Mods hebu wekeni hili debe pembeni kwanza kwa mwezi mzima maana linapika kelele mno ni tu na lina distruct kwa kweli .
Ndugu yangu Linyungu mbona unapanda Temperature. Tena uko juu chini, ni dakika chache tu zilizopita ulinialika kirafiki katika Thread nyingine, ukidai mnanisubiri. Uliandika hivi... #79
"Kuna mada huku tunakutafuta acha utumbo huku njoo pale onyesha kama unaweza kuaminika .Acha unusu akili na kutawaliwa kwa masaburi" Nilifikiri tutajibizana hoja kwa hoja..... Mara leo unapeleka maombi kwa Mod nifungiwe mwezi mmoja.
Ninachoamini mimi ni kwamba CHADEMA ni chama kinachokuwa kwa nguvu ya soda kwa sababu Propaganda inazotoa kamwe haitaweza kuzitekeleza. Ni nini adhma ya chama kama hicho.. wananchi kukatishwa tamaa na chama hicho na kukikimbia na kuhamia vyama visemavyo ukweli japo unauma. Na kwa historia ya Tanzania CHADEMA si chama cha kwanza kukua kwa nguvu ya soda, vipo vyama vilivyoanzishwa na Mrema kweli nilijua kuwa sasa tumepata mkombozi. Lakini mkombozi akawa mkimbizi na hali hiyo inanukia CHADEMA.
Tanzania si nchi pekee ya Afrika ambayo ni masikini na wala si nchi pekee Afrika yenye rasilimali nyingi, lakini tukija kwenye umasikini wote letu ni moja. Umeyasikia ya Swaziland, sijakwambia ya Zaire, Liberia , Siera leone n.k. Ninachotaka kusema ni kwamba adui mkuu wa umasikini Afrika ni mmoja, kama hatukukaa na kuambiana ukweli basi tutapiga kelele majukaani bila kuondoa umasikini ambae ndie mlengwa mkuu katika chaguzi zote.
Kwa hiyo naomba CHADEMA wajipange upya kama wanataka kushika Dola La Tanzania. Sitoruhusu kamwe kukiruhusu chama chochote kile kushika madaraka Tanzania kama hakiathibitisha kuwepo kwa amani nchini. Haka kaamani kadogo tulikonako ni muhimu sana kwangu kuliko kushabikiwa kuingia vitani eti kwa jina la kutoa umasikini. Nchi zote zilizoingia vitani Afrika, mwananchi wa kawaida bado hajaona faida yake baada ya vita kwisha na Tanzania sio Exceptional. Chukulia LIberia na Siera Leon kama mfano.
Hivyo ndivyo ninavyoamini mimi Zawadi Ngoda, sitaki kajumba kangu kaUdongo kabomolewe kwa vurugu zenu na ndio maana nimeshikia bango hoja. Hiyo ndio silaha yangu pekee. Kama unataka nifungiwe kwa hilo OK.