nasdaz naungamkono bandiko lako hapo kwa mara ya kwanza naomba nikubaliane na wewe kuwa chadema bado haijafanya bidii ya kujitangaza huko na siku ikifanya hivyo naamini itakuwa na wafuasi tena wengi tu..
Hiyo ni ONE STEP FOWARD kwavile umeuona ukweli ambao wengine hawataki kuukubali!!!! Nakumbuka mwaka jana alikuja ndugu yangu kutoka bush (ndiko nilikosema ni miongoni mwa vijiji vikubwa kabisa).....dogo kila unachoongea nae ni CUF! CUF! CUF! kimsingi, hataki hata kuisikia hiyo CCM. Nikamuuliza kuhusu CDM, akasema hakuna kabisa CDM kule....kwakweli nilikuwa very disappointed. Na labda nikupe siri leo hii; wakati huo nilikuwa naifagilia sana CDM ingawaje kwa sasa lazima nikiri kwamba SIIPENDI!!!! Nikapata nafasi ya kwenda kule; nikayashuhudia kwa macho yangu niliyoambiwa na yule dogo; ikaniuma sana kwamba chama kama CDM hakipo kabisa kule. Nikaja hapa jamvini na kutoa angalizo ni namna gani CDM wanaweza kujitanua na maeneo mengine.....nilitumia maneno kwamba, POLITICS is almost like ujasiriamali; kwamba penye matatizo kuna political opportunity kwavile ni rahisi kuwaambia wananchi kwamba....mnaona hii, ni kwa sababu ya hawa watu!!!! Wasiopenda kukubali ukweli na kuamini ktk dhahania wakaishia kukandia kwamba watu wa pwani na kusini hawajasoma ndio maana hawajui chochote badala ya kujadili mada husika....nikaja kuwa completely disappointed pale Slaa alipoenda kwenye kampeni za urais.....alitumia just couple of hours kwa mikoa miwili; tena ni kama tu alienda kutoa lawama...hapo ndipo nikaja fahamu kwamba; ehee, kumbe jamaa (CDM) si wenzetu!!!! Huwezi kukaa pamoja na watu msioongea lugha moja, nikaamua kuchana na wana magwanda!!!!