CHADEMA sasa yamvuruga Zitto ACT-Tanzania

CHADEMA sasa yamvuruga Zitto ACT-Tanzania

Zitto ni mwasiasa wa pekee anayeendana na CHADEMA. Wamalize tofauti zao uchaguzi wa mwaka huu aungurumishe ndani ya CHADEMA.


BP

Aende zake kwenye genge lake la wasaliti linalovurugana kwa sababu ya mgao wa pesa ya escrow
 
mimi niliwahi kusema kuwa chadema hawawezi kusimama wenyewe bila zitto ndiyo maana wanafanya vitimbi ili arudi japo zitto naye hewa kabisa.

Mwambieni afute kesi aone! Cdm hatuwezi kufuga popo kama yeye.kama mnampenda mshaurini vizuri acheni kumpotosha,cdm hahitajiki na ndio maana kwa sasa chama kimetulia baada ya kuwafurumusha wasaka tonge na mamluki kama yeye.
 
chadema ni chama cha ajabu sana kazi yao kuvuruga wenzao japo zitto naye hata akivurugwa sawa tu maana ni mpuuzi tu,kwanza mwizi na mla rushwa wa kwanza.

wewe ni ME au KE maana haueleweki
 
mkuu mimi nadhani zitto acha avurugwe tu kazidi upuuzi juzi bungeni kupitia kamati ya PAC wamehongwa hela na mengi wamekuja kutupotosha kwa kutetea rushwa walizokula.

Jambo lingine baya zaidi zitto anapenda sana ushirikina mtu kama huyo hafai kwenye jamii yenye kumuamini mungu kama yetu akae kwa shetani na michadema yao pamoja na ICT yote majuha tu.
na wewe umevurugwa siyo bure!
 
Nadhani kunakukengeuka hapa,Hivi kati ya Mwigamba na Limbu ni nani wakuja pale ACT??

Mwigamba ameenda pale ACT amewakuta kina Limbu,Mahona na Nyakarungu. Wawezaje basi kudai eti Limbu anatumiwa na Chadema kuiteketeza ACT? Maana kilichowazi ni kwamba Mwigamba,Kitila,Zitto walikwisha wahi kufanya kazi na Chadema hivyo ni rahisi kusema Chadema inawatumia wao (kina Mwigamba) kuivuruga Act, wao wanadaije basi kwamba Chadema inawatumia kina Limbu??

Huu ni upunguani wa watu waelewa..!!! Kina Mwigamba watoke wakaanzishe chama chao na wasitake kuwavuga wenye chama ktk malengo waliojiundia tena waache kabisa kuihusisha Chadema na mipango yao ya kishetani. Kaeni kushoto vima nyie.. eti Chadema, Chadema.... pambafu..!!! mlijua kukikuza chama kufikia hadhi iliyonayo Chadema leo ni kazi ndigo kama kuvua Migebuka sio..!!!!????

BACK TANGANYIKA
 
utamaliza vipi tofauti zenu na mtu aliyeanzisha chama kipya kwa hasira?

kimsingi zitto hajajitokeza hadharani na kukiri kam yy ndiyebkaasisi ACT zilizopo ni allegations tu. kwani ni nani ndani ya cdm hana makosa? cdm hadi kufika hapo ilipo imepitia dhoruba nyingi kuliko hiyo issue ya zitto.nikwanini wasikae wakamaliza tofauti zao?
 
Kwani ZITTO ni muhusika kwenye ACT?
 
mkuu mimi nadhani zitto acha avurugwe tu kazidi upuuzi juzi bungeni kupitia kamati ya PAC wamehongwa hela na mengi wamekuja kutupotosha kwa kutetea rushwa walizokula.

Jambo lingine baya zaidi zitto anapenda sana ushirikina mtu kama huyo hafai kwenye jamii yenye kumuamini mungu kama yetu akae kwa shetani na michadema yao pamoja na ICT yote majuha tu.

Kumbe zzk ni mshirikina!
Umemjuaje au wewe pia ni mtu wa imani hizo?
 
mimi niliwahi kusema kuwa chadema hawawezi kusimama wenyewe bila zitto ndiyo maana wanafanya vitimbi ili arudi japo zitto naye hewa kabisa.

We kanga moko njoo hivyohivyo ulivyo (uchi).!!

Kuja hapa na Matokeo ya uchaguzi serikali za mitaa mwaka 2009 wakati Zitto yupo, Then njoo tena na matokeo ya serikali za mitaa mwaka 2014 wakati Zitto anashikilia kadi ya Mahakama. Halafu njoo tena na Matokeo serikali za mitaa yakihusisha ACT, Kisha tuambie nani AMEANGUKA nani AMEINAMA na nani AMELALA...!!!

Unajichetua chetua tu hapa huku mwenzio kashikilia kadi ya CHADEMA kwa Mikono ya mahakama..!! We unakuja hapa huku umebana pua.....(..Nilisema Chadema...Nyambafu..!!)

Hatuoi wanaume hapa.

BACK TANGANYIKA
 
Hakika Zitto ni Kirusi ijapokuwa nimempenda kazi ya kuwamaliza maswi, Muhongo na wale waliohusika kukwapua ESCROW
 
hahahahahahahhahahah....Kitila na Mwigamba united

Watu hovyooooooo

Badala ya kushughulikia issues mnahangaika na CHADEMA

chadema haina mda mchafu...ina deal na wezi CCM sio nyie vibaraka wa CCM
 
Mimi nadhani kwa vile hawa akina Mwigamba inaonekana ni non-compatible CHADEMA na sasa ACT, ni busara kwao kujikusanya na kuanzisha chama chao kuliko kwenda kwenye vyama ambavyo wengine wamevianzisha, halafu baadaye wanaanza kuwatuhumu waliovianzisha kwa kashfa za kijinga za kuihusisha CHADEMA.

Mwigamba, Kitila, Zito and the like, waanzishe chama chao. Chama ambacho kitaongozwa na wasomi, wasafi, wawazi na wenye upeo usio na kikomo kuliko kung'ang'ania kwenye vyama ambavyo vilianzishwa na wasio na elimu.

CHADEMA walisema MBOWE hana elimu kama wao (wakasahau kuwa kusoma hakuhesabiwi kwa idadi ya miaka ya kukaa darasani), na hivyo hastahili kuongoza chama (cha ajabu hawasemi kama alistahili au hakustahili kushiriki kuanzisha chama); wakaenda ACT wakijistanabaisha kuwa wao wana maono na upeo wa pekee, na tanzania watashuhudia kupaa kwa ACT lakini kwenda kwao ACT kumesababisha ACT kusonga mbele kwa algorithmic motion.
 
Tutafahamu malengo halisi ya ACT,muda mchache tu umebaki.Waachwe wafunguke vizuri.
 
kama mnaona hafai mwacheni akafanye siasa anapo ona panafaa
acha upotashaji jamaa yangu, hakuna alie mzuia kufanya siasa nje ya cdm, yeye mwenyewe ndio king'ang'anizi, kwani hujui kuwa amefungia kesi kuzuia uanachama wake, au unajichetua tu maksudi
 
mkuu mimi nadhani zitto acha avurugwe tu kazidi upuuzi juzi bungeni kupitia kamati ya PAC wamehongwa hela na mengi wamekuja kutupotosha kwa kutetea rushwa walizokula.

Jambo lingine baya zaidi zitto anapenda sana ushirikina mtu kama huyo hafai kwenye jamii yenye kumuamini mungu kama yetu akae kwa shetani na michadema yao pamoja na ICT yote majuha tu.

Nyie MAGAMBA mtakoma mwaka huu ; mnafikiri Zitto ni rahisi kama tikiti maji! Zitto ni level nyingine! Zitto sio rahisi kummaliza kama mlivyo mmaliza Amina Chifupa, muulize Ben Saa8, magudulia ya sum.u ameamua kuya-park stoo baada ya ku-prove failure kummaliza Zito.
 
chadema haiwezi kuwa salama kwa kuendelea kuhangaika na kummaliza zitto, kama chama kikuu cha upinzania kinapaswa kutambua kuwa habari za migogoro yake na zitto yamesha pita hivyo wajikite ktk uchaguzi mkuu ujao. viongoz wenye upeo mdogo wa kufikiri hupoteza muda katika kutafuta ushindi ktk mambo yasiyo na maslai ya taifa kusambaratisha ACT has nothing to do with the prosperity of this country. by the way zama tulizo nazo si za kuangalia chama bali utashi wa mtu binafsi wa kutatua matatizo ya wananchi. hata zitto awe mbaya kiasi gani bado taifa hili na wanakigoma wanamuhitaji kuliko walivyo wahi kumuhitaji huko nyuma.Umuhimu wa zitto katika taifa hili ni mkubwa kuliko mbunge yeyote wa chadema, hili ni dhahili kutokana na historia na mambo aliyo wahi kuyafanya kwa taifa.usaliti wake kama kweli upo hauwezi kuondoa umuhimu wake katika kutetea maslahi ya wanyonge. Viongoz wa chadema wanafanya yote hayo kwa maslai ya chama, hii inafaida gani kwetu...........
 
Inakuwa vp Mwigamba anasema kuwa ukitaka kuimaliza ACT ndio unakuwa unamkomoa Zitto -ambaye ni mwanachama wa chama kingine yaani Chadema?
 
Back
Top Bottom