CHADEMA ni akina nani?

mkuu nadhani ungeomba sera za vyama uzisome kisha upime na kuchanganya na akili zako
 
Ndugu wana JF

Ninahitaji kujiunga na chama cha siasa hapa kwetu. Lakini, kabla sijafanya maamuzi ni chama kipi nijiunge nacho, inanibidi nitizame nyuma ya pazia la kila chama cha siasa hapa nchini "lifting of the vail".

1. Nilipofunua pazia la TLP na NCCR-Mageuzi, nikamkuta Mh. Lyatonga Mrema, n.k

2. Pazia la CCM: Niwewakuta waasisi akina Baba wa Taifa, Mzee Karume, n.k

3. C.U.F nimewakuta akina Prof, n.k

4. Naomba kujua ni nani na wako wapi waasisi wa CHADEMA?

Nisaidieni, maana ninataka kujiunga na chama cha siasa haraka iwezekanavyo

Unajiunga na chama kwa kuangalia itikadi au sura za watu?
 
Chadema ni mijibaba yenye miraba minne, yenye fedha na mali, akili na utashi inayotaka kutawala nji hii mwaka 2015 kwa nguvu za aina yoyote baada ya CCM kushindwa kuvua gamba. Period
 
Shukrani kwa wote waliochangia.

Inapoitaja CUF, huwezi acha kumtaja Prof. I. Lipumba, Seif Sharif, n.k

Unapoitaja UDP, hakika huwezi acha kumtaja Mzee J. Cheyo, n.k

Unapoigusa CCM, lazima uanze na TANU + Afroshiraz, na waasisi wake kama Baba wa Taifa, Kawawa, Bibi Titi, Karume, Seti Benjamin, n.k

Kwanini, hamuokenani kukubali kutizama nyuma ya pazia la CDM.

"Tell me your friend, and will tell you................"
Jee ukitazama (red) ndio utapata picha halisi ya hicho chama kwa sasa? kama unataka kutunga kitabu cha historia ya vyama swali lako lingekuwa la msingi sio kwa maana ya kujiunga.
 
Shukrani kwa wote waliochangia.

Inapoitaja CUF, huwezi acha kumtaja Prof. I. Lipumba, Seif Sharif, n.k

Unapoitaja UDP, hakika huwezi acha kumtaja Mzee J. Cheyo, n.k

Unapoigusa CCM, lazima uanze na TANU + Afroshiraz, na waasisi wake kama Baba wa Taifa, Kawawa, Bibi Titi, Karume, Seti Benjamin, n.k

Kwanini, hamuokenani kukubali kutizama nyuma ya pazia la CDM.

"Tell me your friend, and will tell you................"

Umewajuaje viongozi au waasisi vyama vingine halafu ushindwe kuwajua wa CDM? wewe ni shabiki tu ndo maana unatafuta sura za watu na si sera. Watu makini hujiunga na vyama kwa kuangalia sera na itikadi ya vyama na kujiridhisha kwamba wanatekeleza lakini wafuata mkumbo kama wewe huangalia nani yuko ndani ya chama, je huyo unaemtaka akihama chama utamfuata au huyo usiemtaka akihamia chama ulichopo nawe utahama? swali lako ni fyongo.
 
Nenda chadema kuna wapinga ufisadi wa kweli. CCM kuna mafisadi haswa. Wapo chenge, Lowasa Rostam ambao ni wajumbe wa NEC hadi sasa ninapoandikia email hii. NEC ina maamuzi makubwa kuliko CC.
 
Nakushauri utembelee Website yao na kujionea kila kitu kule kuanzia waasisi, katiba na mwelekeo wao lakini vle vile kama utakuwa na suala lolote bsi utauliza kule na kujiridhisha na unachohitaji.
 
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama mbadala kinachokua na kinachoongozwa kwa Falsafa ya “Nguvu ya Umma” na kuamini katika itikadi ya “Mrengo wa Kati”. CHADEMA inawataka watanzania kuelewa kwamba mabadiliko ya kweli yataletwa na kubadilisha mfumo wa utawala. Maendeleo ya kweli hayawezi kuletwa na mafisadi walewale wa chama kile kile chenye uoza ule ule wakiendeleza yale yale kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. CHADEMA inatambua kwamba kwa falsafa ya Chukua Chako Mapema (CCM), Tanzania yenye neema kamwe haitawezekana. Lengo la CHADEMA ni kusimamia mabadiliko ya kweli na uhuru wa kweli ili kuunda Taifa la watu walio huru na lenye kuzingatia misingi ya utawala bora na linalotoa fursa kwa wananchi wake kushiriki katika kuboresha maisha yao. Tanzania endelevu, yenye haki na isiyovumilia ukandamizaji wa aina yeyote kwa wananchi wake-ndiyo nchi tunayoitaka. CHADEMA inafanya kazi kuhakikisha kuwa vyombo vya utawala na viongozi wanafanya maamuzi ya busara na makini yanayowaletea wananchi nafuu ya maisha na kuwapa matumaini ya kuendelea kupiga hatua za kimaisha katika nyanja zote za maendeleo.


Falsafa ya Chama CDM​
  1. Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika “Nguvu na Mamlaka ya Umma” (The People’s Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.
  2. Aidha falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.
  3. Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.
  4. Historia inaonyesha kuwa “UMMA” wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.
  5. CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka “Nguvu ya Umma”. Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.
  6. CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa “kuchaguliwa” kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza “waliowachagua” kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
  7. Hivyo basi, falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.
  8. Falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.
Sasa tafuta za vyama vingine:hug:
 
Ulivoangalia walio nyuma ya hivyo vyama umegundua nini. Na kama unataka kujua walionyuma ya cdm nenda kwenye website yao au nenda makao makuu ya chama
 
jamani kama hamjui ni bora mseme ili huyu jamaa ajue wapi akatafute haya anayohitaji. anauliza swali kama kuna mjuzi amwambie.
Hili lituma ila nalisema, nilipokua kidato cha nne niliwahi kumuuliza mwalimu wangu wa history swali fulani darasani kwa nia ya kujua na wenzangu kwani lilikua limetushinda darasa zima tuna maoni tofauti, badala yake niliambulia matusi na kuambiwa najifanya mjuzi sana wa kuuliza na kilichofuata mwalim yule alinichukia. sasa mbona kwa anaejua majibu hutoka haraka sana. ili aulizwe lingine ajibu. nini hofu ya kujibu swali la kwanza ? au kunaogopwa swali litalofatia ? ushauri wangu hata mimi sijui ila naomba anaejua ampe jibu na tusojua tuache kumtukana na kumpa lugha za kejeli.
 
Ndugu wana JF

Ninahitaji kujiunga na chama cha siasa hapa kwetu. Lakini, kabla sijafanya maamuzi ni chama kipi nijiunge nacho, inanibidi nitizame nyuma ya pazia la kila chama cha siasa hapa nchini "lifting of the vail".

1. Nilipofunua pazia la TLP na NCCR-Mageuzi, nikamkuta Mh. Lyatonga Mrema, n.k

2. Pazia la CCM: Niwewakuta waasisi akina Baba wa Taifa, Mzee Karume, n.k

3. C.U.F nimewakuta akina Prof, n.k

4. Naomba kujua ni nani na wako wapi waasisi wa CHADEMA?

Nisaidieni, maana ninataka kujiunga na chama cha siasa haraka iwezekanavyo

wewe ni mtanzania??

haiingii akili unajua waanzalishi wa vyama vyote hapo juu lakini umeshindwa kujua Chadema??

inabidi ukafanye upya utafiti wako, vinginevyo kuna jambo unatafuta....na utalipata
 
Ndugu wana JF

Ninahitaji kujiunga na chama cha siasa hapa kwetu. Lakini, kabla sijafanya maamuzi ni chama kipi nijiunge nacho, inanibidi nitizame nyuma ya pazia la kila chama cha siasa hapa nchini "lifting of the vail".

1. Nilipofunua pazia la TLP na NCCR-Mageuzi, nikamkuta Mh. Lyatonga Mrema, n.k

2. Pazia la CCM: Niwewakuta waasisi akina Baba wa Taifa, Mzee Karume, n.k

3. C.U.F nimewakuta akina Prof, n.k

4. Naomba kujua ni nani na wako wapi waasisi wa CHADEMA?

Nisaidieni, maana ninataka kujiunga na chama cha siasa haraka iwezekanavyo

The Following User Groaned at You Nyami2010 For This Awful Post:
Sigma(Today)
 
hivyo vyama vingine ulivijuaje waasisi wake mpaka ushindwe kujua waasisi wa CDM km sio majungu??? au wewe muimba taarabu nini?
 
wewe kamtafute mtu anaitwa Fahami Dovutwa ndio atakuelekeza kama atakuingiza kwenye chama chake ambacho ni tawi la chama cha magamba.......au muone Luteni Makamba anaweza kukushauri kwakuwa unafanana nae mawazo.......:rip:CCM.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom