CHADEMA ni Imara zaidi kuliko CCM

CHADEMA ni Imara zaidi kuliko CCM

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,176
Reaction score
48,460
Kuna siku niliuliza kama Mbowe anapaswa kuondoka kwenye nafasi yake ya Uenyekiti (itafika siku ataondoka tu) nani achukue nafasi yake. sijawahi kupata jibu. Lakini bado kila wakati likitoea jambo ndani ya CHADEMA lazima jina la Mbowe litajwe na kusemwa yanayotokea ni kwa kuwa yeye ni Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA.

Lakini uimara wa kitu hupimwa kutokana na mashambulizi ama majaribu inachokumbana nayo. CHADEMA tangu baada ya kujiuhisha (Rebranding) mwaka 2006 kimekuwa ni chama kinachopanda na kuoenesha uimara wa kupambana na matatizo yanayosababishwa na CCM pamoja na dola dhidi yake!

Kila likitokea jambo wapinzani wa CHADEMA hulifanya jambo hilo kama ni jipya na litaisambaratisha CHADEMA. Kama viongozi wa chama kutoka CHADEMA na kujiunga CCM wameshatoka hadi viongozi wa kitaifa na bado CHADEMA inasonga mbele.

Kwa ulinganifu CHADEMA ni chama Imara sana kuliko CCM kwa kuwa chenyewe kinafanya siasa bila ya kutegemea dola dhidi ya CCM ambayo bila ya kutegemea dola ni chama dhaifu sana kuliko hata TLP ya Mrema.
 
Hata mimi niliwahi kuwa kama wewe kushabikia huo upuuzi.

Mwanaume akianza kuweka makazi sehemu anajenga kabisa au kununua mali isiyoweza kuhamishika kirahisi ila kwenu Chadema hata nyumba hamna na bado mnajidai chama kikuu cha upinzani.

Jengeni nyumba mnatia aibu.
 
Kuna siku niliuliza kama Mbowe anapaswa kuondoka kwenye nafasi yake ya Uenyekiti (itafika siku ataondoka tu) nani achukue nafasi yake. sijawahi kupata jibu.
Jibu ni kwamba wanachadema wengi watapenda nafasi hii ichukuliwe na Lissu lkn mgogoro utaibuka pale Mbowe atapotaka kwa lazima kumrithisisha Lema
 
Chadema hata nyumba hamna na bado mnajidai chama kikuu cha upinzani.
Uimara wa chama unapimwa kwa kuwa na Jengo? Unajua kwamba TANU kabla ya kushika madaraka ya dola kilikuwa kinatumia majumba ya watu kwa ajili ya kazi za chama hicho. Unajua kwamba pamoja na majengo lukuki CCM waliyopora toka kwa watanzania wote chenyewe bado kinategemea kuchukua wanachama wa CHADEMA ili kujiimarisha!!?
 
Tulioshuhudia mapito ya NCCR ya Mkapa tunashuhudia the same thing kwa Chadema ya JPM...Tunachoshangaa ni majasiri kama nyie mnaoamini Chadema ni ile ile ....badala ya kushtuka na kuchukua hatua ....tuliomjua Lamwai hatukuamini siku moja atakwenda CCM ....
 
Hata mimi niliwahi kuwa kama wewe kushabikia huo upuuzi.

Mwanaume akianza kuweka makazi sehemu anajenga kabisa au kununua mali isiyoweza kuhamishika kirahisi ila kwenu Chadema hata nyumba hamna na bado mnajidai chama kikuu cha upinzani.

Jengeni nyumba mnatia aibu.
 
Tulioshuhudia mapito ya NCCR ya Mkapa tunashuhudia the same thing kwa Chadema ya JPM...Tunachoshangaa ni majasiri kama nyie mnaoamini Chadema ni ile ile ....badala ya kushtuka na kuchukua hatua ....tuliomjua Lamwai hatukuamini siku moja atakwenda CCM ....
Nyakati huwa hazifanani na wakati Lamwai anatoka NCCR kwenda CCM alionywa kamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wake hakuamini, leo unapotaja jina lake kwa wanasiasa wa sasa ni kama unataja jina la dawa ya kienyeji, HAWAMJUI.

Kuna mabandiko tumeandika humu kwamba viongozi wa CHADEMA wachukue hatua na tukipata nafasi ya kuwasiliana nao tunafanya hivyo. Lakini unadhani bila ya dola CCM ingekuwa na hata chembe ya nguvu ilizonazo leo CHADEMA? Mabadiliko ni jambo lisiloepukika na wana CHADEMA wengi sana tunatamani yatokee ndani ya chama lakini si kwa gharama zile zile zilizoua NCCR.
 
Chadema chini ya Mbowe ni imara mno, hata rais jiwe analijua hili ndio maana kwa hofu kubwa akapiga marufuku shughuli za vyama vya siasa kasoro chama chake kinyume kabisa na katiba ya nchi, anajua akiipa Chadema uhuru wa kufanya siasa zake kama matakwa ya katiba na sharia za nchi yalivyo hakika itakuwa aibu kwake yeye binafsi kama rais na chama chake
 
Write your reply...
Chadema ni Chama kubwa anayeondoka na aondoke hatuna jinsi.
Ila kila ZAma na kitabu chake kasema mzee Mwinyi.
Hata JKNyerere alikuwepo aliondoka.
Tenda mazuri kwa wakati wako Bwn Mungu atakurehemu muda ukifika!!
 
Kuna siku niliuliza kama Mbowe anapaswa kuondoka kwenye nafasi yake ya Uenyekiti (itafika siku ataondoka tu) nani achukue nafasi yake. sijawahi kupata jibu. Lakini bado kila wakati likitoea jambo ndani ya CHADEMA lazima jina la Mbowe litajwe na kusemwa yanayotokea ni kwa kuwa yeye ni Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA.

Lakini uimara wa kitu hupimwa kutokana na mashambulizi ama majaribu inachokumbana nayo. CHADEMA tangu baada ya kujiuhisha (Rebranding) mwaka 2006 kimekuwa ni chama kinachopanda na kuoenesha uimara wa kupambana na matatizo yanayosababishwa na CCM pamoja na dola dhidi yake!

Kila likitokea jambo wapinzani wa CHADEMA hulifanya jambo hilo kama ni jipya na litaisambaratisha CHADEMA. Kama viongozi wa chama kutoka CHADEMA na kujiunga CCM wameshatoka hadi viongozi wa kitaifa na bado CHADEMA inasonga mbele.

Kwa ulinganifu CHADEMA ni chama Imara sana kuliko CCM kwa kuwa chenyewe kinafanya siasa bila ya kutegemea dola dhidi ya CCM ambayo bila ya kutegemea dola ni chama dhaifu sana kuliko hata TLP ya Mrema.
Hakika umemalizia vema sana na uimara wa CHADEMA upo hapo, ila katika hesabu kuna matendo makuu mawili; (+) na ( -). Kama matukio ya hivi karibuni kwa CHADEMA yanaakisi kitendo cha (+), hatuhitaji kuwa na wasiwasi, ila kama yanaakisi (-) lazima tuendelee kutafakari. Matokeo ya kutoa, hudunisha, hupunguza, hudhohofisha, hufifisha na hatimae hupunguza nguvu kabisa, hivyo hufisha.

Njia ya kupunguza, sio muhimu sana, muhimu ni matokeo. Sikuwahi kumsikia Prof. Lipumba akikiri hadharani kudhohofika kwa CUF na hata Maalim hajasema hivyo. Tunasikia ni wahuni, ni njama, wasio itakia mema CUF. Sijawahi kusika Mzee Mrema akiri TLP haipo kiuhalisia, wala Mhe. James Mbatia anaamini NCCR inanguvu kuliko wakati mwingine wowote.

Tunahitaji kutafakari zaidi kuliko kuhutimisha kijanja kijanja haitatusaidia.
 
Uimara wa chama unapimwa kwa kuwa na Jengo? Unajua kwamba TANU kabla ya kushika madaraka ya dola kilikuwa kinatumia majumba ya watu kwa ajili ya kazi za chama hicho. Unajua kwamba pamoja na majengo lukuki CCM waliyopora toka kwa watanzania wote chenyewe bado kinategemea kuchukua wanachama wa CHADEMA ili kujiimarisha!!?
Hajui huyo mwambie TANU walikuwa wakitumia majumba ya watu wakati kikiwa ni TAA walitumia ukumbi was student center tabora ambao ni wakanisa Catholic for meeting acha kubaki karne ya 10 hii ni karne ya 21 mkuu
 
Hvi kuna watu bado wanaimani na chadema.....duh hii inanikumbusha vita ya US Vs Japan kule kwenye visiwa vya pacific... japan ilikuwa inachezea kichapo kizito pote katk visiwa vya Philippine, midway, guadiucanal, Saipan, Iwo jima na Okinawa lakn bado Japanese walijitoa ufahamu wakijiaminisha kuwa wanaweza kushinda mwisho wa Siku walijikuta wanapoteza roho za askar na raia wapato 2.5ml....ndo yatakayoikuta chadema
 
Chadema chini ya Mbowe ni imara mno, hata rais jiwe analijua hili ndio maana kwa hofu kubwa akapiga marufuku shughuli za vyama vya siasa kasoro chama chake kinyume kabisa na katiba ya nchi, anajua akiipa Chadema uhuru wa kufanya siasa zake kama matakwa ya katiba na sharia za nchi yalivyo hakika itakuwa aibu kwake yeye binafsi kama rais na chama chake
Chadema kama hawana tatizo vile, wakati wanachama wanazidi kukimbia!
 
Attachments

  • IMG-20180728-WA0042.jpg
    IMG-20180728-WA0042.jpg
    28 KB · Views: 31
Write your reply...

Kuhonga watu vitu na kuwapa vyeo sio dalili nzuri ya taifa adilifu.
CHADEMA Ina wanachama na mashabiki wengi ila watu wana busara na hekima, sio mambumbu mbumbu.
Taratibu ndio mwendo.
Lakini Mungu hafurahishwi na wauwaji!!
 
Back
Top Bottom