Chadema ni kama timu ya mpira.......

5. Mizengo Pinda
6. Bernard Membe
7. Edward Lowassa
8. Andrew Chenge

mbona wewe mwenyewe hujajiweka?din tz haupo hizo danganya toto ya magambaz,hiv wanadai toto lako jiz nan anayetakiwa kumwadhibu?anenaye udin anufaika nao
 
Nimefurahishwa na kitu kimoja kwamba walau sasa demokrasia inakomaa Tanzania.Wananchi wamefumbuka na wanaelewa mbivu na mbichi.Wakati wa kudanganya watu umepita kwani vijana wanazidi kupata elimu ya uraia.
Niseme wazi kwa hapa ilipofikia ni vigumu Chadema kusambaratika.Ni kwa nini nasema hivyo.Nakumbuka miaka ile ya 90 wakati NCCR wakiwa na nguvu kubwa,pale role model alikuwa anaonekana mtu mmoja tu Augustine Lyatonga Mrema basi! Wafuasi wake walifanya chochote kisa Mrema kasema.Wafuasi wake walifikia kumbeba kama maiti!!!
Chadema ni tofauti sana.Hakuna mtu maarufu pale bali chama ndicho maarufu.Kama mwanademokrasia niwapongeze viongozi wa chadema kwa kuijenga chadema kama taasisi.Chadema leo anaweza kuondoka mtu yeyote na chama kikabaki imara sana.Angalieni mfano mdogo tu mauaji ya Nyamongo.Alienda kule Godbless Lema wanasiasa wakasema maneno mengi sana kwamba Lema anachochea vurugu kule,alivyoenda Marando na Tundu Lissu wakasema afadhali Lema kuliko hawa!!! Walisema Slaa asipokuwa bungeni chadema imekufa na wananchi hawatapata mtetezi tena walipoingia kina Mdee,Mnyika,Zitto,Lema na Wenje wakasema afadhali ya Slaa.Wakati wapiganaji wa chadema wakiwa bungeni huku nje Slaa anaongoza mashambulizi makali mikoani akiwa na akina Mpendazoe,Abdallah Safari,Marando,Mwita Mwikabe,Wilfred Lwakatare,Benson Kigaila na wengine siwamalizi kuwataja.
Hatimaye demokrasia imekua na ni vigumu sana kuimaliza Chadema..utamfunga nani uimalize nguvu? Labda wote uwapeleke gerezani kitu ambacho hakiwezekani.
Nimekosa la kusema ndio maana naiona Chadema kama timu maarufu ya mpira ya REAL MADRID.....

Niongeze kwa kusema kuwa ambae anaweza kubisha kwanza hana akili, hii ni timu tena timu ambayo inafundishwa na coach mwenye akili ka JOSE/HOZEE MOURINHO. Utafanyeje ili kuwavutia watanzania kuzikubali sera za ku-A.NGU.KA ZAIDI?
 
Huyu Jamaa aliye uchi na mwenye ngozi kama nguruwe anatakiwa kufungiwa (Ban) maana anachochangia humu hakiendani na habari yenyewe iliyowekwa mezani
 
5. Mizengo Pinda
6. Bernard Membe
7. Edward Lowassa
8. Andrew Chenge
Chadema kwani hakuna waislam? au kwa sababu hakuwataja?
12. Said Amour Arfi (makamu m/kiti bara, mbunge mpanda kati)
13. Said Issa Mohamed (makamu m/kiti Zanzibar)
14. Hamad Mussa Yusuph (Naibu katibu mkuu zanzibar)
15. Mustapha Bouay Akunay (mbunge Mbulu)

Hata hivyo chama kinakuwa na wanachama wengi katika maeneo kilipoanzia. wanachama huongezeka kutoka sehemu nyingine kadri ya kukubalika kwake. ikumbukwe CCM ilianzia pwani ya bahari ya hindi amako waishio wengi ni waislamu. kilisambaa nchi nzima na kupata viongozi wa dini na maeneo tofauti. CDM ndo ilivyo sasa inasambaa nchi nzima na kupata watu wa kila aina ya watanzania
 
Endelea tu kuota ndoto za mchana ! hii nchi haichukuliwi kwa maandamano au wingi wa watu mikutanoni, ni zaidi ya ufikiriavyo


Hilo tunalijua, usalama wa taifa, Katiba mbovu na Tume ya CCM ya Uchaguzi, ndivyo unavyomaanisha, hayo pia yatashugulikiwa usijali mkuu.
 
nimeipenda hiyo timu hata bila kocha bingwa (urais 2015) tunauchukua safiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
nakubaliana na wewe lakini:

mimi ningeshauri kwamba kwasababu leo chadema ni taasisi basi ingejigawa katika makundi mawili ya kudumu hadi 2015.

la kwanza ni wale ambao si wabunge ambao wataendelea kutuelimisha wananchi bila kujali kwamba kuna vikao vya bunge au la, hawa wapite kila kijiji wakutane na wananchi na kusikiliza kero zao, liongozwe na dkt slaa lakini wajigawe katika makundi zaidi ya moja.

la pili ni wale ambao ni wabunge, hawa watasaidia kuwakilisha zille kero zilizoibuliwa na kundi la kwanza pamoja na kuwaongezea nguvu kundi la kwanza wakati hakuna vikao vya bunge,
liongozwe na mbowe kama kawaida.

nimesema hivyo kwasababu nataka chaguzi za 2014 na 2015, kila mtu awe ameelewa maana ya kupiga kura na zaidi kuzilinda.

asante.
 
endelea tu kuota ndoto za mchana ! Hii nchi haichukuliwi kwa maandamano au wingi wa watu mikutanoni, ni zaidi ya ufikiriavyo
tatizo lenu mnadhani mnaakili sana. Chadema in wasomi wa kutosha tena vijana wanajua mambo mengi wala husitahili hata kuwa mashauli wao. Baki na akili fupi tu. Umati ndo watanzania wenyewe. Rejea misri na tunisia.
 
Sera gani mkuu??? Maandamano kila kukicha

Hayo hayo maandamano ndio yatakutoa madarakani baada ya wananchi kutambua haki zao na wewe na mshua wako mtarudisha vyote mlivyoiba sivyo tutawazika baharini sbb mmeshatulia maraia wetu kibao
 
Back
Top Bottom