ukisoma rasimu iliyopo uwepo wa Tanganyika kama ilivyo znz hauwezi kutoa kiongozi ceremonial.
Shirikisho lina mambo 7 kati ya 20+ yatakayohitaji mtendaji.

Tatizo la kuwa na marais 3 si la Tanganyika. Chanzo chake ni znz kutokubali kuwa na kiongozi kama waziri mkuu. Wao wanaamini uwepo wa jina rais hata kama halina maana yoyote, ni sehemu ya Utamaduni.
Hivyo huwezi kuwa na rais wa pande moja.

Serekali za majimbo hazina maana nyingine zaidi ya hizi za mikoa zilizopo. Tofauti ni kuwa viongozi wake watatokana na wananchi na kutakuwa na majimbo yenye mabunge yao ndiyo maana yanapendekezwa kwa kanda.
Hili si jambo geni, mbona kuna bunge la Texas, Crolina n.k. na yanafanya kazi bila tatizo na serikali kuu.

Mambo ya serikali kuu yameainisha kuwa saba, mengine yatashughulikiwa na serikali za washirika ambazo kama Tanganyika itaamua kuwa na majimbo nayo itakuwa na mipaka yake katika ngazi mbali mbali.

Hadi sasa hivi tuna serikali kuu, serikali za mikoa, wilaya, halmashauri, vijiji na vitongoji na hatuoni kama kuna tatizo, kwanini!

Unaposema kuwa serikali za majimbo hazina maana nyingine zaidi ya hizo za mikoa zilizopo; kwamba hivi sasa tuna serikali kuu, serikali za mikoa, wilaya, halimashauri, nk., na hakuna tatizo, then what is the point of having serikali za majimbo?

Kama hakuna tatizo then why Chadema is trying to fix something which is not broken?
 
Unaposema kuwa serikali za majimbo hazina maana nyingine zaidi ya hizo za mikoa zilizopo; kwamba hivi sasa tuna serikali kuu, serikali za mikoa, wilaya, halimashauri, nk., na hakuna tatizo, then what is the point of having serikali za majimbo? Kama hakuna tatizo then why Chadema is trying to fix something which is not broken?
Mkuu EMT, kwanza, huu ni mtazamo wangu, siwakilishi mawazo au ufafanuzi wa chama chochote.

Pili, hukunisoma vizuri hapo juu. Nimeeleza kuwa hata sasa hivi tuna serikali za mitaa, wilaya na mikoa. Tofauti na mfumo wa majimbo, katika majimbo serikali inachaguliwa na wananchi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na inakuwa answerable kwa wananchi.

Wakati wa mkoloni kulikuwa na majimbo(province) kutegemeana na interest za maeneo.
Kanda ya ziwa(lake province) Mwanza, Mara na Kagera ambazo ukiangalia interest zao katika mazao kama pamba na uvuvi zilikuwa sawa na ndilo chimbuko la Nyanza cooperative union.

Ndivyo ilivyokuwa kwa mikoa ya kaskazini, Kilimanjaro, Tanga na Arusha.
kwa nguvu ya kahawa ndipo kilipotokea KNCU na vile vya mikonge.

Kulikuwa na local authority zilizokuwa na uwezo wa kuratibu mipango kulingana na matakwa yao. Ndilo chimbuko la shule za NA kwa maana ya Native authority.
Ukiangalia vyama vya ushirika na NA utaona vilikuwa na maendeleo makubwa sana kwasababu viliwajibika kwa wananchi pale walipo na si serikali kuu.

Huo ni mfano mmoja tu. Tofauti na sasa serikali za mikoa na halmashauri zinawajibika kwa serikali kuu. Watawala wanaletwa kutoka Dar es Salaam wakiwa hawajui vipaumbele vya wananchi. Mipango inapangwa Dodoma bila kuangalia haja za maeneo.

Mfano,Dodoma wanapotenga pesa kwa ajili ya shule za kata nchi nzima ni uharibifu wa pesa.
Mkoa wa Kilimanjaro ulishamaliza mambo hayo, tatizo lao si shule. Tatizo la Kilimnajaro ni kufufua kilimo cha umwagiliaji. Hii ni tofauti na Lindi ambako tatizo lao ni shule.

Watu wa kanda ya kaskazini (Arusha, Tanga, Kilimanjaro) wanaweza kutumia fursa za shule za Kilimanjaro kwa pamoja na kuendeleza kilimo cha umwagiliaji na kanda zingine zikiwa na vipau mbele vyao.

Serikali za majimbo zitakuwa na mabunge yao kutokana na resource zao.
Watalipa kodi serikali kuu, sehemu kubwa ya mapato yao yanabaki jimboni.
Tofauti na sasa ambapo mkoa unaolipa mapato taifa unapata mgao mdogo wa pato la taifa.

Nimalizie kusema sasa hivi tuna serikali za mikoa na vijiji kama mkono mrefu wa serikali.
Tunatakiwa tuwe na serikali zisizo na ufungamano na serikali kuu katika mambo yasiyohusiana na serikali kuu, ziwe independent.

Hofu ya kuwepo serikali nyingi na ku-adulterate power ya serikali nyingine ina mashiko tu pale ambapo hakuna mpangilio wa majukumu. Vinginevyo tuna mifano maelfu ya duniani yakuthibitisha hili.
 
pole mkuu, unayemwambia kajitoa akili kwa makusudi!
 
Last edited by a moderator:
Ukitaka kumdanganya mtanzania weka mambo kwa maandishi lakini kwa kusikia na kuona hawadanganyiki lakini ni warahisi kusahau.

hoja ya serikali 3 ni hoja ya wananchi na sio cdm,rejea ripoti ya tume ya marehemu Nyalali.....na hii ya warioba,
Ni kweli serikali ya majimbo ni cdm,nayo haina madhara kwa kupeleka madaraka kwa wananchi,mbona makanisa wametumia mfumo huo miaka nenda rudi na umeonyesha ufanisi?

gharama sio hoja kwani tume ya Warioba walishatoa majawabu.
Kazi za wakuu wa mikoa na wilaya ni zipi zaidi ya kuwa makada wa ccm kwa gharama za wananchi wote badala ya gharama za ccm tu.
 
Wanataka na wao waongoze serikali Yao ya majimbo maana kupata Urais Kwao ni ndoto na haiwezekani.
 
CHADEMA wanataka kuwe na serikali tatu. Wakati huo huo wanataka kuwe serikali ya majimbo. Kwa maana hiyo, kutakuwa na Rais wa Muungano na wakuu wawili wa serikali za Bara na Zanzibar. Pia kutakuwepo na gavana katika kila jimbo ambao watakuwa na mamlaka kamili kwenye majimbo yao.

Ukiondoa suala la gharama ambalo kwa demokrasia ni vyema kuzipitia kiutawala hii imekaa sawa? Utawala wa majimbo chini ya serikali tatu unawezekana? Dhana kuu ya sera ya serikali ya majimbo ni kuhamisha madaraka ya maamuzi kutoka kwa watu wachache na kuyarejesha mikononi mwa wananchi vijijini.

Kama ni hivyo, hizo serikali mbili za Bara na Zanzibar zitakazokuwa zinaongozwa na wakuu wawili zitakuwa zinafanya nini? Madaraka ya wakuu wa serikali hizo mbili hayatagongana na madaraka ya magavana wa majimbo? Kama serikali moja chini ya utawala wa majimbo haiwezekani, solution ni kuwa na utawala wa majimbo chini ya serikali tatu?

Binafsi nadhani Chadema walipokuja na hoja ya majimbo, hawakutarajia kwamba baadae, hoja ya serikali tatu ingepokelewa kwa mikono miwili na umma; Nadhani (sina uhakika) Chadema wali amini kwamba kuivunja 'unitary system' iliyopo isingekuwa kitu kirahisi, sasa kwa vile nia yao kama chama ni kutafuta ufanisi zaidi ndani ya mfumo uliopo, basi wakaona kwamba sera ya majimbo ingekuja na jibu ambapo madaraka na maamuzi juu ya uendeshaji wa serikali pamoja na rasilimali za wananchi, masuala haya (maamuzi na madaraka) yanasogea karibu zaidi na wananchi, badala ya kuwa centralized kama sasa ambapo manufaa kwa wananchi hayaonekani;

Katika mazingira ya sasa ambapo hoja ya Tanganyika inazidi kupamba moto, kuna umuhimu wa Chadema kujipanga vizuri ili wasionekane kwamba wanachanganya wananchi kwani ni jambo rahisi sana kwa viongozi wa CCM kubomoa hoja ya serikali tatu iwapo itaunganishwa na hoja ya serikali ya majimbo, hasa katika muktadha wa muungano kama ulivyoainisha hapo juu ambapo kwa kweli its impractical in a multitude of ways;

That said and done, haina maana kwamba taifa haliwezi kuwa na federal government, provincial governments and local governments kwa wakati mmoja kwani mafanikio ya federalism duniani (USA, Canada na Australia) wote wanafuata mfumo wa namna hii na wamekuwa na ufanisi wa hali ya juu katika kuboresha maisha ya wananchi wao, na ni sababu kubwa kwanini mataifa mengi yanakimbilia mfumo wa shirikisho vis a vis unitary system of governance; Tukichukulia mfano wa Marekani, taifa hili lina serikali zaidi ya hamsini (50) – kwa mfano, kuna federal government yenye katiba yake, na pia kuna 50 states, kila moja ikiwa na Katiba zake; Hii ni nje ya serikali za mitaa ambazo pia zipo marekani, na zipo zaidi ya serikali za mitaa 30,000 (elfu thelathini); Tukiingia Canada, they have ten provinces, each with its own government, kwahiyo ukijumlisha na serikali kuu, Canada ina serikali sio chini ya kumi na moja; Tukienda Australia, kule kuna six provinces , hivyo kufanya jumla ya serikali kuwa sio chini ya saba; Kwa maana hii, shirikisho la serikali tatu, nne, tano, kumi.... sio tatizo, suala la maana ni je, nani ni washirika wa shirikisho husika? Lengo lao ni kufanikisha nini? Wapo tayari ku surrender mambo gani kwa shirikisho husika? Vinginevyo wananchi katika taifa lolote lile huwa tayari kugharamia mfumo wowote ambao haulazimishwi kwao bali unaotokana na matakwa yao baada ya kuridhika juu ya ufanisi wa mfumo husika;

Nimalizie kwa kusema kwamba - kama Chadema inakabaliwa na changamoto kubwa katika mjadala unaoendelea, basi zaidi ni katika kutetea hoja juu ya mfumo wa shirikisho la serikali tatu unaofuata sera ya majimbo; Hoja ya Chadema inaweza kuwa practical kwa njia tatu:

- Kwanza iwapo Zanzibar 'kwa hiyari yake' itaamua to surrender safari yake towards full autonomy and self determination na badala yake kukubali kutambulika kama moja ya majimbo ya "Tanzania"; Hata hivyo, chini ya utaratibu huu, haitakuwa tena serikali tatu, bali kuu moja na nyingine kadhaa za majimbo ya tanganyika na majimbo ya zanzibar (aidha kama jimbo moja au kama mawili - Pemba na Unguja); Chini ya utaratibu huu, Zanzibar kama jimbo pamoja na majimbo mengine ya Tanganyika (lets say seven provinces?) kutakuwepo na distribution of power kwa majimbo husika, with each of the spheres (majimbo) having 'constitutionally' given powers and functions kama ilivyo kwa majimbo ya Marekani, n.k; Chini ya mfumo huu, the federal government will have powers of over sight over provincial governments (Za Tanganyika na Zanzibar), & provincial governments will have power of oversight on municipal governments;

- Pili, iwapo Tanganyika na Zanzibar zitaamua kwa hiyari kuungana, huku wakikubaliana kwamba mamlaka halisi yabakie katika nchi moja moja binafsi; Katika mfumo huu, serikali kuu (ya muungano) haitakuwa na nguvu; Mfano mzuri ni mfumo wa European Union ambapo nchi binafsi kama vile Ufaransa, Ujerumani, Uingereza, Uholanzi, Italia, Ureno, n.k zina nguvu ya kufanya maamuzi ya mwisho na sio bunge la Jumuiya ya Ulaya au Watendaji wake;

- Tatu, iwapo Muungano utavunjika, hivyo Tanganyika to pursue mfumo wa majimbo kwa urahisi zaidi;

Nje ya sura hizi tatu, binafsi sioni jinsi gani Chadema wanaweza kutetea Sera ya majimbo katika muktadha wa muungano; Vinginevyo ningependa kuelimishwa zaidi juu ya hili;
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mkuu EMT, kwanza, huu ni mtazamo wangu, siwakilishi mawazo au ufafanuzi wa chama chochote.

Pili, hukunisoma vizuri hapo juu. Nimeeleza kuwa hata sasa hivi tuna serikali za mitaa, wilaya na mikoa. Tofauti na mfumo wa majimbo, katika majimbo serikali inachaguliwa na wananchi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na inakuwa answerable kwa wananchi.

Wakati wa mkoloni kulikuwa na majimbo(province) kutegemeana na interest za maeneo.
Kanda ya ziwa(lake province) Mwanza, Mara na Kagera ambazo ukiangalia interest zao katika mazao kama pamba na uvuvi zilikuwa sawa na ndilo chimbuko la Nyanza cooperative union.

Ndivyo ilivyokuwa kwa mikoa ya kaskazini, Kilimanjaro, Tanga na Arusha.
kwa nguvu ya kahawa ndipo kilipotokea KNCU na vile vya mikonge.

Kulikuwa na local authority zilizokuwa na uwezo wa kuratibu mipango kulingana na matakwa yao. Ndilo chimbuko la shule za NA kwa maana ya Native authority.
Ukiangalia vyama vya ushirika na NA utaona vilikuwa na maendeleo makubwa sana kwasababu viliwajibika kwa wananchi pale walipo na si serikali kuu.

Huo ni mfano mmoja tu. Tofauti na sasa serikali za mikoa na halmashauri zinawajibika kwa serikali kuu. Watawala wanaletwa kutoka Dar es Salaam wakiwa hawajui vipaumbele vya wananchi. Mipango inapangwa Dodoma bila kuangalia haja za maeneo.

Mfano,Dodoma wanapotenga pesa kwa ajili ya shule za kata nchi nzima ni uharibifu wa pesa.
Mkoa wa Kilimanjaro ulishamaliza mambo hayo, tatizo lao si shule. Tatizo la Kilimnajaro ni kufufua kilimo cha umwagiliaji. Hii ni tofauti na Lindi ambako tatizo lao ni shule.

Watu wa kanda ya kaskazini (Arusha, Tanga, Kilimanjaro) wanaweza kutumia fursa za shule za Kilimanjaro kwa pamoja na kuendeleza kilimo cha umwagiliaji na kanda zingine zikiwa na vipau mbele vyao.

Serikali za majimbo zitakuwa na mabunge yao kutokana na resource zao.
Watalipa kodi serikali kuu, sehemu kubwa ya mapato yao yanabaki jimboni.
Tofauti na sasa ambapo mkoa unaolipa mapato taifa unapata mgao mdogo wa pato la taifa.

Nimalizie kusema sasa hivi tuna serikali za mikoa na vijiji kama mkono mrefu wa serikali.
Tunatakiwa tuwe na serikali zisizo na ufungamano na serikali kuu katika mambo yasiyohusiana na serikali kuu, ziwe independent.

Hofu ya kuwepo serikali nyingi na ku-adulterate power ya serikali nyingine ina mashiko tu pale ambapo hakuna mpangilio wa majukumu. Vinginevyo tuna mifano maelfu ya duniani yakuthibitisha hili.

Ipo mifano mingi tuu duniani kuhusu serikali za majimbo. Lakini sijui kama unaweza kunipa mfano wa nchi ambayo ina marais watatu na pia serikali ya majimbo.

Nadhani watu wengi wanaangalia pendekezo la serikali tatu separately from utawala wa majimbo. Lakini hoja yangu ni kuwepo kwa mfumo wa serikali tatu unaofuata sera ya majimbo. Mchambuzi amejaribu kutoa options tatu.

Option ya Zanzibar ku-surrender its current autonomy na kukubali kuwa jimbo au majimbo mawili sidhani kama inaweza kukubaliwa huko Zanzibar. At the moment, I don't think Zanzibar is willing to loose its autonomy but strengthen it even more.

Option ya pili ya Tanganyika na Zanzibar kuungana na kukubaliana kuwa mamlaka halisi yabakie katika nchi moja, means that effectiveness ya huo muungano utategemea na political will ya pande zote. Pia kwa vile tunafuata dualist approach ina maana kuwa sheria ambazo zitakuwa zinapitishwa na bunge la muungano lazima ziwe incorporated by an Act of Parliament of the respective States. Muungano wa aina hii utakuwa karibia na East African Community which we are struggling to accept.

Option ya tatu ni kuvunjika kwanza kwa muungano ili Tanganyika iweze kuwa na rais mmoja pekee chini ya utawala wa majimbo. Kinachofanyika sasa ni kujaribu kuimarisha muungano kwa kuwa na serikali tatu.
 
Inawezekana,mbona serikali mbili iliwezekana na wakuu wa mikoa ambao ni shemeji zao waliowateua,iweje ishindikane kwa magavana anbao watapigiwa kura!
 
Ukitaka kumdanganya mtanzania weka mambo kwa maandishi lakini kwa kusikia na kuona hawadanganyiki lakini ni warahisi kusahau.

hoja ya serikali 3 ni hoja ya wananchi na sio cdm,rejea ripoti ya tume ya marehemu Nyalali.....na hii ya warioba, Ni kweli serikali ya majimbo ni cdm,nayo haina madhara kwa kupeleka madaraka kwa wananchi,mbona makanisa wametumia mfumo huo miaka nenda rudi na umeonyesha ufanisi?

gharama sio hoja kwani tume ya Warioba walishatoa majawabu.
Kazi za wakuu wa mikoa na wilaya ni zipi zaidi ya kuwa makada wa ccm kwa gharama za wananchi wote badala ya gharama za ccm tu.

Sijasema kuwa hoja ya serikali tatu ni ya Chadema. Ila nilichosema ni kwamba Chadema inaunga mkono pendekezo la serikali tatu.

Pia sijasema kuwa utawala wa majimbo hauna ufanisi. Hoja yangu ipo kwenye how mfumo wa serikali tatu aka marais watatu fits into utawala wa majimbo?

Makanisa yana utawala wa majimbo lakini sidhani kama yana mkuu wa kanisa Tanzania (muungano), then Mkuu wa Kanisa Tanzania Bara na Mkuu wa kanisa Zanzibar. Umenipata?

Kwa mfano, Jimbo Katoliki la Zanzibar ni mojawapo kati ya majimbo 33 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Kwa hiyo, kule Zanzibar kuna mkuu wa jimbo tuu na siyo mkuu wa kanisa hilo kwa upande wa Zanzibar. Pia huku Bara hakuna mkuu wa kanisa wa Tanzania bara aka Tanganyika.

....Nimalizie kwa kusema kwamba - kama Chadema inakabaliwa na changamoto kubwa katika mjadala unaoendelea, basi zaidi ni katika kutetea hoja juu ya mfumo wa shirikisho la serikali tatu unaofuata sera ya majimbo; ...

Hoja yangu ndiyo ipo hapo. Ila baadhi ya watu wanajadili sera ya majimbo na mfumo wa shirikisho la serikali tatu separately. Wachache wanajaribu ku-reconcile these two systems and how they can work together, let alone be implemented successfully.

Practically, hizo options mbili za mwanzo ulizotoa ni ngumu kuwa implemented.

Option ya tatu maybe Chadema wanaunga mkono mfumo wa shirikisho la serikali tatu with a hope kuwa mfumo huu utaharakisha kuvunjika kwa muungano.

Baada ya kuvunjika kwa muungano, then itakuwa rahisi kuanzisha mfumo wa utawala wa majimbo Tanganyika kwa sababu kikwazo cha Zanzibar hakitakuwepo tena.
 
Inawezekana,mbona serikali mbili iliwezekana na wakuu wa mikoa ambao ni shemeji zao waliowateua,iweje ishindikane kwa magavana anbao watapigiwa kura!

Useme tuu inawezekana. Sema inawezekana kivipi. Unasema mbona serikali mbili inawezekana as if tayari tuna utawala wa majimbo.

The fact kuwa magavana watapigiwa kura haina maana kuwa hukutakuwa na uteuzi wa "shemeji zao" ambao hatimaye watapigiwa kura.

Kama imewezekana kuteua wagombea ubunge "ambao ni shemeji zao" kugombea ubunge watashindwa kufanya hivyo kwa hao magavana?
 
Back
Top Bottom