acha tusitete hata kata moja lakini heshima itakuwepo...wewe ni sawa na Mwanaume unamfuma mkeo analiwa na jamaa halafu unasita kutoa maamzi kisa utapata wapi mke mzuri kama yeye....Shughuli ya Arusha ni nzito, CDM hawawezi kutetea viti vyote hivyo. Madiwani walichagliwa kw anguvu ya Umma, leo wanatolewa kwa nguvu ya CDM CC.
Madiwani watano wa CDM, waliovuliwa uanachama na Kamati kuu ya chama hicho mwishoni wa wiki iliyopita wanakwenda mahakamani kupinga uamuzi huo.
Diwani wa Kata ya Elerai, John Bayo, alieleza kwa njia ya simu akiwa njiani kutokea Dodoma walipokwenda kuhojiwa kabla uamuzi wa kutimuliwa kufikiwa.
Bayo alisema kabla ya kuchukua uamuzi wowote watazungumza na wapiga kura kwenye kata zao kuwaeleza yaliojiri na kuacha nafasi ya uamuzi wa hatua zinazostahili mikononi mwa umma uliwaamini na kuwapa dhamana yb uongozi.
"Binafsi sina kinyongo na chama changu nimepokea nimepokea uamuzi huo, lakini nakuhakikishia nitaendelea na nafasi ya udiwani hadi uchaguzi mkuu ujao, kuna njia nyingine ya kupinga uamuzi huo kupitia vikao au mahakama" alisema Bayo.
SOURCE: Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongoza
8 August 2011
Mimi namweshimu sana crashwise kwa jinsi anavyotuletea habari za AR lakini siku za hivi karibuni anaonekana kama kaumizwa na kitendo cha madiwani kufuzwa ila bado anajitahidi sana ku balance habari asionekane yuko upande gani.
kwa ujumla nimefurahia sana na maamuzi ya chadema! ilikuwa hakuna njia nyinggineMaamuzi haya ndiyo tuliyasubiri kwa muda mrefu, ni maamuzi makini na yenye nia ya kujenga kitu ambacho kimekosekana hapa nchini, ni maamuzi yanayolenga kuipeleka nchi kwenye utawala wa kufuata sheria na uwajibikaji.
Kwa Maamuzi haya napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa CC ya Chadema, mmefanya kile ambacho wengi tulitaka kukisikia, na ieleweke hakuna mtu muhimu kuliko chama kwa maendeleo ya taifa hili, na pia ieleweke hata kama uchaguzi ukirudiwa na ukafanyika kwa haki na kufuata taratibu na sheria na ccm wakashinda kata zote itakuwa sawa kuliko kubakia na watu waliowarafi wa madaraka na kama ikitokea hivyo yatakuwa ni maamuzi ya wana wa A town. lakini ninaimani na wana A town na ngoja tusubiri uchaguzi na kata zote zitarudi Chadema.
na ikithibitika kwamba Meya aliyeingia office kwa kuvunja taratibu amehusika katika kuwa rubuni tuwajulishe magamba nao waone ukweli na wafanye maamuzi magumu kama wataweza.
Ni wewe wasema! Tuliwachagua kwa kudhani ni watu kumbe ni viatu! Subiri uchaguzi ufanyike ndo utaelewa maana yake!
Si kweli kabisa, Habari ya Arusha ndo imeshaisha vizuri kabisa na pengine itaiongezea sifa Chadema kama ilivyoripotiwa leo na baadhi ya magazeti. Hivi hawa madiwani wakikodi magari na kutoa matangazo ya mkutano wao, watasemaje? Maana hawawezi tena kutumia jina la Chadema.
Ama watatumia majina yao?
Sikutegemea John Bayo niliyemfahamu japo kidogo angefanya uamuzi wa kitoto namna ile. Am very sorry for him.
Hakika hao madiwani ni majasiri sana na wanasiamamia yale waliokubaliana hivyo hawamo katika kundi la wanafiki kama alivyo Mbunge wao Lema na madiwani wengine waliokuwa vigeugeu.
Sina tu katiba ya Chadema lakini nina hakika wakienda mahakamani kudai haki yao ya kuondolewa uanachama wao na sababu walizotoa CC ya Chadema nina imani watarudishwa kwa amri ya mahakama na kuendelea na udiwani wao.
lakini vile vile nina imani kama uchaguzi utafanyika katika kata zote hizo tano CCM watachukua kata zote kwani wananchi wamechoshwa na malumbano kila siku bali wanataka maendeleo. na hapo sasa kutakuwa hakuna haja ya muafaka baina ya CCM na Chadema.
Lakini vile vile 2015 Godbless lema hawezi pewa Ubunge hapo Mjini Arusha. Kwani ameonyesha ni dhaifu sana na hana ushirikiano na madiwani wake hivyo hawezi kuwaletea maendeleo watu wa mjini Arusha,
.
Sina tu katiba ya Chadema lakini nina hakika wakienda mahakamani kudai haki yao ya kuondolewa uanachama wao na sababu walizotoa CC ya Chadema nina imani watarudishwa kwa amri ya mahakama na kuendelea na udiwani wao.
,
Ukimtaliki mkeo mahakama ina haki ya kulazimisha awe mkeo?
- Kusimamia kituambacho si cha msingi ni wendawazimu…
- katiba ya chadema Hii hapa
- Hata tukibaki na diwani mmoja tutadai uchanguzi utakaofata kanuni na sheria..
- Mbunge ameonyesha hana ushirikiana kwa lipi kutokwenda kuchukua wagonjwa wa kata za madiwani wake na kuwapeleka kwa Babu Loliondo…haha
- Godbless Lema bado ananguvu kuliko unavyodhania na kama huamini njoo alhamisi makamanda watakapo kuwa Arusha…..
Kaka Hope ni mweji Arusha,Mimi mgeni na nina siku kama Mbili mjini hapa na nimekuwa nikiongea na watu tofautitofauti, na kuna mtu kaniambia kuwa DIWANI wa KITI MAALUMU Kafungua DUKA la HARDWARE KUBWA HAPO TOWN kwa hizo hela za RUSHWA, Je wewe unasemaje kuhusu hilo?