CHADEMA ngoma mbichi Arusha

Kama hata katiba ya Chadema huna hizo imani zinatoka wapi.........wewe endelea tu kuwa na imani zako.
 
Hongera CC Chadema kwa kuonyesha mfano wa kutoa maamuzi magumu, hakuna anayemiliki CDM bwana! Tatizo hapa siyo kurudisha seats ila kuondoa majambawazi ndani ya chama
 


Nimekuwekea link ya katiba ya CHADEMA huko juu kama hukuiona hii hapa tena Gonga hapa

nainaonekana kama hujui kilichotokea kwenye sakata hili hebu msome Dr. Slaa hapa chini…

 
Yaani kwa kweli, ninaombea sana ishu ya madiwani Arusha isije kuvuruga CDM, wananchi waelewe tu kwamba chama hakiwalei watu wanaokiuka utaratibu na kufanya mambo kinyume na utaratibu tuliojiwekea!
 
Chadema walitenda haki kuwaondoa magamba yaendelee kutapatapa wataishia tum na magamba yao waende CCM sasa wakatetee ugamba wao.Chademe juu na chama tawala 2015.
 
Swala la wao kwenda mahakamani ni kupoteza muda ili angalau waendelee kula bata kidogo kwa tiketi ya cdm. Ukweli ni kwamba mahakama haiwezi kutengua maamuzi yaliyofanyika kwa mujibu wa katiba!
 
Kwa uchanga wa fikra, inaonekana kama ngoma mbichi, lakiini chama chochote kisichozingatia kanuni, hupoteza dira. Kumbuka maneno ya Kolimba. Hagereni sana CDM kutoa picha ya good ledership (Not good governance).
 
Shughuli ya Arusha ni nzito, CDM hawawezi kutetea viti vyote hivyo. Madiwani walichagliwa kw anguvu ya Umma, leo wanatolewa kwa nguvu ya CDM CC.

Hapa umegonga penyewe hasa. Viti 5 vya madiwani wameshavikosa maana vyote vitarudi CCM. Ile nguvu ya umma iliyowachagua mbunge Lema na hao madiwani si nguvu ya CHADEMA au Dr Slaa, ingekuwa hivyo CHADEMA kingeshinda nchi nzima. Ni nguvu ya watu wa Arusha, ambayo akina Slaa na Mbowe wameamua kuipuuza. Elimu ni ghali.
 
Karibu kesho kwenye mkutano wa CDM.
 
Nimesoma tena sakata zima nimegundua kuwa bado Kamati kuu ya CHADEMA iko sahihi katika uamuzi wake wa kuwafukuza madiwani hao uanachama kwa utovu wa nidhamu.

Madiwani hao 5 wamedhihirisha kuwa hawasimamii tena msingi ambao chama chao kiliweka kuhusu suala hili, kwa hiyo hawawezi tena kuendelea kuwa ndani ya chama hicho. Kwa bahati mbaya, bado itawagharimu CHADEMA kukosa viti hivyo.
 
Karibu kesho kwenye mkutano wa CDM.
Makamanda wameshaanza kuingia na leo watafanya mikutano kwenye kata zifatazo Elerai atakuwepo wenje na makamanda wengine, Kimandolu sijajua nani atakuwepo huko, Mjini kati atakuwepo Tundu Lisu na wabunge viti maalumu....ila kazini ni kesho hapo NMC
 
Swala la wao kwenda mahakamani ni kupoteza muda ili angalau waendelee kula bata kidogo kwa tiketi ya cdm. Ukweli ni kwamba mahakama haiwezi kutengua maamuzi yaliyofanyika kwa mujibu wa katiba!

hata wao vile vile watakwenda kudai kuwa wameondolewa uanachama wao na kuona kuwa katiba ilikiukwa.

Ndio maana kuna mahakama ambayo inatoa haki kwa pande zote kuleta hoja na kisha mahakama inatoa haki kwa upande mmoja.

wana kila haki ya kwenda mahakamani kudai haki yao walioporwa.
 
Kama hata katiba ya Chadema huna hizo imani zinatoka wapi.........wewe endelea tu kuwa na imani zako.

Kutokana na kusoma tamko lililotolewa la kuwavua uanachama madiwani hao. Kimsingi na Elimu yangu hafif ya Sheria naona kuna mengi sana yamekiukwa na wana nafasi kubwa sana kuwashinda kama watawapeleka mahakamani.

Kwenye katiba ya CHADEMA nilitaka kuona kipengele kimoja tu cha KUFUKUZWA UANACHAMA ili niweze kutoa comment zangu kwa uhakika ingawa kwa aina yoyote wana nafasi kubwa kuwashinda mahakamani kutokana na mazingira na hoja hafifu zilizotumiwa na CC ya Chadema kuwaengua.
 
Bwana Kithuku

Nimependa jinsi ulivyojifahamisha muda mfupi na kuweka tena mawazo mapya baada ya kusoma! Nahisi mara nyingi watu wengi tunakuja na judgements kabla ya kujiridhisha na kile tunacho-conclude.

Binafsi pamoja na kwamba si mwanachama wa chama chochote cha siasa ni mpenzi wa CDM. Hata hivyo nilifurahishwa na kipindi kilichotumika kwa CDM kufatilia mzozo huu kabla ya kuja na maamuzi haya. Sidhani kama CDM CC hawakufanya uchambuzi wa kutosha (kisheria na kimadhara kuhusu kata hizo) kabla ya kuja na maamuzi ya kuwafukuza. Yumkini kila aliyesoma yale ambayo Dr Slaa aliandika kuhusu chanzo cha mgogoro atajua CC ya CDM wanajua athari za maamuzi yao, na pengine inaweza kuwa ni spring-board to higher levels of political win.
 

Rudini CCM there is only where you are allowed to be stupid, msitupotezee muda!
 
Rudini CCM there is only where you are allowed to be stupid, msitupotezee muda!

ni chama kimoja tu chenye uerevu na kutetea wanyonge hawa waliionewa na CDM. Ni CCM please tunawaomba muwapokee hawa watumishi wema ili waende kwa kasi zaidi nguvu zaidi na zaidi.

Hivyo basi warudi CCM watarudisha diwanii zao na kujenga A town. kwa kweli kule wasihangaike hakuwafai kabisaa na kesi futeni watapoteza muda tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…