CHADEMA na UKAWA tukubali ku surrender, hatukujipanga

CHADEMA na UKAWA tukubali ku surrender, hatukujipanga

Freeland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
14,481
Reaction score
10,233
Wadau;

Kati ya vitu ambavyo CHADEMA wamenikera ni wao kushindwa kuandaa mtu kwa ajili ya kugombea Urais mwaka 2015

Tangu mwaka 2010 walikuwa na muda wa kutosha kutengeneza mtu mpya kwa ajili ya position hiyo

Walikuwa na uwezo wote wa kufanya Poaching na kumpata mtu huyo

Lakini kwa Ubinafsi tu wa kudhani slaa anatosha ndio maana tuko hapa tulipo

Dr Slaa hana mvuto tena...hana kipya anachoweza kukisema kwa wananchi....watu wamemzoea sana.....kama Dr slaa akishindana na Magufuli ...Magufuli atashinda kwa asilimia 95,yaani 95%.

CCM wamejitahidi kupambana na mgogoro wa ndani ya chama chao na kukiacha chama salama....CCM wameonesha kiwango cha juu cha management ya kisiasa...kitu ambacho sisi tumekishindwa

CCM wako very organized....Tukibisha ni ubishi tu

Ushauri wangu..Tuweke silaha chini na tutoe matumaini kwenye Urais...Tuweke Concentration Kubwa kwenye Ubunge ili tupate Bunge lililo Imara

Tukiwa na Bunge Imara..Rais Mwenye Maamuzi...Tutafika Mbali
 
Umeongea la maana sana, huwa nikisema ukawa hawajajipanga watu wanatokaga povu na kutupa matusi ktk comments zangu, ila ukweli ndo huo! Na ukweli mchungu ila MAGUFULI anaenda kuigaragaza ukawa! Focus kwa ukawa sasa iwe ni kuongeza idadi ya wabunge bungeni ma pia kuanza kuandaa mtu/ watu mbadala wa chaguzi zijazo!! Slaa ni ku-force ila HANA mvuto!
 
Muda wote mlitumia kupambana na ACT sasa ndio mnastuka, tulieni dawa iingie, na mkimchagua Slaa lazima waliberali wajitoe ukawa, dah naziona dalili za kila mmoja kuchukua mbao yake na jahazi ikizama

Haa ha ha walidhani watakutana na mgombea dhaifu,sasa Bulldozer hilo, kanda ya ziwa imeondoka tayari kwenye equation za Chadema.
 
Dr slaa amekosaje mvuto?
Nachokijua mwanasiasa huwa anakosa mvuto kwa kashifa au kutekeleza ahadi zake je dr slaa unamuweka upande upi??
 
Unataka UKAWA wajipangaje? Kama kreti za bia au? Nani kakuambia Slaa amekosa mvuto? Ni lini umefanya utafiti na kupata data za ushindi wa Magufuli?

Tulia wewe acha kuweweseka..

Issue ya kukubalika kwa Magufuli huna ata haja ya kuuliza hapa, kaa na rafiki zako kumi kisha fanya hiyo kura ya maoni wewe mwenyewe,utaona!
 
Dr slaa amekosaje mvuto?
Nachokijua mwanasiasa huwa anakosa mvuto kwa kashifa au kutekeleza ahadi zake je dr slaa unamuweka upande upi??

Kwani Mrema aliishaje mvuto?Watanzania wanakinai maneno yaleyale kila siku.Sasa niambie Dr Slaa ana lipi jipya ambalo hakulisema 2010?
 
slaa mvuto umepungua,hata mikutano yake siku hizi haina impact sana.
mwachieni lissu apambane na magufuli...
 
slaa mvuto umepungua,hata mikutano yake siku hizi haina impact sana.
mwachieni lissu apambane na magufuli...

Mikutano mpaka amvizie gwajima jumapili pale ili aonekane anakubalika,
Kila zama na mtume wake
 
Hujui siasa, subiri uone kuna maajabu yanakuja....
Kamanda naona umeamua kujifariji kuna maajabu gani tena Dr.Slaa kuwa mgombea urais?

Muda wenu mwingi mnatumia kupambana na ACT-Wazalendo leo hii imebakia miezi mitatu tuingie kwenye uchaguzi unaleta drama.


Kila siku UKAWA wanajifungia watu wanne wanatoka bila maelewano maajabu ambayo watakuja nayo ni UKAWA kuvunjika na Kila mtu kuingia kwenye uchaguzi kivyake wapate kura mbili mbili na mwisho wa siku watasema usalama wa taifa wamewaibia kura.

Cc; Mkandara JokaKuu Kimweri
 
Last edited by a moderator:
slaa mvuto umepungua,hata mikutano yake siku hizi haina impact sana.
mwachieni lissu apambane na magufuli...

I agree with You

Lissu anaweza kuwa na Impact Kuliko Slaa
 
Mziki upo njiani subirini mtaona mapambano yanayokuja huko ukawa wataisoma namba hao CCM
 
Back
Top Bottom