Chadema ni lini mtawachukulia hatua ma-radicals ndani ya chama chenu kama ANC walivyofanya?


Asante sana kwa kunikosoa mkuu.Mkuu wangu mkandara ninachoongelea kwenye mabadiliko ya fikra,ideologies na principles naongelea Mfumo.Ndiyo maana mara nyingi nikikosoa wazee wanapokemea vijana na kutaka tuendelee na status quo najikuta mara nyingi matatani hata hapa JF.

Mara nyingi nimekuwa nikijadili juu ya vijana kuaminiwa na kusikilizwa.Kama hautasikilizwa,ukatishwa kwa vyovyote ni njia ya kuziba vijana mdomo ili wasipambane na mfumo.Ndiyo maana nikiongelea radical reform watu wanapata shida kelewa.ni radical reform kiuchumi,kisiasa na kijamii.Na hizi haziwezi kuwa na maana kama hatutabadili fikra.kubadili fikra ni kufungua akili,ni kama maua yanayochanua kupokea kitu fulani.Hata katiba mpya ije kama hatutaendesha vita kali ya mapambano ya fikra bado tutageuka taifa la malumbano.tutaanza kulumbana juu ya katiba mpya badala ya kusugua fikra kujadili fursa zilizoletwa na katiba mpya

Mkuu wangu,ndiyo maana signature yangu na kaulimbiu yangu nikiwa nagombea uenyekiti wa BAVICHA ya MOVEMENT FOR RADICL CHANGE ilileta utata.Ni juu ya kufanya overhaul kisiasa,kiuchumi na kisiasa kwa kuanza na uhamasishaji wa kifikra zaidi.Nashukuru tunaelekea huko.Chama changu kimeanza sasa na movement for change.hii ni dhana pana kifalsafa

Mfumo tulio nao wa kisera ni wa kupeleka mambo kikawaida.Business as usual,hatuonyeshi kuwajibika kitaifa,hatuonyeshi kama ni watu wenye ambition duniani ukilinganisha na mataifa mengine.mfumo wetu zaidi ya facebook,twitter na google hautufanyi tuonekane kama tuko aware na kinachoendelea kwingine.tunaishi kama vyura bwawani tukidhani hiyo ndiyo dunia nzima kumbe kuna nchi kavu.
Msomi akiwa na digrii moja hawajibiki katika jamii inayomzunguka.haleti tofauti yoyote kifikra,kwetu elimu inatumika kama bastola ya kutishia watu.Hatujichanganyi na watu na kuambukiza fikra mpya bila majigambo.Ufisadi unaouona leo ni matokeo ya mfumo na ndiyo tunatakiwa tupambane nao.Kwa taifa ambitious huwezi kuona uthubutu wa serikali na makampuni ya kigeni yakikandamiza raia kama ninavyoshuhudia leo hii huku Geita

Leo hii hatuwaandai vijana kuwa na sauti au capacity ya kukosoa mfumo.wazee hawa walishindwa kufanya hivyo na sasa baadhi yao wanataka vijana ambao ni wazee wa baadae waendelee hivyo hivyo,yaani kilichobadilika ni kujua kuingia tu facebook,twitter,mavazi na mbwembwe kwenye harusi zetu na za marafiki.tunajenga taifa la ovyo.Sera ya kilimo kwa mfano hakuna kijana mwenye mwamko kwa kuwa amelelewa hivyo kimfumo.hajalelewa kuona fursa na kuwa aggressive.Mawazo yake hayaaminiki.Youths patriotic Movement inakuja kuongoza mapambano haya.Itakuwa kielelezo cha haya tunayopigania.Tunaandaa vision 2025 kupambana na vision 2030 ya washindani wetu kisiasa na kiuchumi ukanda huu wa Afrika mashariki (Kenya) huku wenzetu wakijitahidi kuweka mazingira ya kupambana na mfumo huku sisi tumweka Embargo.Kwa mazingira haya tutarajie fedheha huko baadae hapa A.Mashariki.Hiki ni kitu ambacho siko tayari kukiona nikiwa hai.hata sasa tumeshafikia alarming stage

Taifa hili na jamii unayoiona ni mfumo ulioandaliwa kuzuia ukosoaji,au kukinga fikra mpya za kupambana na mfumo.Tumekuwa taifa la kupambana na watu.Hata mimi kidogo niingie katika mtego wa kupambana na kundi la watu kama wazee kama nisingekuwa makini na baadhi ya wakuu kama ninyi kunikumbusha hapa
 
ujana ni kundi kubwa lenyeshauku ya kuona mabadilko chanya yanatokea katika nyanja zote za maisha yao ya kila siku na ya taifa kwa ujumla, laini kuna hatari km vijana kwa umri wao watajiona ndio wenye haki na wajibu wa kutenda , kufikiri na kuamua mustakabali wa jambo kubwa kama hatma ya taifa kwa kuwadharau na kuwatenga watu wa marika mengine katika jamii. vijana ni wazuri na wawe mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya udhalimu wowote katika nchi kwakushirikiana bega kwa begana kila anayejita mwananchi, aidha watu wa rika nyingine wanaweza kuwa wasanifu wazuri wa miango mingi tunayoiona ikisimamiwa nakutekelewa na vijana. nadhani ni vema tukajikita katika kuangalia changamoto zinazoikabili taifa na kuweka vigezo vya sifa kwa mtu tunayemtaka kuwa MUSA wetu kuelekea nchi tuliyoililia kama taifa. hebu tujikite katika kuyaangalia matatizo yetu zaidi na kuainissha sifa a uongozi tuanautaka ,halafu ndiyo kila autakaye ukuu ajipime kwa vigezo tunavyoviset kuliko kuanza kuwapa watu madaraka hata kabla ya vigezo kufuatwa. tukiri zaidi ya kigeo cha umri kuepukakujenga makundi kwatizamo ya umri!
 


Mkuu Kimbunga,

Wanachofanya akina Zuma ni mkakati wa kurahisisha kuchaguliwa tena.Wanajua akina Mbalula na Mothlate hawatapata access kwa Malema.Wanataka jamaa wasipate support yoyote ya kuonekana hadharani na JUJU ndiyo maana wamesizitiza jama hatakiwi kufanya mikutano,kuonekana kwenye mikutano ya ANC hata kama amealikwa. Tusubiri tuone mchakato wa Limpopo
 
mi nawashangaa watu wanamuona malema ni shujaa...na haswa haswa hawa pimbi wa cdm. mnajua malema ana mshahara wa $2000 kwa mwezi lakini anamiliki majumba ya kifahari na magari ya kifahari bil ya kua na biashara yeyote..huyu siyo mtu wa kumtumia kwenye propaganda za peoples power wala nini huyu malema anachoongea na anachofanya hayauwiani kabisa ni opportunist anachukulia advantage ya umaskini, economic and social frustrations za vijana huko SA kujifanya ni kamanda wa wanyonge wakati kila jioni anakunywa champagne na hao hao mabwanyenye anaowachukia...
 
Mkuu wangu nakusikia sana, hiyo Youth Patriotic Movement imekuwa kama Parapanda kwa vijana kama ilvyotokea wakati wa kupigania Uhuru, lakini hadi sasa ni kitu gani hasa mnachokiona tofauti na mnataka kukibadilisha vipi yaani mageuzi siku zote yanatoka mfumo badili kuleta ule unaowawezesha wengi kupata maisha bora zaidi..yaani tunatoka ule usiokubaliwa kwenda ule unaokubaliwa na wengi zaidi. Ni mageuzi yapi ambayo vijana mnataka kuyaleta na mnaona mnaweza kuyaleta kwa njia zipi..

Wakati wa Uhuru tulitaka kmwondoa Mkoloni na ikasomeka tunataka kuwafukuza wazungu japokuwa kulikuwa na ukweli kwamba huwezi kuondoa mfumo wa kukoloniwa pasipo kumwondoa mzungu mtawala.
1. Je, hii ndio moja ya msukumo unaozungumzia au ni mageuzi ya kuondokana na nini haswa?
2. Je, unaamini mfumo hasi sii wa chama CCM bali ni viongozi watu hasa wazee wanaotaka kuendelea kutawala kwa njia zile zile zilizopitwa na wakati ndani ya vyama na serikali.
3. Ni Taifa gani mnalotaka kulijenga ktk mageuzi haya..
- Nadhani inatosha kunipa picha..maana sioni ndani bado.
 

Man kwa hili umekuja kilimbukeni sana, kumbe ni mambo hizi ndo zinakusababisha ujikute unachugua upande mbovu wa historia namna hii, achana na maisha binafsi ya watu, wewe leta hoja na ukijibiwa usipanic namna hii.
Dah yani kumbe ni mambo hizi aisee? Usiwe emotional namna hii aisee.

 

:focus::focus:
 

Mkuu Ben, naona umetumia nguvu nyingi kumjibu mtu ambaye hajui hata anachozungumza.
By the way, umemsaidia huyu jamaa na vilaza wengine kufahamu kwa undani kuhusu hili jambo.
 
Gagnija,

Asante lakini Sina ubaguzi kama unavyosema,nikiongelea kuhusu changamoto zinazowakabili vijana ni ubaguzi?je nikisema vijana ni kundi muhimu kisiasa,kiuchumi na kijamii katika kuleta mageuzi katika nyanja hizo tatu nilizotaja ni ubaguzi?
UZee haukwepeki hata wewe utakukuta hivyo bac movement zako zisibebe ajenda ya ujana bali ukombozi wa pekee ambao utaletwa na makundi ya rika zote
 
Huyu Ben Sanane ni nani? Huko chadema anacheo gani? Ni mwajiriwa wa Chadema ama wa Taasisi gani? yeye siasa na movement zake anafanyia JF tu? Mbona hajaonekana Arumeru, Kirumba, Lizobon na Kiwira kwenye kampeni? Huyu Ben hasa ni nani?

Ukitafakari kwa makini Nuclear 1= Ben. huyu nuclear1 ni ben mwenyewe anaanzisha uzi na kuibuika kwa ID ya Ben na kuanza kufanya siasa na kueneza propaganda zake za kuwakashifu wazazi wetu kisa tu ni wazee anasahau kuwa uzee haukwepeki hata yeye utamkuta labda ajiue kuukwepa
 

Japo nakubaliana nawe kwa 65%,Napinga kwa 35%kuwa Zuma alishiriki kumsaliti Gaddafi
 
Mkandara,

Mie nilimshangaa Ben mara ya kwanza baada ya kusoma kuwa Shujaa wake ni Malema na Mugabe. Hapo mie ndipo nilichoka sana. Na ndiyo siasa anazotaka eti aziingize hata hapa Tanzania.

Hii haina tofauti na CCM kuwa Chama Cha Mapinduzi ila yepi?

Watu kama Ben ni watu ambao hawafai kabisa kuwa Majemadari vitani. Ni mtu ambaye anafikiri kujipeleka kichwakichwa kushambulia basi ndiyo njia sahihi. Nilishamueleza Waberoya huko nyuma kuwa Kagame na kundi zima la Watusi (Museven) ambalo lilianza kupigana vita ya Uganda na Tanzania, hawaendi vitani kabla ya kuwa na uhakika watashinda.

Nyerere angelimvamia kichwa kichwa Idi Amini, tungelitandikwa na morali ya wanajeshi ikafa. Ila walijipanga kwanza, wakaangalia mataifa makubwa wameelekeza wapi nguvu zao na macho yao. Nguvu ya adui ikoje na morali ya wanajeshi ikoje. Wakawapa mwezi mzima wafurahie ardhi ya Tanzania. Walipokuja kuwa na uhakika kuwa sasa wapo Fulumasinonda (Full machine in order) wakaingia kazini na kuimaliza. Na ndivyo walivyofanya Watusi huko Rwanda na Burundi.

Ben anataka kujenga ghorofa wakati hatujamuona hata kibanda cha kuku akijenga (kwa kumbukumbu zangu). Ajabu ni kuwa hawa vijana wote Radical, ukakamavu wao siku zote ni kutaka KUVULIA KWENYE TENGA. Kama kweli wanataka kufanya mabadiliko ya kweli, na wana nguvu kiasi hicho, si waanzishe chama chao na watu wawapigie kura?
Kwa nini Malema kama kweli ni Mbabe hivyo, asianzishe chama chake mwenyewe?

Ariel Shalon alikuwa mtu wa Likudi Party ila alipoona mambo hayaendi anavyotaka yeye, akaanzisha chake cha Kadima. hivi kwa nini na nyie msianzishe vyenu kama mnaona mnazibwa? Kwa nini Malema asianzishe chake kama huko mikoani wanamuona Mungu? Ila jibu ni rahisi sana, wavulia kwenye tenga utawajua. Congo nasikia wanasema "Mamba mjanja kumayi." Ndiyo maana hata Lowassa, ubabe wake wote upo ndani ya CCM, ukimtoa CCM basi anakuwa kama Mamba nchi kavu.

Kuwaondoa hawa viongozi wa Chadema kwa sasa wakati tupo vitani, itakuwa kichekesho na makosa makubwa sana. Ninatamani tupate viongozi kama Musa ambao watatuvusha Tanzania kufika kwenye Demokrasia ya kweli na kupata katiba mpya. Zaidi ya hivyo, kuhakikisha vyombo vya usalama vyote na Mahakama, vinakuwa huru na Bunge linakuwa na Wananchi kweli na siyo wahuni fulani kama huyu Kudadadeki au akina Shibuda na ndoto zao za posho. Yupo tayari kumlamba miguu Rais ili muradi na yeye wamkumbuke. Mtu analipwa kwa kujikomba kwake na siyo kwa kazi nzito anayoifanya.

Kama vijana wenyewe ndiyo hawa wanaoota tu uongozi ili na wao watumikiwe na chama na si wao wakitumikie basi kweli hatuna vijana. Na kama ukija pewa uongozi wowote ndani ya Chadema ukiwa na msimamo wako huo, basi Chadema wajuwe wamemkaribisha Malema ndani ya nyumba. Uzuri ni kuwa Chadema wana uthubutu wa kufukuza wanachama.

Tanzania si nchi inayopigania kumuondoa Mkoloni bali kubadilisha System na kuweka Demokrasia ya kweli. Huo ukali wenu sijui mnataka kumuondoa nani. Kwa hali tulipofikia sasa, kuna kila dalili Tanzania itabadilika bila ya kumwaga damu kama Wakenya, South Africa, Mali, Ghana nk. Funguka kijana na ubadili haraka mwenendo wako.
 

you are mixing a lot of things kutokana na emotional connection na Malema.... step back, think outside the box utaweka vizuri zaidi

we dont need to refer/learn anything from ANC, they learnt a lot from us via CCM na vyama vingine kiritimba ndani ya subsahara

You need to build your own case around tanzania context na hasa umuhimu wa mabadiliko fulani ndani ya chadema.......LAKINI BILA KUCHAFUANA KIJINGA

 
Mkuu kimbunga,

Hao wasikubabaishe maji yamewafika shingoni.......wanatafuta kuchafua watu kwa nguvu zote.saiasa za hoji hazifanyiki tena ukishaona watu wamefikia hatua hiyo.tuendelee na mjadala ,let us ignore them

Ben my bro

Kuna kitu kimekutokea hakiefanani na wewe, and sorry if i am wrong, Regia was a very good friend, she knew how to buffer your flights of idea!!!

You are really high these days...... i pray that you find some one to act like CPZ to your ambitious life

You are young, smart na able, but uko extravagant kwenye plans na very clumsy kwenye execution
 
This is so low

na kwa sheria za JF you deserve a permanent ban mkuu.... sidhani kama hao wengine kwenye hizo picha wanahusika kwa namna yoyote humu JF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…