Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama vilivyo vyama vingine bila ya shaka kimekuwa na mipango ya vitega uchumi ili kiweze kujiendesha na kufadhili shughuli zake mbalimbali bila ya kutegemea sana ruzuku au misaada ya wafadhili. Je, Chama hiki sasa hivi kina miradi gani kitega uchumi, yenye kuingiza faida gani, na inasimamiwaje? Au ndio "hatuna fedha ya kutosha, ruzuku yenyewe kidogo, na CCM wao wanajichotea mabilioni".
Je, Chadema imeweza kuanzisha sekondari moja ya Chama ikajionesha kuwa ni nzuri na ikashindanishwa na sekondari nyingine binafsi na za serikali?
Je, Chadema imeweza kuanzisha Kliniki au hospitali fulani ya Chama kwa ajili ya wananchi n.k
Je, Chadema imeshikiri vipi katika harakati za kusafisha jiji la Dar na kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu kwa kutoa mafunzo n.k?
Je, Chadema imeweza kujenga jengo lolote ambalo ni la kisasa na wakaweza kulipangisha kama kitega uchumi?
Je, Chadema wameweza kuanzisha kampuni ya kibiashara ambayo iko chini ya Chama na kuonesha jinsi wanaweza kusimamia miradi hiyo?
Je, CHadema ina vitega uchumi vipi kama Chama vinavyoonesha uwezo wa kusimamia miradi, kupanga, na kudhibiti mapato na matumizi zaidi ya fedha zinazoingia kwenye chama kupitia michango, ruzuku na misaada?