Ndugu wana JF
Ninahitaji kujiunga na chama cha siasa hapa kwetu. Lakini, kabla sijafanya maamuzi ni chama kipi nijiunge nacho, inanibidi nitizame nyuma ya pazia la kila chama cha siasa hapa nchini "lifting of the vail".
1. Nilipofunua pazia la TLP na NCCR-Mageuzi, nikamkuta Mh. Lyatonga Mrema, n.k
NCCR sio Mrema bali ni: Mabere Marado, Christopher Mtikila, James Mbatia, Prince Bagenda, Dr. Ringo Tenga, Nindi Chimoto, Ndimara Tegambwage, Anthony Komu, Kibibi Senyagwa, Joseph Selasini, Evodius Mmanda, etc.
TLP sio MREMA bali ni Leo Lwekamwa na wenzake.
2. Pazia la CCM: Niwewakuta waasisi akina Baba wa Taifa, Mzee Karume, n.k
3. C.U.F nimewakuta akina Prof, n.k
CUF sio Lipumba bali ni James Mapalala, Alec Chemponda, Kashaju Bazigiza, Kasanga Tumbo, n.k
4. Naomba kujua ni nani na wako wapi waasisi wa CHADEMA?
Nisaidieni, maana ninataka kujiunga na chama cha siasa haraka iwezekanavyo