CHADEMA ni "professional"

CHADEMA ni "professional"

Ivi CHADEMA si ndio waleee Mnaowaita CUF ,CCM B, na Mnauhakika hawa CUF kupitia UKAWA wana lengo moja . ( mfumo wa serikali ,nao CUF wanasupport Serikali tatu au!??

cdm ni chama cha kisasa mno ! Kinaenda na wakati sana zaidi ya mno ! UKAWA oyee !
 
Alafu kumbe leo hata katiba yetu inatambua shirikisho sema CCM wenyewe ndo hawaelewi hilo wao wanadhani ni serikali 2 kumbe ni 3 japo si rasmi

KWA NIABA ya FAMILIA YANGU YA HAPA TANDIKA MWEMBEYANGA , NAKUSHUKURU SANA .
 
Jambo moja ambalo ni la kushangaza ni kwamba CDM wamekuwa ni watu wa siasa za matukio, hawana msimamo hususani katika sera za chama chao,mf CDM na vyama vya upinzani ndio waliokuwa watu wa kwanza kuishutumu tume ya katiba kwamba imechaguliwa na mwenyekiti wa CCM hivyo itawakilisha maslahi ya CCM, leo CDM na washirika wake ndio wamekuwa watu wa kumtukuza Jaji warioba kwamba ni mtu asiyestahiki kupingwa kwa jambo lolote ! lakini walisahau kwamba wao hawakulioni hilo mwanzo wakati Rais amemteua Warioba kuwa mwenyekiti.

Sasa huu kama sio unafiki ni nini? ina maana CDM wapo kupinga jambo lolote ambalo CCM watalisema hata kama ni jema kiasi gani, vipi jaji walioba anaonekana shujaa wakati kina LISU na wenzake waliikosoa sana tume hii?

FUNGUA AKILI MJOMBA , ZILE KELELE ZA AWALI NDIYO ZIMEMFANYA WARIOBA AAMUE LIWALO na LIWE ! WANANCHI KWANZA CCM BAADAYE .
 
Watu wanashabikia serikali 3 kwakuwa tu Chadema inataka, always Chadema wako against na CCM! Ingekuwa CCM inataka serikali 3 Chadema wangetaka 2! Hawana sababu, Leo lao ni kuungana ili wachukue nchi maana Chadema Zanzibar haikubariki, Chadema iko kupotosha wananchi tu, viongozi wake wameshindwa kukiendesha chama itakuwa nchi? Chadema haina nguvu tena ndiyo maana wameamua kuungana na vyama peke yao hawawezi! Na Chadema ndiyo kiko mwishoni, na msitegemee serikali 3 hakuna kitu kama hicho.
Wewe unaesema tusitarajie serikali 3 ni mbili tu tambua hizo mbili hazitadumu na ndio zitakazopelekea muungano kufa kabisa kwani hizo 2 ndio zilizopo sasa na Muungano upo kama jina lakini kivitendo haupo kwani Zanzibar wanaishi wakiwa katika nchi yao kamili kwa kila kitu.
 
Wabunge,Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba na viongozi wa CHADEMA wanastahili sifa. Katika masahi ya Taifa,wako tayari kuungana na yeyote popote ili mradi tu maslahi ya Taifa yanalindwa na kutetewa. Wanaweza kushirikiana na mwanasiasa,mwanazuoni,mwanaharakati,mpendanchi na mzalendo yeyote na katika wakati wowote.

Wapo wanaoshangazwa na CHADEMA sasa kushirikiana na CUF na NCCR-Mageuzi katika kutetea Katiba mpya yenye masahi kwa wananchi wote.Wapo katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). Pamoja na kuwa kila chama kilichopo UKAWA kila sera na malengo yake,tofauti zao zimewekwa kando kwa muda huu wa kuitafuta Katiba mpya. UKAWA wameivana na kuelewana kama waliotoka chama kimoja.

Wanasiasa wanapaswa kujifunza kwa CHADEMA.Wanapaswa kujua kuwa siasa ni hoja za wakati fulani ambazo si lazima zifanane kila uchao. Siasa ni mazingira na namna ya kujenga mantiki kutokana na mazingira yaliyopo. Siasa si kung'ang'ania jambo moja kwa muda wote eti tu kwasababu lina manufaa ya sasa. Vipi kuhusu baadaye?

Na wanasiasa wengine wangekuwa kama hawa wa CHADEMA,nchi hii ingekuwa mbali sana. Kila la kheri CHADEMA!


watu wenye uzalendo na nchi yao si unafi
 
Hata mpige zumari na matarumbeta CHADEMA imekwisha
Kumbe ww gamba ndo maana nlikua nashangaa kwenye ile mada .. Diaspora walikua wanatumia nguvu nyingi kukufafanulia vitu vidogo..
 
Kwi! Kwi! Kwiiii !!! Habari za ujiji mkuu , vipi ile ziara ya MH KINANA , inasemekana kabla ya ujio wake barabara zote zilipigwa deki !

kumba jamaa wa ujiji huyoo

Niliwahi ishi kwa miaka kama mitatu niwa nasoma Muungano primary school na baadae kigoma sekondary barabara zilikuwa mbili kutoka ujiji kwenda bandarini na kutoka mwandiga kwenda mwenga na haya yalikuwa ni maendelo ya takribani miaka (2003-1961)=42 year of development with CCM madarakani

kiwango cha lami ya mwandiga to kigoma mjini kilikuwa cha chini,nikiwa namaanisha baada ya kuweka viwango fulani vya moram sand na kushindilia huwa inamwagwa lami the kokoto ndogondogo by that time watu wa kigoma along that road walifurahi lakini kwa ukweli lami ilikuwa kwa kiwango cha chini sana

labda bosi anipatie upade ya kigoma .....................kwa maana anaipenda CCm na mdogo wake ACT may be there is a change
 
bange na viroba vimekuwehusha
Kumbe gamba sugu.. Ndo maana huwezi jenga hoja.. Ndo maana diaspora walikua wanapoteza muda wao kukufafanulia mambo madogo..ccm inaabishwa na ninyi ambao hamwezi kujenga hoja.. Ni kutukana tukana tu na kutoa mipasho..
 
Unachotaka kusema ni nini mbona hueleweki, kwa sasa kuna serikali mbili na nchi mbili, je unataka twendelee hivyo kuwa na serikali mbili, na kama ni nzuri mbona wanasema kuna kasoro, na je unazijua kasoro za muungano, ni pamoja na kuwa na serikali mbili hizo zikiwa na marais wawili mmoja wa Zanzibar na Wa Muungano, je wa Tanganyika yuko wapi hapo. Kumbuka tulipoungana tuliungana serikali mbili Tanganyika na Zanzibar na nchi hizo zikawa zinaitwa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, sasa ili la Zanzibar limetoka wapi, ina maana Tanzania Visiwani imepotea na kurudi Zanzibar JMT ikibeba kofia ya Tanganyika. Ukisema twendelee na status quo hiyo unatupeleka wapi?
Rais wa JMT hana madaraka Zanzibar na ndiyo maana akienda uko Rais ambaye ni amri jeshi mkuu anakaa chini na uku Rais wa Zanzibar anapokea Rais kama Amrijeshi mkuu, Rais hana mamlaka ya kuchagua Wakuu wa mikoa na Wilaya tena Zanzibar na hali katiba ya inamruhusu na ya Zanzibar ikimkataza, Wana wizara ya ambazo ziko Zanzibar na si za muungano lakini bado Wazanzibar wanakuwa mawaziri kwenye wizara zisizo za Muungano mfano wizara ya Afya, unakuta wabunge wa Zanzibar wanachangia kwenye bajeti hata wizara ambazo haziwahusu. Sasa wewe unayetaka serikali mbili bado unataka haya yaendelee tu. yapo mambo mengi ambayo ni kero na bado unataka kero hizo ziendelee
- Muungano unatakiwa kurekebishwa sio kuuvunja kisa hamjawahi kupata kura Zanzibar ni wabaguzi wakubwa na wabinafsi wakubwa, kila uchaguzi mnashindwa halafu sasa kati kati ya mchezo mnataka kuhamisha magoli ili mshinde tu uchaguzi hatawezekana,

es
 
Kumbe ww gamba ndo maana nlikua nashangaa kwenye ile mada .. Diaspora walikua wanatumia nguvu nyingi kukufafanulia vitu vidogo..

Vitu gani nisivyovielewa kuhusu maisha ya diaspora? Nyie ndo msoelewa mada kazi kushupalia maneno ya khanga wanaume wazima
 
Hata mpige zumari na matarumbeta CHADEMA imekwisha

wenzio tunazungumza katiba wewe unatema hasira zako dhidi ya CHADEMA..tupe hoja zako jadidi tutakujibu...ukijielekeza katika kutafuta maarifa utayapata,,ila kama nia yako ni kuwa mtumwa wa fikra za wengine utaishia kuwa mfuasi na mtumwa wa hao wanaofikiria kwa niaba yako.....

hujachelewa karibu tutafakari kwa pamoja mustakabali mwema wa Tanzania tuikayo..kinyume chake utalazimika kutambulishwa sasa hata baadae kama binadamu uliyesimama upande usiyosahihi wa Historia ya nchi yetu..

wasalaaam
 
Vitu gani nisivyovielewa kuhusu maisha ya diaspora? Nyie ndo msoelewa mada kazi kushupalia maneno ya khanga wanaume wazima
Ni aibu kijana kuwa hivyo.. Labda kama ni mzee..lkn km kijana ujipange uwe na uwezo wa kujenga hoja
 
Back
Top Bottom