CHADEMA ni kikundi cha waliokataliwa, kila siku hili kinazaliwa upya na kukua

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Kwa Afrika tunasoma wale wote waliopingana na serikali au waliokuwa na akili za kutisha nafasi za watawala waliitwa wasaliti, wahaini na viombe hatari kwa nchini. Juzi tumeona mjadala wa Bibi Titi Mohamed, aliposhindana na Mwalimu ndipo alipoitwa muhaini, tunamsoma Kambona, Maaalim Seif, na wengine. Wote hawa waliteseka si kwa sababu awakuitakia nchi mema bali watawala waliokuwepo walifika muda wakawaza kwa manufaa yao na awakutaka mwingine awaze sawasawa.

Lakini pia twende mashuleni na vyuoni, watu wengi wanaofukuzwa shule na vyuo ni wale wenye akili na maarifa ya kuhoji. Vyuoni viongoozi wengi wa mrengo wa kushoto ni wale wasiopenda kusema yes na mwisho wake uishia kufukuzwa vyuo Kama ilivyo kwa akina Sitta, Mnyika na wengine wa kariba hii. Waliohoji wakahojiwa na waliowahoji awakupenda majibu ya wahojiwa

Ipo faida kubwa yakuwa na kundi la waliokataliwa, hapa ndipo uzaliwa machinga, wanaharakati na makundi mengine ambayo kwa namna moja au nyingine kundi la watawala uwaona kama wasio na akili na wasio na mchango kwa Taifa. Lakini kinyume chake kundi hili ndilo uzalisha wazalendo na watu wenye hofu ya Mungu kuliko kundi la watawala ambalo uzalisha waoga na wanaoabudu madaraka na watoa madaraka.

CHADEMA inasumbua kwa sababu misingi yake mikuu nikuangaika na kundi la maskini na wale amabo jamii inawatumia na Kisha kuwadamp. Chadema ina kundi la watu wenye akili na uelewa mpana Sana, Chadema itaendelea kuzalisha Viongozi wengi wanaoaminika na kupewa madaraka makubwa nchi hii Sasa na huko tuendako. Chadema ilipofikia Sasa Ni chama ambacho Viongozi wa CCM kila wakikaa wanawaza Ni Nani wakamsajili ajiunge kwenda kuwasaidia. Kila Kiongozi anayetaka abembelezwe na kupewa ajira anajibanza Chadema na kuonyesha umairi wake Kisha wana CCM na dola wanafika kumrubuni na kumwahidi ajira, tumeoana ma DC na wabunge 19. Si Jambo dogo kutengeneza Viongozi wakwenda kusimamia miamba ya chama Tawala.

Leo hii Mbowe anachoombwa nikukubaliana na masharti ya usajili maana ameonekana Ni Kiongozi mahiri ambaye endapo atajiunga na CCM Basi atawasaidia kusonga mbele. Anatafutwa Lissu , Msigwa, Lema, Joseph, Mnyika, Mwalimu na watu wa karba hii wajiunge kukisaidia chama Tawala. Hawa wote niliowataja wapo kwenye kundi la kukataliwa na Wana uwezo, nguvu, hofu ya Mungu na akili za uongozi. Kwanini CCM isitengeneze watu wa haiana hii? Haiwezi kutengeneza kwa sababu asilimia kubwa ya Viongozi wao ni wakurithishana, wanapewa uongozi si kwa uwezo bali kwa sababu baba au mama au mjomba kasema mtoto apewe ajira. Wanapewa wapate mshahara na waweze kuishi.

Natumai ujio wa Bunge la Wananchi leo umeeonyesha kwamba Hawa watu Wana akili, wamesimama jukwaa la habari na vyombo vichache tu lakini wamekuwa agenda. Wanakwenda majimboni kukaa na wananchi wakati wabunge wa CCM wapo busy DSM, matokeo yake kero za wananchi zitazungumziwa na Wabunge wa Wananchi ambao awakuapishwa. Hapo ndipo utabaini kwamba Hawa watu Wana akili. Walitulia kwa mwaka Sasa na wamekuja na njia mbadala yakukimbiza mwizi, wakianza kuibua kero za wananchi huko majimboni lazima tutajikita kuwasajili na wao bila hiana watakubali madaraka waongezeke wawe wengi waweze kupigana ndani na nje kuelekea ukombozi.

Lakini akili nyingine kubwa Ni usajili wa kidigitali unaoendelea, Kwanza wanapata fedha, pili wanasajili watu amabao wanaumizwa na ugumu wa maisha. Ukiona mlala hoi anakubali kusajiliwa upinzani kwenye siasa Kama za Tanzania Basi Hali si shwari. Wananchi wanapanga foleni kuandikishwa, hii ndio akili ya waliokataliwa ambao Ni wengi nchini.

Mwisho, CCM msipokubali kulazimisha watu wenu wafanye siasa mkategemea Katibu mkuu na Katibu Mwenezi wanaweza kufanya kazi za siasa nchini mnajidanganya. Wananchi wanazidi kuibuliwa huko mashinani lazima mkubali kuwalazimisha watu wetu wafanye kazi ndipo wapewe promotion.
 
Bunge la Wananchi ni Kisiki Kikubwa Sana Ambacho CCM Hawakukitarajia.

Walidhani Kumuweka Ndani FAM ni Dawa.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kila Kiongozi anayetaka abembelezwe na kupewa ajira anajibanza Chadema na kuonyesha umairi wake Kisha wana CCM na dola wanafika kumrubuni na kumwahidi ajira
Hichi ulichosema ni kweli kabisa lakini Kuna cha kujifunza kuwa viongonzi wa namna hii ni hatari kwa mustakabali wa nchi maana kiuhalisia wanapigania maslahi yao binafsi zaidi ndio maana ya kujibanza chadema kwa lengo la kuonekana wapate ajira na sio kuwa na itikadi dhabiti katika kuwatumikia wananchi ie katabi, waitara, covid 29, Kafulila etc Je Sasa Hawa wanasimamia kile walichokua wanasimamia kabla?
 
Hilo bunge la wananchi litakuja kubadilisha upepo wa siasa za nchi hii; hii ni operation nyingine iliyokuja kwa mtindo mwingine.

Niliwahi kuandika baada ya madhila wanayofanyiwa Chadema na viongozi wa nchi hii ni vyema wakae chini waje na plan A+ naona wamenijibu.

Utekelezaji wa hayo maazimio ya hilo bunge utawarudisha Chadema karibu na wananchi, faida nyingine sitaki kuziandika hapa wacha zikaonekane field, ila kusema Chadema itakufa mtasubiri milele.
 
Hichi ulichosema ni kweli kabisa lakini Kuna cha kujifunza kuwa viongonzi wa namna hii ni hatari kwa mustakabali wa nchi maana kiuhalisia wanapigania maslahi yao binafsi zaidi ndio maana ya kujibanza chadema kwa lengo la kuonekana wapate ajira na sio kuwa na itikadi dhabiti katika kuwatumikia wananchi ie katabi, waitara, covid 29, Kafulila etc Je Sasa Hawa wanasimamia kile walichokua wanasimamia kabla?
Au Chama chenyewe (CHADEMA) na mbunge wake Aida Kenan, nini msimamo wao kuhusu uchaguzi wa 2020 na kuhusu ushindi wa mbunge Aida? Huyu mbunge Aida hayupo katika uongozi BAWACHA, BAVICHA na wala humsikii akizungumza chochote kuhusu katiba mpya, kesi ya Mbowe,kukamatwa kwa wanachama au akizungumziwa na viongozi wa chama nk hashiriki mijadala clubhouse au twitter spaces

Je, ni mbunge anayetambulika na chama au la?
 
Au Chama chenyewe (CHADEMA) na mbunge wake Aida Kenan, nini msimamo wao kuhusu uchaguzi wa 2020 na kuhusu ushindi wa mbunge Aida? Huyu mbunge Aida hayupo katika uongozi BAWACHA, BAVICHA na wala humsikii akizungumza chochote kuhusu katiba mpya, kesi ya Mbowe,kukamatwa kwa wanachama au akizungumziwa na viongozi wa chama nk hashiriki mijadala clubhouse au twitter spaces

Je, ni mbunge anayetambulika na chama au la?
Haitufanyi tusisonge mbele.agenda ya sasa ni bunge la wananchi na CHADEMA DIGITAL
 
Back
Top Bottom