CHADEMA sasa Tishio GEITA

Chadema ni chama cha kikanda,kikristo,kichagga.
Mara chadema ni cha msimu
mara chadema kitakufa mwaka mmoja ujao -wasira
 
MIKUTANO ya vuguvugu la mabadiliko (M4C) inayoongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imetikisa Jimbo la Busanda, wilayani Geita, mkoani Geita, baada ya wanachama 18,670 wakiwamo wazee na makada wa siku nyingi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutimkia CHADEMA.
Mbali na kuzoa maelfu ya wanachama, pia chama hicho kimeunda uongozi kwa kuteua wenyeviti, makatibu, na wahazini wa chama kwenye kila kata zilizokuwa hazina uongozi ngazi ya tawi.
Viongozi waliosimikwa ni wenyeviti, makatibu, wenezi na wahazini wa matawi pamoja na wale wa jumuiya mbalimbali za chama hicho hususan wazee (BAWAWACHA), Vijana (BAVICHA) na Wanawake (BAWACHA), lengo likiwa ni kukiimarisha chama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake kwenye jimbo hilo juzi, Kiongozi wa M4C mkoani Geita, Alphonce Mawazo, alisema wana CCM waliojiunga na chama hicho ni kutoka kata 13 kati ya 16 za jimbo hilo.
Alisema kati yao 11,235 ni wanachama wapya na 7,435 ni waliovua gamba na kuvaa gwanda, ili kuhakikisha CHADEMA kinaibwaga CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kuingia Ikulu.
Aliwataja miongoni mwa wazee na makada wa siku nyingi wa CCM waliorudisha kadi za CCM ni Thereza Lugembe (79) mkazi wa Kijiji cha Nyabulolo, Kwando Maduhu (109) mkazi wa Kijiji cha Nyarugusu na Shija Mihambo (87) mkazi wa Bugogo Bukoli ambaye alikuwa mwanachama wa CCM tangu Julai 7, mwaka 1979 kwa kadi namba C.812836.
“Kazi hii si ndogo…tunapambana na chama ambacho kina mizizi kila kona…tumezoea kuona vijana ndio wanajiunga na CHADEMA…lakini unapoona wazee nao wameanza kukimbia ujue saa ya ukombozi imekaribia,” alisema Mawazo.


Source:Tanzania Daima

geita kuna mwamko mkubwa wa kisiasa.pale kijijin nyamalimbe wanakijiji wanajua maana ya vyama ving na mchango wake kisiasa.hongereni makamanda
 
dAH chadema inatisha balaa,,,kuna mahali niko huku mashariki ya mbali, gumzo ni CHADEMA tu! peoples power!
 
Hiv kwann habar nyng za casa source ni tz daima?Are you advertising this or?Nimesusa nunua gazet lolote since wamefungia mwanahalisi!!
 
Ukiangalia kwa makini vidole vimeelekea kaskazini why?

kaskazini ipo juu sijawahi kusikia kibla ipo kusini cdm always up up ....angalia lini uliona jembe na nyundo ikianangalia juu litalima shamba gani?

 
mikutano ya vuguvugu la mabadiliko (m4c) inayoongozwa na chama cha demokrasia na maendeleo (chadema), imetikisa jimbo la busanda, wilayani geita, mkoani geita, baada ya wanachama 18,670 wakiwamo wazee na makada wa siku nyingi wa chama cha mapinduzi (ccm) kutimkia chadema.
Mbali na kuzoa maelfu ya wanachama, pia chama hicho kimeunda uongozi kwa kuteua wenyeviti, makatibu, na wahazini wa chama kwenye kila kata zilizokuwa hazina uongozi ngazi ya tawi.
Viongozi waliosimikwa ni wenyeviti, makatibu, wenezi na wahazini wa matawi pamoja na wale wa jumuiya mbalimbali za chama hicho hususan wazee (bawawacha), vijana (bavicha) na wanawake (bawacha), lengo likiwa ni kukiimarisha chama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake kwenye jimbo hilo juzi, kiongozi wa m4c mkoani geita, alphonce mawazo, alisema wana ccm waliojiunga na chama hicho ni kutoka kata 13 kati ya 16 za jimbo hilo.
Alisema kati yao 11,235 ni wanachama wapya na 7,435 ni waliovua gamba na kuvaa gwanda, ili kuhakikisha chadema kinaibwaga ccm kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kuingia ikulu.
Aliwataja miongoni mwa wazee na makada wa siku nyingi wa ccm waliorudisha kadi za ccm ni thereza lugembe (79) mkazi wa kijiji cha nyabulolo, kwando maduhu (109) mkazi wa kijiji cha nyarugusu na shija mihambo (87) mkazi wa bugogo bukoli ambaye alikuwa mwanachama wa ccm tangu julai 7, mwaka 1979 kwa kadi namba c.812836.
“kazi hii si ndogo…tunapambana na chama ambacho kina mizizi kila kona…tumezoea kuona vijana ndio wanajiunga na chadema…lakini unapoona wazee nao wameanza kukimbia ujue saa ya ukombozi imekaribia,” alisema mawazo.


Source:tanzania daima

ccm rest in hell.
 
kwuikwikwikwiwkiksema mimi usiwaweke wenye akili zao
huogopi hiii kwikwikwikwiwk pole sana
attachment.php

Raha tupu, uliona jeneza likapambwa na rangi za chadema? Jeneza hupambwa na rangi za Taifa na hata maiti hupambwa, Wakiristo kwa suti kuliko aliyoolea na Waislaam kwa sanda yenye manukato ya miski na al oud.
 
Back
Top Bottom