Mwan mpambanaji
JF-Expert Member
- Apr 3, 2008
- 482
- 131
Tatizo la msingi la nchi hii ni watu kupenda udaku zaidi ya kufikiri,mwiba umeprove kuwa wewe ni mpenda udaku na mtu usiependa kufikiri,cdm wapo makini na wataendelea kuwa makini,,
Chama kinaongozwa na watu ambao hawakusoma;
M/Kiti ni DJ na katibi mkuu ni Askofu, unategemea nini kwenye chama hicho zaid ya kukurupuka ?
very interesting, hapo kwenye RED wewe na huyu mkwere wako hapa chini hamna tofauti
View attachment 20950
Ila baada ya Mkwere kugunduwa Chadema ni chama makini, sasa anajipanga kuhamia Chadema na hapo ameshaanza kufanya mazoezi ya ishara ya Chadema ili akishamaliza kuisambaratisha CCM akiingia Chadema asiwe mgeni, ila kazi ya kuiuwa ccm bado hajaimalizia ndio maana ameanza mazoezi, jionee mwenyewe hapo.
View attachment 20951
Chama kinaongozwa na watu ambao hawakusoma;
M/Kiti ni DJ na katibi mkuu ni Askofu, unategemea nini kwenye chama hicho zaid ya kukurupuka ?
chama kinaongozwa na watu ambao hawakusoma;
m/kiti ni dj na katibi mkuu ni askofu, unategemea nini kwenye chama hicho zaid ya kukurupuka ?
Tarehe: 19 Jan 2011
Chadema na ulimbukeni
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/104573-chadema-na-ulimbukeni.html?highlight=
Tarehe: 16 Jan 2011
Hongereni Chadema
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/103344-hongereni-chadema.html?highlight=
Tarehe: 12 Jan 2011
Tuelekeako na Chadema tutafika
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...afika-tu-but-the-price-is-high.html?highlight=
Kama si ulimbukeni ni nini.
Mwiba, ujumbe unaotaka kuufikisha ni kama ifuatavyo;
1. CDM wajipange kwa kila jambo wanalosimamia. Chochote watakachokisema ni lazima wahakikishe wanakisimamia mpaka mwisho. Kama ni kauli bungeni basi wahakikishe wanaisimamia mpaka majibu yapatikane.
2. CDM wakipinga kitu wasirudi nyuma. Wasikubali kubadili msimamo mpaka kieleweke kama ilivyo kauli yao.
3. CDM wasiwe kama CUF kukubali kurudi mezani kisa wameahidiwa nafasi za uongozi. Pia wasikubali kuungana na CCM kwa jambo lolote.
4. Viongozi wa CDM waendeleze mapambano bila kuogopa vitisho na vipigo vya polisi. Wawatie ujasiri watanzania kudai haki na wao waendelee kuwa mstari wa mbele katika kusimamia mapinduzi ya kudai haki.
Mimi nawahasa wanajamii mliokuwa makini huyu ni TUNTU ANAYE BEEP NA PRIVATE NUMBER!msameheni bure!kwani mbuzi mwovu akichunga na mbuzi mwema hata mwema ugeuka kuwa mwovu!!hivyo yeye hawezi kiona viongozi vilaza niwapi!ila kaona wa chadema!
hapo umesema mkuu...kuna chama chenye mbumbumbu kama cha mafisadi? kama unadhani makamba na mkwere ndo top scholor wa tuttuwape mdaharo basi wa m/kiti na katibu wa vyama hivi viwili kama watakubali. Subutu makamba hata umfunge kamba hatii timu na nundu yake ya uso. Mkwere mtamsababishia apoteze fahamu bure!.
Kama ni kuwa limbukeni basi nionavyo Chadema wa... Kweli mkuu,limbukeni huwa ni noma,akipata facts halazi damu,acha wa shamba aitwe mshamba! Limbukeni na mshamba wasingekuwa wa ajabu tuchukulie mfano limbukeni wa kichaga,kinyakyusa na kisukuma wanavyomwamisha mzaramo na mmakonde kariakoo,full kuwatoa nduki na kariakoo mzaramo ataenda kutembea. Kwa sasa mzaramo mwenye mji na mmakonde amefikishwa magomen analipwa na kutolewa nduki. Ivo ivo chadema uliyemwita limbukeni na wakuja ndo anavyomtoa nduki mkwere,ccm. Kashamlipa na kumwamisha karatu,arusha ,moshi,mwanza,musoma,kagera,kigoma,mbeya n.k. Sasa mzaramo,ccm amebaki pwani,ikiwemo magogoni. Punde si punde uyu limbukeni ana mpango wa kumwamisha magogoni ili uyu mzaramo,ccm abakie msoga. Pia limbukeni mwingine CUF kashamtoa zanzibar mzaramo,ccm kwa %49.1 kwa 51.1%. Jamani mwambie uyu mzaramo,ccm aende shule,japo asome tu nyakati ndo aelewe kuwa muda wake magogoni na zbar unahesabika.
Hahahahahahaaa kweli huyu ni tuntu.
Ana beep na private number halafu anaomba kupigiwa!! kazi kweli kweli.
Kama ni kuwa limbukeni basi nionavyo Chadema wanaelekea huko kwani mengi wayafanyayo inakuwa kama ni mambo ya Mshamba ,inasemwa mshamba kaingia mjini.
Ukiangalia mambo ya Chadema utaona hayalingani ni mambo yanazuka kisha husikii kitu kimya ,Chadema walikuja na mizinga sijui wenyewe wanaita mabomu bungeni yakiozwa na kiongozi walimwita mpambanaji ,mabomu sijui maguruneti yao yalitikisa nchi na kuona sasa hivi nchi itapata Chama tawala kipya,lakini wapi yamepita na yaliobakia ni mapovu tu ,hakuna faida hata moja iliyopatikana hadi hii leo ,kama ipo tuambieni ni faida gani ,tokea mzushe hoja bungeni hadi hii leo ,kipi kimejiri huko bungeni ?
Sasa inaonekana kama Chama kinachochochea fujo katika Taifa hili la Tanzania kwani hawasimamii hoja zao ,wanakuwa kama kinyonga wanabadilika badilika ,leo wanasema hivi baada ya sikumbilitatu inakuwa kama sio wao ,wanazusha jipya ,yaani ni watu wa ajabu ajabu kabisa.
Baada ya Uchaguzi mkuu ,Chadema walishindwa vibaya sana ,kinyume na matarajio yao kuona hivyo ,wakazuka ghafla kuwa hatumtambui ushindi wa Kikwete na hata kwenye kikao Cha bunge wakasusia ,hii ilikuwa kuonyesha msimamo wao kuwa hata serikali hawaitambui ,hatukuona usimamiaji wa hoja yao hiyo kuwa CCM haikushinda uchaguzi na Kikwete sio Raisi halali wa nchi ,na leo hii humsikii yeyote yule kujaribu angalau kugusia tu kuwa Kikwete sio Raisi halali ,hakuna hata mmoja mwenye ubavu wa kutamka hayo hadharani ,sasa hivi wamefulia maana wameshindwa kuendeleza msimamo wa kutomtambua Raisi hata kwa mwezi mmoja.
Juzi juzi wanazua hoja ya kuporwa umeya wakati walizidiwa akili ,wakaitisha maandamano yasiokubalika na vyombo vya ulinzi ,matokeo yake tumeyaona ,yanasikitisha na yanatia huruma, hoja yao ya kusema uchaguzi ulikuwa una mizengwe haikuendelea ,mahakamani hatukuwaona kufikisha madai,inamaana walipelekesha watu kupambana na vyombo vya dola wakati hawana mipango endelevu ,misimamo yao inafia njiani na kuwaacha wananchi solemba.
Labda tuangalie misimamo ya CUF ,utaona hawakumtambua Raisi kwa miezi mnayoijua nyinyi ,hawakuingia kwenye vikao vya uwakilishi kwa miezi mnayoijua nyinyi ,walipinga mambo ya muafaka wa Butiama kwa marefu na mapana na walisema hawatorudi mezani na kweli hawakurudi walisimamia msimamo wao ,sasa hapa mwananchi mwananchama wa kawaida unapata moyo na kutoa sapoti ya hali na mali ikibidi maisha ili kudumisha msimamo wa Chama Chako na unaitikia mwito ukijua Chama kipo nyuma yako ,na hii imetokana na kuwa viongozi wanamsimamo uliothabiti na wanaousimamia na kuuendeleza hadi madai yatekelezwe au serikali ikubali kukaa mezani na kupatikana muafaka japo baadae utavunjika ,lakini serikali imewajibika.
Chadema (Viongozi) sivyo walivyo hawasimamii maelekezo na misimamo yao naweza kusema wanayumba na baada ya kutokea patashika hawaonekani kutetea hoja yao iliyosababisha purukushani.Hivyo ulimbukeni waliokuwa nao ni ule wa kufanya mambo ambayo kwao yanakuwa kama ndoto ,unaamka asubuhi kumekucha nayo imeshapita.