Unajua waswahili wanasema kama waujua huu basi miye naujua huu!..
Hii habari za Chadema na ACT kusema kweli inasikitisha sana haswa wakati huu maana unapojaribu kumchafua mwenzako kumbuka naye atakuja na hasira zake na mwisho wa siku vyama vyote vitaonekana havina maana kabisa - uchaguzi haupo mbali atapona nani?. Mimi nitarudia kusema hivi, swala la kugombea Uongozi Chadema ni swala la kijinga kabisa watu wazima kugombania nafasi za uongozi ilihali wengi wenu hamna VISION zaidi ya kuwa mabehewa mkifuata kichwa!. Hivi hamuoni hata aibu jamani kugomba wakati huu ambao CCM inatafuta pa kutokea!
Ugonvi baina ya Zitto na Mbowe ulitengenezwa na utaendelea kukomaa kutokana na hawa wenyewe Mbowe na Zitto kutokukaa wakafikiria kwa nini wao ndio wamekuwa chimbuko na haya yote!.. Naikumbuka sana Chadema ile ya Mbowe,Zitto na Slaa toka wakati Mbowe akigombea Urais na jinsi chama hiki kilivyoweza kutuvutia wasomi wengi na ajabu ni kwamba sisi tulokuwa mjini tulijua linalokuja, tukawatahadharisha lakini wapi, leo Chadema kinakuwa kama chama cha wahuni tu.
Jamani mwee, cheo ni dhamana hakuna mwenye haki ya kuwa mwenyekiti, katibu wala mgombea Urais au Ubunge ni privilege kwa sababu HAKI ya mtu haiwezi kuwa na masharti, Mgombea uenyekiti ana sifa zake ana masharti yake na kadhailika hivyo sio kila mtu anaweza kuwa mwenyekiti ama mgombea Urais. Wanachama na wajumbe ndio waamuzi na isifike wakati kamati kuu kujichukulia maamuzi juu ya uongozi wa chama hapo ndipo mlipoharibu na mkubali makosa. Mbowe na Zitto nyie ni majembe wenye sifa kubwa kwa uwezo wenu hizi habari za kuwagawa hazitamfaidisha mwananchi zaidi ya ushindi jkwa CCM.
Zitto na Mbowe nawaomba sana tena kwa unyenyekevu mkubwa acheni utoto, mrudi katika basics za Chadema ile ilowavuta wananchi pasipo mikwaruzano ya ndani. Kila mmoja wenu ana nafasi yake ktk Ujenzi wa Taifa letu na nitasema tena Mbowe ni kiongozi mzuri sana anajua namna ya ku mobilize watu, ana Charisma ambayo ni kipaji alichopewa na Mungu kisiasa na wala hana mfano isipokuwa hawezi kuwa rais wa nchi hii. Hilo lazima alikubali kutokana na muda,
Naye Zitto hawezi kuwa kiongozi wa chama kutokana na watu wengi kutomuamini hata iwe kwa kiapo maana fitna ilishajengwa miongoni mwao, lakini Zitto anaweza kuwa rais mzuri na tegemeo la wananchi kuliko wagombea wote walokwisha jitokeza ama tunaowaona kutokana na moja kubwa kuwa Zitto ana VISION ya Tanzania ya kesho! anayajua mapungufu yote ya uongozi nchini, anajua umaskini wetu kiuchumi kwa sababu anajiweka karibu na wananchi (wakulima na Wafanyakazi). Huyu ni mfano bora wa rais mtarajiwa anazo sifa kwa madogo aloweza kuyafanya.
Mpende, msipende maelezo yangu lakini huu ndio ukweli ambao watu wengi wametumiwa kukivuruga chama na hamkuyaona isipokuwa pale ilipofikia wakati wa mabadiliko. Zitto asingeweza kushnda uchaguzi wa Chadema na wala hapakuwa na haja wala sababu ya kuogopa mageuzi kwa sababu lengo lilikuwa zuri ili chama kiwe na mwelekeo, leo hii Chadema haijulikani inafuata itikadi gani zaidi ya kwamba chama kinashirikishwa kuuvunja Muungano!
Maasalaaam..