CHADEMA na ulimbukeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA na ulimbukeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jan 20, 2011.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kama ni kuwa limbukeni basi nionavyo Chadema wanaelekea huko kwani mengi wayafanyayo inakuwa kama ni mambo ya Mshamba ,inasemwa mshamba kaingia mjini.

  Ukiangalia mambo ya Chadema utaona hayalingani ni mambo yanazuka kisha husikii kitu kimya ,Chadema walikuja na mizinga sijui wenyewe wanaita mabomu bungeni yakiozwa na kiongozi walimwita mpambanaji ,mabomu sijui maguruneti yao yalitikisa nchi na kuona sasa hivi nchi itapata Chama tawala kipya,lakini wapi yamepita na yaliobakia ni mapovu tu ,hakuna faida hata moja iliyopatikana hadi hii leo ,kama ipo tuambieni ni faida gani ,tokea mzushe hoja bungeni hadi hii leo ,kipi kimejiri huko bungeni ?

  Sasa inaonekana kama Chama kinachochochea fujo katika Taifa hili la Tanzania kwani hawasimamii hoja zao ,wanakuwa kama kinyonga wanabadilika badilika ,leo wanasema hivi baada ya sikumbilitatu inakuwa kama sio wao ,wanazusha jipya ,yaani ni watu wa ajabu ajabu kabisa.

  Baada ya Uchaguzi mkuu ,Chadema walishindwa vibaya sana ,kinyume na matarajio yao kuona hivyo ,wakazuka ghafla kuwa hatumtambui ushindi wa Kikwete na hata kwenye kikao Cha bunge wakasusia ,hii ilikuwa kuonyesha msimamo wao kuwa hata serikali hawaitambui ,hatukuona usimamiaji wa hoja yao hiyo kuwa CCM haikushinda uchaguzi na Kikwete sio Raisi halali wa nchi ,na leo hii humsikii yeyote yule kujaribu angalau kugusia tu kuwa Kikwete sio Raisi halali ,hakuna hata mmoja mwenye ubavu wa kutamka hayo hadharani ,sasa hivi wamefulia maana wameshindwa kuendeleza msimamo wa kutomtambua Raisi hata kwa mwezi mmoja.

  Juzi juzi wanazua hoja ya kuporwa umeya wakati walizidiwa akili ,wakaitisha maandamano yasiokubalika na vyombo vya ulinzi ,matokeo yake tumeyaona ,yanasikitisha na yanatia huruma, hoja yao ya kusema uchaguzi ulikuwa una mizengwe haikuendelea ,mahakamani hatukuwaona kufikisha madai,inamaana walipelekesha watu kupambana na vyombo vya dola wakati hawana mipango endelevu ,misimamo yao inafia njiani na kuwaacha wananchi solemba.

  Labda tuangalie misimamo ya CUF ,utaona hawakumtambua Raisi kwa miezi mnayoijua nyinyi ,hawakuingia kwenye vikao vya uwakilishi kwa miezi mnayoijua nyinyi ,walipinga mambo ya muafaka wa Butiama kwa marefu na mapana na walisema hawatorudi mezani na kweli hawakurudi walisimamia msimamo wao ,sasa hapa mwananchi mwananchama wa kawaida unapata moyo na kutoa sapoti ya hali na mali ikibidi maisha ili kudumisha msimamo wa Chama Chako na unaitikia mwito ukijua Chama kipo nyuma yako ,na hii imetokana na kuwa viongozi wanamsimamo uliothabiti na wanaousimamia na kuuendeleza hadi madai yatekelezwe au serikali ikubali kukaa mezani na kupatikana muafaka japo baadae utavunjika ,lakini serikali imewajibika.

  Chadema (Viongozi) sivyo walivyo hawasimamii maelekezo na misimamo yao naweza kusema wanayumba na baada ya kutokea patashika hawaonekani kutetea hoja yao iliyosababisha purukushani.Hivyo ulimbukeni waliokuwa nao ni ule wa kufanya mambo ambayo kwao yanakuwa kama ndoto ,unaamka asubuhi kumekucha nayo imeshapita.
   
 2. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  mwiba na pumba zako kalale ..hujui kesho shule
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  UMEPOTEZA MUDA WAKO KUANDIKA CRAAAAAAAAAAAAAAAAP

  POLE KWA MUDA WAko
   
 4. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  mwiba.. yaani bandiko bovu namna hii halafu bado wana JF wanasema ni crap... nasikitika sana
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Aheri ya ULIMBUKENI wa kudai haki ya wanyonge na kutafuta kulinda maslahi ya taifa kuliko kujaa ndani ya suti ya STAARABU WA CCM huku ukidhulumu hadi akina Matonya mitaani na kuwaua wenzao kibao wakidai maelezo jinsi kodi zao zinavyotumika kulipa maruani kama akina Dowans.
   
 6. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,066
  Trophy Points: 280
  Crap,
  hivi wewe huwa huna jingine kichwani lenye maslahi ya taifa zaidi ya habari za Chadema?, juzi umewasifia CDM haijapita hata siku moja leo wamekuwa limbukeni mbaya zaidi ni kwa habari zilezile naona wewe ndiye limbukeni wa Chadema, jiangalie mwisho CDM itakufanya uonekane chizi JF.
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nyinyi wengine ufinyu wenu wa kufahamu unawapa tabu,lakini nina uhakika kabisa kiongozi wako akisoma atafahamu kwa kina kilichokusudiwa na bila ya shaka yeyote ile ,muda si mrefu utaona ni jinsi gani Chadema watakavyokuwa waangalifu na kauli zao na misimamo yao.
   
 8. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Tatizo lako Mwiba umekaa sana nje ya Nchi.

  Kama ulijilipua Usomali, pole sana.

  Ndiyo maana mnaota kila siku kuvunja muungano.

  Kwa sisi tulio Bongo, hiyo wala haitupi shida.

  Shida yetu ni Foleni, Mgawo wa umeme/maji, bei juu, ...................... Wewe pigwa tu baridi huko Majuu.
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mnajua Bin Ladin wa Alkaeda zamani alikuwa akionyweshwa kwenye TV akitoa hotuba zake kutoka secret location, Wamarekani wakasema asionyweshwe tena kwa sababu huwa anatoa viashirio vya ishara na wahusika wanazifahamu ,hivyo iwe ikitolewa audio tu bila ya kideo ,sasa ufunuo uliomo kwenye mada walengwa ndio wataelewa nyie pangu pakavu mtabakia na kupiga miayo tu.
   
 10. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  mwiba tunajua mahali ulipo na lengo lako... na tunatambua unazo siri nyingi unazo share na bin laden.... please usijeleta al qaeda hapa TZ... mafunzo unayoyafanya kajilipue huko huko... kunakojiri machafuko ... sio hapa... udini huo uaoutaka hapa kwetu haupo... sawa sawa
   
 11. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,066
  Trophy Points: 280
  Tarehe: 19 Jan 2011
  Chadema na ulimbukeni
  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/104573-chadema-na-ulimbukeni.html?highlight=

  Tarehe: 16 Jan 2011
  Hongereni Chadema
  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/103344-hongereni-chadema.html?highlight=

  Tarehe: 12 Jan 2011
  Tuelekeako na Chadema tutafika
  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/102153-tuelekeako-na-chadema-tutafika-tu-but-the-price-is-high.html?highlight=

  Kama si ulimbukeni ni nini.
   
 12. B

  Bull JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chama kinaongozwa na watu ambao hawakusoma;

  M/Kiti ni DJ na katibi mkuu ni Askofu, unategemea nini kwenye chama hicho zaid ya kukurupuka ?
   
 13. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  HACHANA NA HUYU PANZi
   
 14. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  neno la ukombozi kwao wanaopotea kama wewe mwiba ni upuuzi,ila kwetu sisi tunaoelewa lina maana kubwa,,sio lazima wewe uelewe sie twasonga ,mbele...stugle continues
   
 15. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mwiba, ujumbe unaotaka kuufikisha ni kama ifuatavyo;

  1. CDM wajipange kwa kila jambo wanalosimamia. Chochote watakachokisema ni lazima wahakikishe wanakisimamia mpaka mwisho. Kama ni kauli bungeni basi wahakikishe wanaisimamia mpaka majibu yapatikane.

  2. CDM wakipinga kitu wasirudi nyuma. Wasikubali kubadili msimamo mpaka kieleweke kama ilivyo kauli yao.

  3. CDM wasiwe kama CUF kukubali kurudi mezani kisa wameahidiwa nafasi za uongozi. Pia wasikubali kuungana na CCM kwa jambo lolote.

  4. Viongozi wa CDM waendeleze mapambano bila kuogopa vitisho na vipigo vya polisi. Wawatie ujasiri watanzania kudai haki na wao waendelee kuwa mstari wa mbele katika kusimamia mapinduzi ya kudai haki.
   
 16. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  very interesting, hapo kwenye RED wewe na huyu mkwere wako hapa chini hamna tofauti

  View attachment 20950


  Ila baada ya Mkwere kugunduwa Chadema ni chama makini, sasa anajipanga kuhamia Chadema na hapo ameshaanza kufanya mazoezi ya ishara ya Chadema ili akishamaliza kuisambaratisha CCM akiingia Chadema asiwe mgeni, ila kazi ya kuiuwa ccm bado hajaimalizia ndio maana ameanza mazoezi, jionee mwenyewe hapo.

  164713_186021948088433_100000418869866_584556_5893087_n.jpg
   
 17. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Kawasaidie wale watoto wa chama chako kuandika tamko.........waambie waende shule, watulie wakiwa wanataka kufanya jambo na wasiwe kama VICHECHE vywenye njaa...........vikitumwa vinaenda tuuuu!!

  Mwenyekiti wa CCM ni BA economics
  Katibu wa CCM ni mwalimu wa shule ya msingi

  Unataka kusema nini tena?
   
 18. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Hizi ndo akili za akina Mangungo wa Msovero. Never serious. Huwezi jua kama ni kichwa yake ni mtu. Full pumba
   
 19. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo hao ndio viongozi wote wa CHADEMA? Sawa kabisa. Umenena vizuri.

  Heri ya chama kinachoongozwa na Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Captain Yusuph Makamba. Heri ya chama kinachoongozwa na Prof. Ibrahim Lipumba na Shariff Hamad. Heri ya chama chako.

  Uongozi unaanzia kwenye maisha binafsi, jiulize viongozi unaowakubali wewe ambao hawakurupuki kwenye maisha yao wamewahi kufanikiwa nini!? Familia zao zimefanikiwa nini zaidi ya kuwa wanasiasa?

  DJ anamiliki biashara zenye mafanikio na kutambulika. Askofu ni Mwenyekiti wa CCBRT na ameendesha hiyo taasisi kwa mafanikio. Viongozi wako wamefanikiwa na nini?

  DJ na Askofu hawana mtoto anakula unga na kuvuta bangi, je viongozi wako?

  Mengine tuyaache utatafakari mwenyewe! Regards
   
 20. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #20
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  kuna chama chenye mbumbumbu kama cha mafisadi? kama unadhani makamba na mkwere ndo top scholor wa tuttuwape mdaharo basi wa m/kiti na katibu wa vyama hivi viwili kama watakubali. Subutu makamba hata umfunge kamba hatii timu na nundu yake ya uso. Mkwere mtamsababishia apoteze fahamu bure! Kaa kimya kama huana cha kuchangia mjomba!
  Ccm imebaki na mafisadi na watoto wao(uvccm/ kama wewe bado unajikomba huko na siyo mmoja wa hao imekula kwako. Kumbuka tunisia wamekamatwa wote waliokuwa viherhere wa wakifaidi Uchumi nyuma ya bin ali.
   
Loading...