CHADEMA, serikali tatu na serikali ya majimbo

Serikali za majimbo ni tamu hasa mnapoamua kuwa na serikali moja kama ilivyo Marekani. Tatizo ni Wazanzibar ambao muungano wanautaka huku wakitaka kuwa na madaraka yao hapo hapo. Hiyo haiwezekani. Tukubali serikali tatu kwa sasa hasa ukizingatia matukio ya kidhalimu yanayotokea Zanzibar kwa sasa. Kuendelea kung'ang'ania serikali mbili hasa kwa wenzangu wa CCM kwa sasa ni kuendeleza maumivu kwa wakristo wanaoishi Zanzibar hasa ukizingatia maelezo yaliyotolewa na padri kutoka Zanzibar hivi karibuni. Tatizo lilipo kwenye CCM kwa sasa ni watu kukosa ajira na kudhani ukitoa maoni tofauti wa wakubwa ambao ni watu wachache tu hata kumi hawafiki basi mtu hawezi kupata ukuu wa wilaya au mkoa. Haya ni makosa makubwa, tutakuwa na kizazi ambacho hakitaweza kufikiri mbele itakuwaje.

Kwa hiyo sera ya Chadema ya majimbo umewekwa kapuni effectively mpaka hapo muungano utakapovunjika?
 
CHADEMA wanataka kuwe na serikali tatu. Wakati huo huo wanataka kuwe serikali ya majimbo. Kwa maana hiyo, kutakuwa na Rais wa Muungano na wakuu wawili wa serikali za Bara na Zanzibar. Pia kutakuwepo na gavana katika kila jimbo ambao watakuwa na mamlaka kamili kwenye majimbo yao.

Ukiondoa suala la gharama ambalo kwa demokrasia ni vyema kuzipitia kiutawala hii imekaa sawa? Utawala wa majimbo chini ya serikali tatu unawezekana? Dhana kuu ya sera ya serikali ya majimbo ni kuhamisha madaraka ya maamuzi kutoka kwa watu wachache na kuyarejesha mikononi mwa wananchi vijijini.

Kama ni hivyo, hizo serikali mbili za Bara na Zanzibar zitakazokuwa zinaongozwa na wakuu wawili zitakuwa zinafanya nini? Madaraka ya wakuu wa serikali hizo mbili hayatagongana na madaraka ya magavana wa majimbo? Kama serikali moja chini ya utawala wa majimbo haiwezekani, solution ni kuwa na utawala wa majimbo chini ya serikali tatu?
Jamani hebu tujadili na hili,katika rasimu ya katiba mpya inayopendekeza muundo wa serikali tatu kwa kuwa na "SHIRIKISHO" la bara na visiwani kwa kumaanisha kwamba Muungano wetu utaendelea kuwepo mimi naona si sahihi kwani kama tunahitaji muungano basi tuwe na serikali moja tu.Mantiki yangu ni kwamba,maneno yaliyotumika ambayo ni "JAMHURI YA MUUNGANO" kwa sasa na "SHIRIKISHO" kwa hii rasimu ni maneno yenye maana tofauti kwani MUUNGANO haina maana sawa na SHIRIKISHO hivyo basi ni maoni yangu kwamba rasimu hii ya katiba yenye muundo wa serikali 3 pamoja na watu wote wanaopendekeza hilo shirikisho naona wanatupotosha kwani endapo tutapata katiba itakayotamka "SHIRIKISHO" wao wanasiasa watakuja na tafsiri ya kisheria ambayo itaonesha maana sahihi ya SHIRIKISHO ambayo haipo sawa na maana halisi ya neno MUUNGANO.

"TUNAWEZA KUSHIRIKIANA KUPITIA SHIRIKISHO LA NCHI MBILI LAKINI TUSIUNGANE"

HIVYO BASI KAMA TUNAUHITAJI MUUNGANO TUWE NA SERIKALI MOJA YA MUUNGANO TU.AHSANTENI wazalendo watanzania wenzangu.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Serikali za Majimbo ni Sera ya Chadema itakapoungwa mkono kushika madaraka.

Serikali tatu ni mapendekezo yaliyopo mezani ambayo wote tunashiriki kuyajadiri na kuyatolea maamuzi bila kujali itikadi zetu.

Nakukumbusha tu sera ya CCM ni UJAMAA na KUJITGEMEA. Tumekuwa wajamaa lini na tunajitegemea kivipi?

Hoja yako mezani naiona kama ya kichochezi kwa sababu suala la majimbo halipo kwenye mjadala wa sasa kuhusu katiba. Suala la serikali tatu ndilo suala mezani tujadili.

Narudia kwa hali ya sasa nafarijika na maoni ya Katiba kuhusu serikali tatu na hasa ya ikiwemo serikali HALISI YA TANGANYIKA.

Naongolea sera ya mfumo mpya wa utawala ya Chadema (siyo rasimu ya katiba) and how one can reconcile it na Chadema kuunga mkono mapendekezo ya kuwa na serikali tatu.

Otherwise, ni sawa na kuniambia kuwa mependekezo ya kuwa na serikali tatu automatically yamefutilia mbali sera ya utawala wa majimbo ya Chadema? Is that what you are trying to say?
 
Kama unataka jibu rahisi ni HAPANA
 
Jamani hebu tujadili na hili,katika rasimu ya katiba mpya inayopendekeza muundo wa serikali tatu kwa kuwa na "SHIRIKISHO" la bara na visiwani kwa kumaanisha kwamba Muungano wetu utaendelea kuwepo mimi naona si sahihi kwani kama tunahitaji muungano basi tuwe na serikali moja tu.Mantiki yangu ni kwamba,maneno yaliyotumika ambayo ni "JAMHURI YA MUUNGANO" kwa sasa na "SHIRIKISHO" kwa hii rasimu ni maneno yenye maana tofauti kwani MUUNGANO haina maana sawa na SHIRIKISHO hivyo basi ni maoni yangu kwamba rasimu hii ya katiba yenye muundo wa serikali 3 pamoja na watu wote wanaopendekeza hilo shirikisho naona wanatupotosha kwani endapo tutapata katiba itakayotamka "SHIRIKISHO" wao wanasiasa watakuja na tafsiri ya kisheria ambayo itaonesha maana sahihi ya SHIRIKISHO ambayo haipo sawa na maana halisi ya neno MUUNGANO.

"TUNAWEZA KUSHIRIKIANA KUPITIA SHIRIKISHO LA NCHI MBILI LAKINI TUSIUNGANE"

HIVYO BASI KAMA TUNAUHITAJI MUUNGANO TUWE NA SERIKALI MOJA YA MUUNGANO TU.AHSANTENI wazalendo watanzania wenzangu.

Hoja ya kuwa na serikali moja na utawala wa majimbo imekaa sawa?

Kama imekaa sawa lakini haikubaliwi Zanzibar, basi suluhisho ni kuwa na serikali tatu na pia utawala wa majimbo?
 
Kama unataka jibu rahisi ni HAPANA

Kama jibu ni hapana, then how do you reconcile utawala wa majimbo na serikali tatu?

Nimeandika hapo juu, kwa mfano, chukulia madaraka ya magavana wa majimbo katika nchi kama Marekani au mawaziri wakuu wa majimbo ya Afrika ya Kusini.

Huoni kuwa madaraka ya wakuu wa serikali ya Bara na ile ya Zanzibar yatakuwa almost sawa na madaraka ya magavana wa majimbo?

How would you demarcate the powers kati ya serikali za bara na visiwani na serikali za majimbo?
 
Cdm ni wakatolic ndiyo maana wanafuata formula za kanisa kama chama rafiki cha german cha cdu sasa formula hiyo hapa haitufai,kwa sababu tayarikuna mpango wa serikali 3,kiufupi utawala wamajimbo haufai,kwasababu kuna majimbo mengine yapo mbele kimaendeleo na mengine yapo nyuma kimaendelo ,leo hii unaweza kufananisha arusha na lindi? Huo ni ukatolic tu,haumna chama hapo kuna kanisa tu.
 
Sikatai kuwa mfumo wa sasa wa tawala za mikoa una malengo ya kisiasa zaidi kuliko ya kiutawala na kimaendelea.

Sikatai kuwa mfumo wa tawala za mikoa unadhibitiwa kisiasa na watawala mawakala wanaounda tawala za mikoa.

Pia sikatai kuwa uanzishwaji wa mfumo wa majimbo utapunguza gharama za uendeshaji.

Vile vile sipingi malengo ya utawala wa majimbo.

Suala langu lipo kwenye how do you reconcile utawala wa majimbo na serikali tatu?

Chukulia, kwa mfano, madaraka ya magavana wa majimbo katika nchi kama Marekani au mawaziri wakuu wa majimbo ya Afrika ya Kusini.

Huoni kuwa madaraka ya wakuu wa serikali ya Bara na ile ya Zanzibar yatakuwa almost sawa na madaraka ya magavana wa majimbo?

Nadhani tatizo lako hapa ni hili neno "jimbo" ambalo kimsingi tunaweza liita "mkoa". Tofauti ya Mikoa ya sasa na Majimbo yanayozungumziwa ni kuondoa utegemezi wa kifikra( Entitled Mentality), kiutendaji na kisera kutoka kwa serikali kuu(central government) ambayo kwa mfumo wa serikali tatu ni serikali washirika Zanzibar na Tanganyika ambao wanaunda federation.

Majukumu mengi ya kiutendaji kisekta yatasimamiwa na kutekelezwa na Magavana na majukumu ya kiwizara yatasimamiwa na serikali washirika zikiongozwa na wakuu wa serikali hizi.Kimsingi kuna Psychological problem ambayo naiona kwa watu wengi ambayo ni neno "Rais" kwa mantiki wa Maraisi watatu ambapo kimsingi wangeitwa 'Mawaziri Wakuu" au jina lingine ambalo litaondoa utata huu.Nadhani hili linapaswa kuangaliwa katika kuandaa katiba za nchi washirika.
 
CHADEMA wanataka kuwe na serikali tatu. Wakati huo huo wanataka kuwe serikali ya majimbo. Kwa maana hiyo, kutakuwa na Rais wa Muungano na wakuu wawili wa serikali za Bara na Zanzibar. Pia kutakuwepo na gavana katika kila jimbo ambao watakuwa na mamlaka kamili kwenye majimbo yao.

Ukiondoa suala la gharama ambalo kwa demokrasia ni vyema kuzipitia kiutawala hii imekaa sawa? Utawala wa majimbo chini ya serikali tatu unawezekana? Dhana kuu ya sera ya serikali ya majimbo ni kuhamisha madaraka ya maamuzi kutoka kwa watu wachache na kuyarejesha mikononi mwa wananchi vijijini.

Kama ni hivyo, hizo serikali mbili za Bara na Zanzibar zitakazokuwa zinaongozwa na wakuu wawili zitakuwa zinafanya nini? Madaraka ya wakuu wa serikali hizo mbili hayatagongana na madaraka ya magavana wa majimbo? Kama serikali moja chini ya utawala wa majimbo haiwezekani, solution ni kuwa na utawala wa majimbo chini ya serikali tatu?

Chadema ilipendekeza kuwepo na mfumo wa majimbo haukukubaliwa na tume, lakini pia tumekuwa na sera ya serikali tatu na kwenye katiba tulipendekeza na hiyo ikakubalika, shida ya nini sasa mkuu.. Au swala ni Buku saba tu..
 
Kama jibu ni hapana, then how do you reconcile utawala wa majimbo na serikali tatu?

Nimeandika hapo juu, kwa mfano, chukulia madaraka ya magavana wa majimbo katika nchi kama Marekani au mawaziri wakuu wa majimbo ya Afrika ya Kusini.

Huoni kuwa madaraka ya wakuu wa serikali ya Bara na ile ya Zanzibar yatakuwa almost sawa na madaraka ya magavana wa majimbo?

How would you demarcate the powers kati ya serikali za bara na visiwani na serikali za majimbo?

Hii ni Tanzania si Marekani.

Hakuna majimbo kwa sasa.

Kwenye kufikia lengo kuu la utawala wa majimbo, mimi binafsi naona umuhimu wa kurudisha serikali ya Tanganyika kwanza kama mpito fulani. Zanzibar wana masheha nadhani ni aina yao ya utawala wao ambao siujui na sitaki kuujua kwa sababu wana Katiba yao. Tukipata Tanganyika yetu tutajadiri namna ya kujitawala kwenye mazingira ya kiTanganyika. CHADEMA ikishika madaraka ni kwamba tutakuwa tumekubali serikali za majimbo; hilo litaangaliwa na kuamuliwa kikatiba au kisheria. Natumaini wakati huo "demarcations" (mipaka ya madaraka) itaainishwa.
 
Nadhani tatizo lako hapa ni hili neno "jimbo" ambalo kimsingi tunaweza liita "mkoa". Tofauti ya Mikoa ya sasa na Majimbo yanayozungumziwa ni kuondoa utegemezi wa kifikra( Entitled Mentality), kiutendaji na kisera kutoka kwa serikali kuu(central government) ambayo kwa mfumo wa serikali tatu ni serikali washirika Zanzibar na Tanganyika ambao wanaunda federation.

Majukumu mengi ya kiutendaji kisekta yatasimamiwa na kutekelezwa na Magavana na majukumu ya kiwizara yatasimamiwa na serikali washirika zikiongozwa na wakuu wa serikali hizi.Kimsingi kuna Psychological problem ambayo naiona kwa watu wengi ambayo ni neno "Rais" kwa mantiki wa Maraisi watatu ambapo kimsingi wangeitwa 'Mawaziri Wakuu" au jina lingine ambalo litaondoa utata huu.Nadhani hili linapaswa kuangaliwa katika kuandaa katiba za nchi washirika.

Hata kama wakuu wa hizo serikali mbili wangeitwa mawaziri wakuu, watakuwa wanasimamia wizara zinazofanya kazi gani kama shughuli nyingi zitakuwa zimehamishiwa kwenye majimbo? Gavan wa jimbo atakuwa anawajibika kwa nani?
 
Chadema ilipendekeza kuwepo na mfumo wa majimbo haukukubaliwa na tume, lakini pia tumekuwa na sera ya serikali tatu na kwenye katiba tulipendekeza na hiyo ikakubalika, shida ya nini sasa mkuu.. Au swala ni Buku saba tu..

Divide and rule mnayotumia wafuasi wa CCM na CDM usidhani unaweza kui-apply kwa kila mtu.

Sawa Chadema ilipendekeza kuwepo na mfumo wa majimbo lakini haukukubaliwa na tume.

Lakini pia imekuwa na sera ya serikali tatu na kwenye katiba walipendekeza na hiyo ikakubalika.

Swali na siyo shida au buku saba ni Chadema kwa hiyo imetupilia mbali sera yake ya majimbo baada ya kukataliwa?
 
CHADEMA wanataka kuwe na serikali tatu. Wakati huo huo wanataka kuwe serikali ya majimbo. Kwa maana hiyo, kutakuwa na Rais wa Muungano na wakuu wawili wa serikali za Bara na Zanzibar. Pia kutakuwepo na gavana katika kila jimbo ambao watakuwa na mamlaka kamili kwenye majimbo yao.

Ukiondoa suala la gharama ambalo kwa demokrasia ni vyema kuzipitia kiutawala hii imekaa sawa? Utawala wa majimbo chini ya serikali tatu unawezekana? Dhana kuu ya sera ya serikali ya majimbo ni kuhamisha madaraka ya maamuzi kutoka kwa watu wachache na kuyarejesha mikononi mwa wananchi vijijini.

Kama ni hivyo, hizo serikali mbili za Bara na Zanzibar zitakazokuwa zinaongozwa na wakuu wawili zitakuwa zinafanya nini? Madaraka ya wakuu wa serikali hizo mbili hayatagongana na madaraka ya magavana wa majimbo? Kama serikali moja chini ya utawala wa majimbo haiwezekani, solution ni kuwa na utawala wa majimbo chini ya serikali tatu?

EMT kwa kuanzia napenda kukuuliza Serikali ya Zanzibar sasa inafanya nini? Halafu nigekuuliza tena ulioona wapi nchi ikawa haina serikali? Yaani Tanganyika iwe ni nchi pekee katika uso wa dunia ambayo haina haja ya kuwa na serikali?

Muungano wa Tanzania ni muungano wa nchi mbili na hivyo inawajibika kila upande uwe na serikali yake iwapo makubaliano sio kufanya muungano wa nchi moja kama ulivyo wetu wa Tanzania.

Usawa uko wapi kama nchi moja inakuwa na serikali yake, usawa uko wapi ikiwa wananchi wa upande mmoja wanajihudumia kupitia serikali yao, huku upande mmoja unaongozwa na mchanganyiko wa pande mbili na wananchi wake wakitumia pato la jumla la pande mbili?

Inawezekana mtu alie nje ya taifa hili asifahamu huo mchakachuo uliopo na akashangaa huu ni mseto wa namna gani. Kuondowa mtafaruku huu ndio kunapohitajika kuwa na serikali ya Tanganyika.

Sasa nikujibu Serikali ya Tanganyika itakuwa inafanya nini. Serikali ya Tanganyika itakuwa inashughulikia mambo ya kiutawala wa Tanganyika na itakuwa haiingiliwi katika mamdo ya Watanganyika kama vile inavyofanyika kule zanzibar. Tanganyika itaamuwa iwe na wabunge wangapi na si lazima iwe wabunge wawe wengi kama sasa eti kila wilaya kuwa na mbunge. Pengine hayo majimbo yatatowa wabunge kwa bunge la Tanganyika. Kuulizia mfumo na gharama ni jambo la kipuuzi kwani tangu tulikpopata uhuru tumekuwa na mfumo mmoja? Mfumo wa utawala ni kitu cha kupangwa kulingana na mazingira na matakwa.
 
Chadema ni bendela fuata upepo wao siku zote hawana hoja wanafuata yale yanayotokea kwenye jamii ndiyo wanaruka nayo.
Wasipofuata yanayotokea kwenye jamii watakuwa wanawahudumia akina nani?akili nyingine bwana acha Tu
 
Hii ni Tanzania si Marekani.

Sijasema kuwa Tanzania ni sawa na Marekani, bali nimetolewa mfano wa utawala wa majimbo na Marekani na Afrika Kusini.

Hakuna majimbo kwa sasa.

Hakuna majimbo kwa sasa wapi? Kwenye serikali ya sasa au mfumo wa kitawala unaotumiwa na Chadema sasa?

Kwenye kufikia lengo kuu la utawala wa majimbo, mimi binafsi naona umuhimu wa kurudisha serikali ya Tanganyika kwanza kama mpito fulani. Zanzibar wana masheha nadhani ni aina yao ya utawala wao ambao siujui na sitaki kuujua kwa sababu wana Katiba yao. Tukipata Tanganyika yetu tutajadiri namna ya kujitawala kwenye mazingira ya kiTanganyika. CHADEMA ikishika madaraka ni kwamba tutakuwa tumekubali serikali za majimbo; hilo litaangaliwa na kuamuliwa kikatiba au kisheria. Natumaini wakati huo "demarcations" (mipaka ya madaraka) itaainishwa.

Kwa hiyo, unachojaribu kusema ni kuwa kwenye serikali chini ya Chadema kutakuwa aina mbili za utawala.

Kwamba, kwa upande wa Tanganyika kutakuwa na utawala wa majimbo. Kwa upande wa Zanzibar hakutakuwa na utawala wa majimbo kwa sababu tayari wana aina ya utawala wao.

Still, how would you reconcile serikali kuu ya Mungano, serikali ya Tanganyika na serikali za majimbo?
 
Kiwi, ameeleza vizuri sana.lakini kwa Tanzanian ni shida kuelewa. Chadema walipaswa kutekeleza mfumo huu kwenye sehemu ambazo wanaongoza council ili kutoa picha jinsi ambavyo wananchi wanavyoshiriki ktk kutoa maamuzi juu ya maendeleo yao ili uwe mfano,
 
Back
Top Bottom